We mwanamke inakuwaje unatandikiwa kitanda?

We mwanamke inakuwaje unatandikiwa kitanda?

mzabzab are you serious kazi ya mke katika ndoa ni kupika, kufua na kupiga deki lol, so utaoa ili ufanyiwe hivyo! Na za mume ni zipi?

hizi ni part ya kazi zake bwana wewe....kugegedwa pia kazi ati lol.
mwanaume kazi zake ni; kugegeda, kuput food on the table, provide the wife's wants and needs, kumpenda mke unconditionaly na kumuheshimu
 
ila katika suala lakumtunza mume ni binafsi sina uo umodern au utraditional.babu dc wacha zako mwanaume mwenye adabu na heshima lazima apewe haki yake.my husband is very very bussy ,hata mimi nafanya kazi very busy lakini haihusu playing my part as a good wife.wacha tu niwe local lakin najua ninachokifanya.

Inategemea unapendelea nini, your culture au digitali, au ndio unataka ku-blend vyote. Kwangu mimi, naanza na culture, then digitali itafuata, nayo tu ni kwa sababu nalazimishwa na utandawazi. Ndio maana nikaweka dada wa kazi, kazi nyingine atasaidia, kwa usimamizi wangu (coz mimi ni muajiriwa), na nyingine nitafanya mwenyewe...

Huko chumbani kwangu kuna mambo yangu binafsi na ya baba pia (sisi tuuu..... wawili ambao ni mwili mmoja lol) ... ambayo sio lazima watu wayajue na kuyazoea zoea hovyo! Sasa wewe wataka hata nikiangusha pichu yangu huyo binti aje akumbane nayo akuuuuu.

babu niliona hii mada imeenda sana ila hii post yako imenistua ujue!
mi chumbani kwangu na yule mtu wetu kale katukuu kako ambako ni kabinti sasa hivi kanaingia kufanya nini sasa?unless niwe na shida sijui ya aina gani!sembuse dada!hapana kwa kweli!kama nimechelewa kuondoka nitafunga tu mlango ntakuja kutandika nikirudi!
cha kuonyesha neti langu la malaria haikubaliki a.k.a zinduka la kijani au la blue nini?
ah!hebu acheni masikhara jamani!
mi kwa mzee k ilikuwa mafruku kuingia chumbani kwake na gelofrendi wake!sa mi naanzaje leo kuingiza humo dada,mh!

nyie ni wanawake mnaojitambua ,nawaombeeni waume zenu wawe ni watu wanaothamini huo uelewa wenu na kudumisha upendo kwenye hizo ndoa zenu.
be blessed all.
 
Mie babu sioni siri kwa kweli

Hivi siku ukiugua watu hawataja kukuona chumbani? Tena hata member wa familia?

Kongosho ukiugua hilo ni jambo lingine na hakuna anayeomba kuumwa bibie........ ila katika mazingira ya kawaida unataka kusema nyumbani kwako wageni unawakaribisha mpaka chumbani eti kisa ukiugua mbona wataingia tu kunisalimia?
 
Last edited by a moderator:
wanandoa wanatakiwa kusaidiana,ila na hawa wanandoa wamekoosa ustaarabu,mambo ya chumbani wanagombania mbele za watu,,,,,,,hawana adabu,,,aibu ni yao wote,na iko palepale,,,,,aiibbuuuu
Kweli kabisa
 
ila katika suala lakumtunza mume ni binafsi sina uo umodern au utraditional.babu dc wacha zako mwanaume mwenye adabu na heshima lazima apewe haki yake.my husband is very very bussy ,hata mimi nafanya kazi very busy lakini haihusu playing my part as a good wife.wacha tu niwe local lakin najua ninachokifanya.

dada NIMEKUPENDA KWELI!
MUNGU AKUJALIE MAISHA MAREFU KWENYE NDOA YAKO!
 
kama kutandika kitanda
kupika chakula cha mume
kumuandalia maji ya kuoga mume(haijalishi kuna bath tubes na madijitali mengne ya bafuni basi japo niandae taulo tu la kujifuta)
kunawisha maji mume kabla ya kula
kuwa na special set up ya chakula ya baba tu hiyo
na kimsingi kufanya yale yote niliona mama yangu akimfanyia baba yangu ni ulocal wacha tu niwe wa kienyeji!
YANGU YANANINYOOKEA!basi! ucooperate ukiiingia mpka kwenye chini ya paa la nyumba yangu daaah!
mimi naamini hivo!
 
dada NIMEKUPENDA KWELI!
MUNGU AKUJALIE MAISHA MAREFU KWENYE NDOA YAKO!

mume mwenye heshima na adabu na mwenye kuheshimu uwepo wako lazima atunzwe kama mtoto mdogo,mume wangu huwa ananiambia ''you are the empire on which sun never set'' mkuu na kama ikitokea mume wangu siku hiyo haendi kazini mimi nakwenda lazima niamke mapema nimtayarishie chakula mpaka cha jioni nitakaporudi namwekea chumbani hana muda wakuranda randa na dada wa kazi ,kama naweza yote hayo kutandika kitanda sio issue kwangu hata siku nikiachaa anajua nitakuja kufanya.
 
kama kutandika kitanda
kupika chakula cha mume
kumuandalia maji ya kuoga mume(haijalishi kuna bath tubes na madijitali mengne ya bafuni basi japo niandae taulo tu la kujifuta)
kunawisha maji mume kabla ya kula
kuwa na special set up ya chakula ya baba tu hiyo
na kimsingi kufanya yale yote niliona mama yangu akimfanyia baba yangu ni ulocal wacha tu niwe wa kienyeji!
Yangu yananinyookea!basi! Ucooperate ukiiingia mpka kwenye chini ya paa la nyumba yangu daaah!
Mimi naamini hivo!

ningependa wanawake woote wajue kama ujuavyo wewe!
 
Duh, level.zimetofautiana. Ina maana hausafiri wewe? Anapikiwa na nani then?
mume mwenye heshima na adabu na mwenye kuheshimu uwepo wako lazima atunzwe kama mtoto mdogo,mume wangu huwa ananiambia ''you are the empire on which sun never set'' mkuu na kama ikitokea mume wangu siku hiyo haendi kazini mimi nakwenda lazima niamke mapema nimtayarishie chakula mpaka cha jioni nitakaporudi namwekea chumbani hana muda wakuranda randa na dada wa kazi ,kama naweza yote hayo kutandika kitanda sio issue kwangu hata siku nikiachaa anajua nitakuja kufanya.
 
Duh, level.zimetofautiana. Ina maana hausafiri wewe? Anapikiwa na nani then?
that is another case nikisafiri ,naacha maagizo wapi hotpot za baba ziwekwe sio dining kila mtu aje achakure chakure no zinawekwa mahaliambapo nitamwelekeza chakula chake kitakuwepo na huwa wanaona ninavyomwekea so akifika hm anajua chakula chake kilipo anachukua anakwenda chumbani.
 
Na hilo ndio tatizo la watu wanaooa ili wafuliwe, wapikiwe na watandikiwe vitanda!

Like nyingi zinawekwa na akina dada ku support POINTLESS kama hii hapa. Majukumu ya mwanamke halisi ni kumsaidia mumewe na si vinginevyo. Wanawake wenye hizo qualities ndo wanafaa kuwa wake za watu kinyume na hapo tunaingia kwenye gender issues.

Kama mwanamke anataka ndoa ambayo yeye hatataka kumsaidia mumewe kutandika kitanda au kumwekea maji ya kuoga halazimishwi kuwa mke wa mtu anaweza tu kujikalia singo akawa na full fledged FREEDOM. Malumbano ya nani kamwonea nani ndani ya ndoa huletwa na ninyi masista do amabo kutokana na kutotumia vema exposure zenu mnajikuta mnaenda extreme na hivyo kutaka kuchakachua maana ya ndoa. Ndoa ni ndoa na gender ni gender na huwezi ku mix mbili hizi bila kuleta migogoro mikubwa kwani ukitaka kkuwa safe au baki kwenye gender au kwenye ndoa ila si vyote kwa pamoja uta mess up.
 
Swali zuri sana marrykate?

Kitu gani ninamfanya mtu kuwa mke? Ni kupika, kutandika kitanda na kazi nyingine za ndani??

Na kwa wale wanaofanyakazi za kiofisi ambazo ni demanding kiasi kwamba muda unawabana tunawafikiria??

Nadhani tunafikiria kwa ufinyu mno...lol!!

Babu DC!!

na mimi hapa sijaelewa kabisa, kwa kazi kama zangu hizi ofisini saa kumi na mbili kamili asubuhi na kurudi ni saa moja jioni au zaidi, mume wa dizaini hii simuwezi kabisa, nilidhani mpaka mtu anakuoa, ni kwamba anakupenda na yupo tayari kusaidiana na mimi kwa kila kitu, kumbe analitaka mtu wa kutandika kitanda, na pengine umemuacha amelala sijui hapo inakuwaje unatoroka kazini kuja kutandika kitanda? mlicholalilia wate wawili? ni kiwete huyu au?
 
Kwa mwanamke mwenye akili timamu na anaitumia vizuri hawezi kumruhusu beki tatu kuingia chumbani kwake sembuse kumtandikia kitanda? wanawake wa dizaini hiyo ndio wanawapatia mabeki tatu wawafulie hata c.h.u.p.i zao

Chumba nacholala na mke wangu hata mtoto wetu anaingia kwa ruhusa, sasa watu hapa wanashabikia hata vitu vya kijinga tu kisa kujifanya kutafuta usawa. There is no usawa wa kijinsia katika dunia hii labda huko mbinguni kwa watakaofika.
 
Ubwanyenye huu utaishia lini...unaoa utegemee mamaa akufulie, tandikie hapo hapo awe mtafutaji, huo kama anamajukumu mawili zaidi.

Mwache atandikiwe bwana....

Wewe unaona ubwanyenye kuna wenzako wanafurahia na kama wewe unaona shida potezea kwani wako ambao wako tayari kuzifanya hizo kazi kama expression ya LOVE kwa waume zao na waume wana jinsi ya ku express LOVE kwa wake zao. Kwa sababu MMEKARIRI DEFINITION YA LOVE ndio maana unaona kumtandikia mumewo kitanda ni unyanyasaji.

Ndo maana hamjiulizi kwa nini ndoa nyingi za wanawake waliozaliwa kuanzia 1976 na kuendelea hazidumu. Badala ya couples kujadili jinsi ya kujenga familia na kujiletea maendeleo zinabaki kujadili NANI MWENYE HAKI KULIKO MWINGINE AU NANI AWE SUBMISSIVE NA NANI ASIWE. Why do nt we stick to the fundamental teachings za maneno ya Mungu badala ya kuleta mafundisho yasiyojenga ndoa? .
 
Ubwanyenye huu utaishia lini...unaoa utegemee mamaa akufulie, tandikie hapo hapo awe mtafutaji, huo kama anamajukumu mawili zaidi.

Mwache atandikiwe bwana....

Na jamaa ajiburudishe na HG, patamu hapo
 
Nyie wadada nimewapenda sana. Mungu azidi kuwabariki katika ndoa zenu. Kuna watu wameharibiwa sana na uzungu na kusahau kwamba wao ni wamatumbi na mila zetu za kimatumbi ziko wazi katika hili. Ndio maana wanawake wengi wa siku hizi ndoa zinawashinda kwa sababu ya kuendekeza vitu vya kijinga. Katika ndoa hakuna kitu kinaitwa usawa wa kijinsia isipokuwa ni mgawanyo wa majukumu, baasi.

kama kutandika kitanda
kupika chakula cha mume kumuandalia maji ya kuoga mume(haijalishi kuna bath tubes na madijitali mengne ya bafuni basi japo niandae taulo tu la kujifuta) kunawisha maji mume kabla ya kula
kuwa na special set up ya chakula ya baba tu hiyo na kimsingi kufanya yale yote niliona mama yangu akimfanyia baba yangu ni ulocal wacha tu niwe wa kienyeji!
YANGU YANANINYOOKEA!basi! ucooperate ukiiingia mpka kwenye chini ya paa la nyumba yangu daaah! mimi naamini hivo!

mume mwenye heshima na adabu na mwenye kuheshimu uwepo wako lazima atunzwe kama mtoto mdogo,mume wangu huwa ananiambia ''you are the empire on which sun never set'' mkuu na kama ikitokea mume wangu siku hiyo haendi kazini mimi nakwenda lazima niamke mapema nimtayarishie chakula mpaka cha jioni nitakaporudi namwekea chumbani hana muda wakuranda randa na dada wa kazi ,kama naweza yote hayo kutandika kitanda sio issue kwangu hata siku nikiachaa anajua nitakuja kufanya.

ila katika suala lakumtunza mume ni binafsi sina uo umodern au utraditional.babu dc wacha zako mwanaume mwenye adabu na heshima lazima apewe haki yake.my husband is very very bussy ,hata mimi nafanya kazi very busy lakini haihusu playing my part as a good wife.wacha tu niwe local lakin najua ninachokifanya.
 
Wewe unaona ubwanyenye kuna wenzako wanafurahia na kama wewe unaona shida potezea kwani wako ambao wako tayari kuzifanya hizo kazi kama expression ya LOVE kwa waume zao na waume wana jinsi ya ku express LOVE kwa wake zao. Kwa sababu MMEKARIRI DEFINITION YA LOVE ndio maana unaona kumtandikia mumewo kitanda ni unyanyasaji.

Ndo maana hamjiulizi kwa nini ndoa nyingi za wanawake waliozaliwa kuanzia 1976 na kuendelea hazidumu. Badala ya couples kujadili jinsi ya kujenga familia na kujiletea maendeleo zinabaki kujadili NANI MWENYE HAKI KULIKO MWINGINE AU NANI AWE SUBMISSIVE NA NANI ASIWE. Why do nt we stick to the fundamental teachings za maneno ya Mungu badala ya kuleta mafundisho yasiyojenga ndoa? .

Hiyo yaa kuanzia 1976 umeitoa wapi kwanini isiwe kuanzia 1980 au nyingine?
 
Kwa mwanamke mwenye akili timamu na anaitumia vizuri hawezi kumruhusu beki tatu kuingia chumbani kwake sembuse kumtandikia kitanda? wanawake wa dizaini hiyo ndio wanawapatia mabeki tatu wawafulie hata c.h.u.p.i zao

Chumba nacholala na mke wangu hata mtoto wetu anaingia kwa ruhusa, sasa watu hapa wanashabikia hata vitu vya kijinga tu kisa kujifanya kutafuta usawa. There is no usawa wa kijinsia katika dunia hii labda huko mbinguni kwa watakaofika.

Kaka naona leo mie na wewe....hapa lazima kieleweke.

Kwanza nijuvye mzee mwenzangu, kwa nini house girl haruhusiwi kuingia chambani kwako kufanya kazi zake kama anavyofanya sehemu nyingine ya chumba??

Kwani ni mahali pa kuagulia kiasi kwamba mnaficha matunguli??

Naomba unielimishe leo...mie ni denti, tena njuka!!

Babu DC!!
 
na mimi hapa sijaelewa kabisa, kwa kazi kama zangu hizi ofisini saa kumi na mbili kamili asubuhi na kurudi ni saa moja jioni au zaidi, mume wa dizaini hii simuwezi kabisa, nilidhani mpaka mtu anakuoa, ni kwamba anakupenda na yupo tayari kusaidiana na mimi kwa kila kitu, kumbe analitaka mtu wa kutandika kitanda, na pengine umemuacha amelala sijui hapo inakuwaje unatoroka kazini kuja kutandika kitanda? mlicholalilia wate wawili? ni kiwete huyu au?

Hapa sasa ndipo ninaposhindwa kuwaelewa wadogo zangu...

Mnalilia kusaidiwa kazi, na wakati huo mnaweza mipaka......

Kama kweli mnataka msaada, inakuwaje msaada wa house girl hamuutaki?

Babu DC!!
 
Kaka naona leo mie na wewe....hapa lazima kieleweke.

Kwanza nijuvye mzee mwenzangu, kwa nini house girl haruhusiwi kuingia chambani kwako kufanya kazi zake kama anavyofanya sehemu nyingine ya chumba??

Kwani ni mahali pa kuagulia kiasi kwamba mnaficha matunguli??

Naomba unielimishe leo...mie ni denti, tena njuka!!

Babu DC!!

Mzee mzima kweli leo kazi ipo kama na wewe umegeuka kuwa denti.
Chumbani kwangu na mke wangu ni mahali petu pa binafsi/maalum (private) kufanyia mambo yetu, huko tunajiachia. Chochote kinachofanyika huko ni chetu wawili mimi na mama rhobi tu ndo tunajua na tunaopaswa kujua. Mzee mzima chumbani kwako ndio mahali pa kujifunga khanga. Tatizo ninyi waswahili wenzangu mnafunga khanga mnatoka nazo kwenda sokoni hapa mtanishangaa.

Si kila unachokifanya kinakuwa ni kwa ajili ya "public consumption" hapa nakusudia public ya familia yako, lile mnalodhani kwamba linaweza kufikishwa kwa wengine ndo mnalitoa. Kama mna jambo lenu huko ndo mnaweka cabinet na kulidadavua, huko ndiko mnakaliana bila wasiwasi wowote manake mko wenyewe (hapa najua wengine wanajifanya wameendelea wanadandiana hata sebuleni mbele ya ndugu jamaa na marafiki)

Na la mwisho, siri yenu wewe na mkeo inakuwa siri ikiwa ni yenu wawili tu lakini mkishamruhusu mtu mwingine kuingia chumba chenu cha siri basi hakuna tena usalama hapo. Tena hawa mabeki tatu tunaowaokota tu mitaani wameshaleta mabalaa kwenye ndoa/familia za watu. Hapa kuna mambo mchanganyiko kama vile mabeki tatu kuwatia kwenye kumi na nane zao wanaume, kuibiwa, kuvujisha siri za familia na mambo mengine kama hayo. Sasa kwa kulitambua hilo ndipo wahenga wetu wakatufundisha kutoruhusu watu wengine kukizoea chumba changu na mke wangu.
 
Back
Top Bottom