NO 4: The Trophy Wife.
I am the Trophy wife, the original trophy wife. Achana na Copycat humble wife kujiita trophy wife, geza geza tu. Hana lolote. Anajaribu wakati wenzie tunafanya kweli. Kwanza how can a one legged man have a trophy wife. Si maajabu ya dunia hayo. Only men like my man, strong, aggressive, gangstar men like hubby bae can afford trophy wifes. Atakuja kumuua captain Hooks kwa pressure nawaambieni.
Well i am a trophy wife in deed not just dellusionaly but i can back it up with a never ending designer collection ranging from handbags, shoes, dresses, shades. My closet is to die for. Only dirty money and dirty money only can afford that. Nashangaa Mume wa humble wife anakubalije huu upuuzi wa mkewe kushindana na stering kwa legit money.
Kila baada ya miezi 3 sometimes week 2, i change my car. And i love them fancy. The bigger, the more expensive the better. Naweza sema mimi ni black chyna wa bongo, only that mimi nina mume official. Not to mention extravagant parties nazofanya kila nikijisikia. I have thrown parties for nothing so many times until people never care any more to ask what is the occasion.
My homes maana sio moja are the most extravagant than any breathing soul in this story. And ihave multiple homes in the same city and arround the world. Nikisema niko home lazima niulizwe home wapi maana we have a mansion ununio, we have a luxury villa apartment Masaki. Nilienda to na strong wife akaniambia panauzwa, nikapapenda and i decided baby should buy it for me for birthday. Tuna appartment ingine posta, juu ya ofisi ya mume. Nisiwakaushe uzazi we have homes.
Let me not get started on my entire jewelry collection. I love them heavy, i love them big.Pia hii ni njia moja ya Mr. kutakatisha pesa haramu. Basi anaipa tu. Haina haja ya kuwa na event. Nimejaza kabati zima la vito vya thamani.
I have only one son, ila mume ana watoto wa 2 wa kike from his previous marriage wanaishi na maza wao. Na huyu mtoto nilimzaa kwa raha kama nazaa mfalme. Maana i had a personal Dr. 24hrs. Na kujifungua nilienda marekani, dogo akapata passport ndo nikarejea.
It has not been always this green. I had my share of dark sad and gloomy days. Acha kabisaaa. I am the teachers daughter. Unajua ukiwa mtoto wa mwalimu raha sana, although, dad was poor but he was respected. Watu wanamuita mwalimu mwalimu. Wana muamini na kumuheshimu sana. Wanamsikiliza. It is a humble job. Andsome how kuwa respected down town gave him some sort of balls he should not have.
Mara ya kwanza nakutana na hili gangstar, nilikuwa kwenye party, under dressed and out of place. Then i met him, all the girls were after him, and i was out of place. Then akaja akanisalimu na kuniomba namba. Nilidataaaa. Nikaona kweli na zaliii la mentaliii. Kesho akaniita kwao. Mi nikaenda sinajua napendwa vile vile out of place kama kawa.
I dont know why ila mimi kuwa pale ilimtibua tibua vuzi zote baba yake. As if kuna kitu kibaya nimefanya. The old man was rude and mean, the mom was nice. Ila ikaonekana kama wana some sort of conspiracy ya kifamilia ambayo nahusika afu sielewi kivipi. Mara maza amwambie mwanae tumemkomeshaa kabisaa. Wembe huu huu. In short sikuelewa.
Knirudisha tumesimama nje, si mzee baba katufuma, asikomae kaka aingie ndani. Akaingia. Basi anamwambia if you want to date my daughter do it properly sio vichakani. Ingia ndani kwangu, look me in the eyes, date her, i know you will treat her well. Moyoni nasema hili baba nalooo jamanii. Hajui hawa kwao wan li mansion. Ila akawa tu muelewa. Akapewa viazi vitamu na chai ya rangi akanywa fresh tu. Aibu naona mimi.
Baada ya hapo ikawa simu hapokei sms hajibu. Niliumwa malariaa. Na ndo nimempendaa kufa. Pendo la utoto linavojua kupanikishaaa. Nakondaaa tu. Nikakata tamaa kabisaa. Siku hio Hamad sina hili wala lile namsikia kama anaongea sebuleni. Nikajua delussion. Nikaja kufatwa yule mchumba wako kaja Mamuu twende yuko sebuleni. Nikasahu yoote na kuwahi. Akanipa nguo twende twende hamna mda wa kupotezaa badilisha. Na mimi kuoga fasta na kubadili na kupanda gari. Mtaani niliwanyoosha peke yangu nina bwana mwenye gari.
Nikazama humo ndani tukaenda kwenye sherehe. Sikujua hata tunaenda kwenye sherehe. Yule baba kuniona tena kapanic hatariii. Yule baba hanipendi tu sijui hata nimemfanyaga nini mwenzenu. Kuniona katumbukia nyongo hatarii. Sikujali sanaa as long as bae yuko na mimi aaaaah hamniambii kitu yani siambiliki, siambilikiii kabisaaa.
Entire party baby yuko busy making moves. And connections kiukweli hatukupata mda wa ku romance wala nini. Jioni nikarudishwa vuuuuu. Yani hata ule mda wa kuzungumza, kujuana kupendana hakunaaa. Inshort i was confused ila nikataka nione kwanza itaisha vipi.
Akawa hapatikaniii, hapatikaniii. Nikaanza sasakujua seriously liko tatizo, lipi sijui. Nikaomba Mungu anioneshe tatizo liko wapi. Nikaomba sanaaa. Siku tu mzee katika mingo mingo zake akakutana na Bae akiwa na msichana mwengine kwa maelezo yake ni mzuriii sanaaa. Sanaaa. I dont stand a chance hata robo. Wakiwa so loved up kwenye mgahawa. Akazama ndani ahakikishe ni wao. Bae akamuona akastukaa. Mzee akamuuliza nini hiki kijana? Are you not supposed to be dating my daughter?
Ikabidi mzee baba azuge zuge we broke up! Basi mzee anamkazia and you are already dating. Akaamua kunitwangia pale pale. Liz i am here with Jay and his new beautiful girlfriend. He said you broke up. Did you break up with him? Yaaani niliingia Mp mwenzenu. Nikaamua tu kujibu where did you see them dad? Akasema mjini huko. Nikaamua kujibu kinyonge yes we broke up dad! Huku nalia. Baba anasema you didnt know did you? Nikajibu tu No dad i didnt but it doesnt matter does it. Namsikia tu anamwambia Jay my son you are an evil man. Jay anajibu mbovu i aint your son and you aint my pops old man. Mzee anamuuliza sijui anaongea mwenyewe who would hurt Liz sucha a humble soul. Nikakata simu.
Kupenda kulikula kwangu. Kulitumbukia nyongo. Zikapita siku tatu naumwa pepo punda mixa kifaduro, mixa fistula. Chakula hakipitiiii kabisaa. Siku ya 4 Jay akapiga simu. Nikasema sipokeiii hata iweje. Ila nilokea kwa speed ya 4g. Akasalimia tu, na mimi nikajibu akasema tomorrow can i see you. Nikasema yes. Moyoni najipa moyo kesha chuja chuja huko kaona mimi ndo kila kitu kwake. Hawezi kuishi bila mimi. Nikanyoa vuzi kabisaaa, just incase ndugu msomaji, just in case.
Kesho akaja na gari lake, kabla sijatoka katoka mzee baba. Hachekiii. Jay akashuka aingie ndani, akamwambia you are not welcome in my home tena ondoka sasa hivi. Akasema liz, akakatishwa Elizabetiii hayupoo na hata akiwepo si kwa ajili yako kumchezea na kumtumia utakavyo. Anajieleza its not what you think. Akaingia ndani akatoka na panga. Anamwambia she might be nothing to you, unamuona mavi mavi tu ila ni mwanangu and she means the world to me, i will not watch you destroy her life. Inorder to destroy her life destroy mines first.
Nikacholopoka mlango wa jikoni pita nyuma nyuma mpaka mtaa 3 nikamtumia sms nipo huku twende zetu. Hapo nilijua tu kabisaa nitafute pa kulala kabisaa. Tumeenda beach najua naombwa msamaha. Nashangaa naambiwa i thought i owed you an explanation of what happened. Nikamkatiza no Jay i understand. Akauliza you do? How? You understand kwamba nampenda Diana kufaaa, she is everything to me. Nampenda mnooo. She can be difficult but i love her either way. Sorry i used you to get even with dad. I atleast should have told you the plot. Nikajibu to its no biggy anything for you Jay.
Moyoniii nawaka makaa ya moto. Kumbe all this time i was a bait. Jamanii. Why? Kwamba mimi ni mbaya hivooo. Au sababu maskini. Get even with dad! Used you! Maneno yalijirudia rudia sanaa akilini mwangu. Nikawa hata simsikilizii. Baadae mida ya saa 5 akanirudisha home. Najua kushanuka. Mlango ushafungwaa.
Sikujisumbua kugongaa kabisaaa. Nikaka tu pale kwenye kibaraza nazungumza mwenyewe. Kwa nguvu. Get even with dad! I used you. I love diana. She is my everything. Nilivurugwa sio kidogo kabisaaa. Nilivurugwa nikavurugika kabisaa. Nikasikia mtu anafungua mlango nikajua maza. Niaksikia inhia ukapumzike kumbe mzee baba mwenyewe. Hakunipiga wala hakusema chochote inaonesha alisikia mazungumzo yangu.
Ukiwa mnene usifanye diet mpende mtu asie kupenda. Utapotomokaaaje. Nilibakia skeleton. Mwenzenu. Nikapigiwa simu na Jay niende. As to why nilienda sijuiii. Ila nilienda. Nikamkuta Jay yuko na Diana. Niliishiwa tu nguvu. Diana analamika why do we have to hangout with her? Jay anamwambia because she is my friend. Diana anajibu she is your friend not mine, i dont like her. Jay anamwambia we spoke about this, you wre going to be nice. Diana anafanya ma attitude. Mi nimekaa hapo pembeni. Jay anatambulisha this is Diana, Diana this is Liz. Nikamwambia Diana nice to meet you. Moyoni natamaniii nimkabe na kumnyofoa koromeooo. She stole my man, she stole Jay. Najikaza. Diana akatoka.
Jay ananiambia she needs friends, please be her friend. She can be difficult at times but she is a nice person when you get to know her. Please be her friend. Nikamwambia tu okay Jay. Ill be her friend. I could see he was glad.
Diana akaja the usual mean rude girl she is. Namsifia Dee the wig is so nice. Akajibu i know and its expensive too. Nikakaa kimya. Jay akamuangalia jicho kali. Tukakaa pale tu napokea manyanyaso ya dee siku nzima. Jaya akasema ananirudisha, Diana akasema atanirudisha yeye.
Cha kushangaza nilitegema kwenye gari atanimeza mzima mzima ila walaaaa! She was actually nice. Kumbe mapepo yake akiwa arround Jay tuuu. Mpaka nafika home, akaniuliza you like this wig so much? Nikamwambia yes. Akalivua akanipaa. Nikakataaa! Akasema chukua tu, mi ninayo mengi sanaa. Chukua na wewe uwe na hilo moja. Kiukweli nililichukua hapana chezea brazillian OG lace wig million na upuuzi. Nikakonsida kama mafao yangu ki inua uchi. Bwana nimkose na lace wig nilikose juuu. Aaaa wapi.
Nimerudi amegeuza tu gari nikalivaa kwanza lace wig langu, nimeingia ndani zuriii, zuriii, kali kaliiii. Nikaoga nalo, mpaka nikalaa nimelivaaa. Chezea OG Brazillian lace wig. Tamaa ya mambo makubwa nimeianza mda sanaa ndugu msomaji. Mda sanaaa.
ITAENDELEA.