Kuna wakati mtu unakosa maneno ya kuielezea dhana fulani kama nilivyokosa maneno ya kuuelezea ubora wako Lara 1... nilianza kufuatilia maandiko yako mwaka 2013. Nakumbuka zaidi ya robo tatu ya watu walikuwa wakikupinga na kukuona kama wakala wa shetani. Miaka mitatu mbele hakuna hata comment moja inayokupinga. Ni muda mfupi sana umefanikiwa kubadilisha mtazamo wa watu kukuhusu wewe.
Japo nilifurahia maandiko yako ila nilikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na mtazamo hasi kukuhusu ila leo mimi ni shabiki wako mkubwa, hongera sana. Huwa naandika stori huko fb, nina wadau wangu wananikubali ajabu, nawaza tu siku wakiijua jamiiforums na zaid wakakujua wewe, aisee biashara yangu itakuwa katika hali ngumu.