We mwanamke inakuwaje unatandikiwa kitanda?

We mwanamke inakuwaje unatandikiwa kitanda?

Yani nyinyi wake zetu mnatia aibu sana, nimetoka kusuluhisha ugomvi kwa jamaa yangu, ugomvi ulikuwa mkubwa sana ila source mshkaji kachoka kutandikiwa kitanda na beki tatu so akamuuliza mkewe kama huyu dada anafua, ananipikia na bado ananitandikia kitanda hv nikwanini namnyima haki yake ya unyumba? mwanamke almanusura apasuke, ugomvi umesuluhishwa ila vipande nimempa, shame on u na wewe kama ni mmoja wao.

Si bora huyo jamaa. Wengine mpaka inapofikia wakati wa unyumba anaitiwa house girl, eti mama mwenyenyumba hajisikii, eti amechoka.
 
Mjenda Chilo
Ugomvi mwingine ni _______________ mtupu! I'd have sympathazied kama issue ya jamaa ingekuwa kitanda chao hakitandikwi,but not who is making the bed? Duh, kwa kweli siielewi hiyo shame unayoongelea ,kwani kazi ya mke kwenye ndoa ni kutandika kitanda:shut-mouth:!!!!???

Tatizo HG wengine wanatandika vitanda vya mabosi wao bila kuvaa nguo yeyote, na wengine wamejaaliwa haswa. Na kwasisi wamakonde tuna msemo wetu "Kaumbire Mungu kibaya ni sumu tu, vingine vyote ni kumemena tu." Sasa hapo ndipo mtafaruku unapoanzia.
 
Siku ukirudi ghafla home, ukapitiliza chumbani kulala, utasikia anachungulia dirishani Au anfungua mlango ghafla, utasikia samahani sikujua kama upo. Ukiuliza unafuata nini anasema nimekuja kudeki na kutandika kitanda. Hapo amesha kuchungulia na ameona infrastructure zote. Sasa kwa nini usitekeleze wajibu wa kulinda alivyo chungulia????????????????

Is not an issue kutandika ila consequences za hayo matendo ndio balaaa. Isitoshe akiwa peke yake anabadilika tofauti na akiwa na mkeo.


Wanaopinga hatuwashangai kwani kunawanawake wanaotafuta hg ili achanjwe na mume wao wanaenda kuchanjwa na mabwasheeee huko so kuficha hiyo ishu wanakutegea ili wapate cha kusingizia.

Utasikia umenidhalilisha sana, mwanaume gani wewe unalala hata na msichana wa kazi, basi akitoka amepaka mapowder na akirudi powder zote hakuna.
Kero tupu.

Napita tuuuuuuu hapa.
 
We nae kumbe ni walewale, yn unapanic kabsa kisa mwenzio hajatandikiwa kitanda? Kwn we ukitandka hyo mikono itakatika? Af eti unapandisha kifua na kusema shame on u, cyo sawa kijana kama pesa tunatafuta wte kwann ktanda tusitandke wte? Em acha mambo ya kizamani mana naona tu na ww unataka kunipandsha jazba ucku ucku!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Ndo wale wale, aibu zako mke kutandikiwa kitanda na housegal. Pesa au cheo havikuondolei uanamke wako.
 
win-win situation inatawamaliza dada zangu wakati mwingine ruhusuni huo the so called mfumo dume maana .. kuna wengine wajuaji kweli humu .. wala hawako kwenye ndoa.. wanapotosha .. ila sio kesi we fanya unachojiskia(dada).. utaleta thread ya kuachika pamoja na kazi yako nzuri nyumba nzuri watakufariji tu watakwambia ndoa bongo .. ila mwisho wa siku anaye umia wewe.. tutafakari vitu vingine wakati mwingine kwa mapana yake .. tunategemea ukienda shule reason inaongezeka kumbe mambo yenyewe ndo haya ya kila kila kitu una argue.. baadhi ya wadada badilikeni
unaona kama issue ya kutandika kitanda ni ndogo sana ila...
 
koma, ndio maana umekosa wa kukuoa! Na utakoma!

Thubutu yakoooooo!!!!!!!
am very young mie kukosa wa kunioa he he he hata 25 sijaiona naharakia nini........ndoa zenyewe hizi uwanja wa vita!
 
mkuu kasema ukwel,ningekuwa mm hata cmuuliz ataanza kuona nalala kwa hg
 
Tatizo lenu mkioa mnajua mmepata housegirl, kama mkeo nae anaenda kazini na anatafuta pesa kama wewe hata kutandika kitandani tandikeni kwa zamu..
Jifurahishe ila ujue mara nyingi matatizo ndani ya nyumba kati ya mama mwenye nyumba na mfanyakazi wa ndani mnayaanzisha wenyewe kwa kuwaacha wafanye kila kitu hadi kutandikiwa kitanda!!!!!hapo hapana,hata kama unafanya kazi huyo binti inafaa apewe mipaka ya kazi zake,vinginevyo ugomvi hautaisha,na mwanaume si wa kushindana nae itakula kwenu.
 
Ngumu kuchangia ...ila wanawake wawatandikie waume zao vitanda banaa..................
 
aiseeeh tumetofautiana sana hapa ,mimi kama huzband/baba/mkuu wa kaya domestic issue sijihusishi nazo labda kwa kupenda mwenyewe ila reason ya wote ni wafanyakazi iwe ndiyo kigezo cha mimi kutandika ,kuosha vyombo ,kudeki ,kupika n.k.....BIG NOOOO (yapo ya msingi ninayopaswa kuhofia na kuyatimiza zaidi ya huo upuuzi wa nyumbani)

nimeona couple ambayo baba na mama ni wafanyakazi, ila baba kama kichwa anatunza familia kuanzia mavazi, chakula, ada, afya na etc. mpk nguo, perfume na viatu vya mke ni yeye na bado anainvest kwa mke wake pamoja ya kuwa msomi anafanya kazi za home, kufua, kupika, anahakikisha nyumba iko safi, mme na watoto wamekula vizuri na kuvaa smart, sasa hebu jaribuni kuwa kichwa cha nyumba muone kama wake zenu hawatabadilika, yaani unakuta mme anataka mpk chakula mke anunue then unataka mke huyo huyo akutandikie kitanda looh! mke ataacha kufanya kwa kuwa anaona na yeye anauwezo wa kuzisaka pesa na kujitunza! heshima kwa ndoa inagharama, igharamien
 
nimeona couple ambayo baba na mama ni wafanyakazi, ila baba kama kichwa anatunza familia kuanzia mavazi, chakula, ada, afya na etc. mpk nguo, perfume na viatu vya mke ni yeye na bado anainvest kwa mke wake pamoja ya kuwa msomi anafanya kazi za home, kufua, kupika, anahakikisha nyumba iko safi, mme na watoto wamekula vizuri na kuvaa smart, sasa hebu jaribuni kuwa kichwa cha nyumba muone kama wake zenu hawatabadilika, yaani unakuta mme anataka mpk chakula mke anunue then unataka mke huyo huyo akutandikie kitanda looh! mke ataacha kufanya kwa kuwa anaona na yeye anauwezo wa kuzisaka pesa na kujitunza! heshima kwa ndoa inagharama, igharamien

sijakuelewa...... ila huyo baba anayetaka mkewe agharamie matumizi ya familia atakuwa anakasoro ila mimi kama mimi i have to worh hard kuweka chakula mezani ,kusomesha ,kutoa huduma ya afya ,kuvalisha n.k wife akichangia awe amependa mwenyewe ....ila kufanya ishu za domestic kisa hakuna wa kuzifanya eti wife hataki ,haitakaa itokee
 
hiyo ndio kazi ya mke...mie nitamiwa nakusaidia tuu..wanwake wakisasa wanaleta zakuleta

mzabzab are you serious kazi ya mke katika ndoa ni kupika, kufua na kupiga deki lol, so utaoa ili ufanyiwe hivyo! Na za mume ni zipi?
 
Last edited by a moderator:
Me nikisemaga siku hizi hakuna wanawake naambiwa Ooooh! Stamina ana chuki na wanawake haya sasa oneni upuuzi wao wenyewe
 
hebu wanawake wenzangu tuwe wa kweli kwa hili, tuache uzungu na tuuvae uafrika halisi,MWANAUME NI MTOTO na anatakiwa kufanyiwa vitu vyote ambavyo unamfanyia mwanao hata kumlisha ikibidi,jaman kitanda unalalia na mumeo kwa nini beki tatu wako akitandike?uchafu wenu,ma uji yenu yaliyomwagika usiku unamwambia akatandike huo ni uonevu wa hali juu.mmekalia kusema wanaume wabaya wakati ubaya tunautafuta wenyewe!mlee, akulee mleane.akienda kwa aliyefundwa akafundika sio hizi kitchen paty za siku HIZI, naamanisha MKOLENI huyo kitanda hatandiki,boxer havui,analishwa na kuvishwa.huwezi shindana na mwanaume ki kazi za nyumbani utachekwa kwa anayejua nini maana mume na ndoa.
 
Mmmh! umm kulthum kama umeolewa basi mumeo ana bahati ya mtende ashukuru mungu! wanawake kama wewe hamzaliwi kila siku!!
 
Hem muwe mnakaa na mama zetu (ze nu) wawafundishe maadili ya mtazania hasa mwanamke kwa mume.
Mkiachiwa nyiyi mnaweza mkataka wakati wa majamboz mtugeuze mtu.ingizie hata vidole vya mkono ili gemu iwe droo
Rubbish again

Mkuu Tripo9 punguza jazba, ni vema kuheshimu mawazo ya wengine hata kama mnatofautiana, sio uungwana kuita post za wachangiaji wenzio kuwa ni rubbish. Ushauri wa kufundishwa maadili naukubali sana.

waone kwanza hata aibu hamuoni hg anaingiaje vyumbani mwa waume zenu ,,,,,,,majukumu yote ya kiuchumi nyumbani mnataka mtimiziwe na mwanaume , mnachotafuta wenyewe ni chenu ,unyumba mnataka mshughulikiwe kisawasawa kama vile mume ni mbeba zege ,pia shughuli za nyumbani mnataka mnataka mume afanye... ubinafsi ubinafsi huo.
upon my dead body nitafanya kwasababu nimejisikia kufanya na siyo kwasababu wife hajafanya au hg hajafanya.....na hata usipofanya wewe siulizi mimi ,ila majukumu yangu ya msingi nitayatimiza effectively the rest nitajiju mwenyewe lakini siwezi kuhoji.

Mkuu asakuta same, hapo nilipobold naomba nieleweke kwamba siungi mkono hg kuingia chumbani kwa baba na mama, let alone kutandika kitanda! Hoja yangu ilikuwa kwamba napata mashaka hiyo ndoa anayoizungumzia mtoa mada imejengwa katika misingi gani, maana ikiwa mnatafuta msuluhishi kwa vitu kama kupika, kufua na kutandika kitanda itakuwaje kwa mambo mengine makubwa zaidi? Tena tatizo sio kwamba hizo kazi hazifanyiki bali tatizo ni kuwa zinafanywa na hg! Ndio maana nikasema kama unaoa ili ufuliwe, upikiwe na kutandikiwa kitanda basi hapo kuna tatizo kubwa sana. Ni vema pia mume ujue kutandika kitanda maana sio kila siku mkeo atakuwepo nyumbani.

Nakupongeza kwa kuamua kutohoji maana kutaepusha mengi, ila nikushauri ikikutokea mkeo hatandiki kitanda usimuulize bali mkiamka asubuhi mwambie ashike shuka upande ule na wewe shika upande mwingine mtandike kitanda. Ukifanya hivyo mara mbili tu naamini atajifunza na kutandika kitanda yeye mwenyewe, la kama kuna tatizo kubwa zaidi linalomsababisha amwachie hg hiyo kazi.

Binafsi napenda kumhudumia mume kadri niwezavyo but sometimes najiuliza nawezaje: mke ameajiriwa DSM, ana changamoto ya long work hours na foleni barabarani - akitoka kazini saa 11 basi huenda akafika home saa 1 usiku au late zaidi. Swali anapika saa ngapi? Kikubwa anachoweza kufanya ni kuset standards na kuzisimamia kuhakikisha chakula mnachokula ni bora kwa afya zenu; akiwahi basi ni heri zaidi - maana atapika mwenyewe.

Suppose tuna washing machine na tumble drier, kuna ubaya gani tukiweka nguo kwenye laundry basket (sio nguo za ndani na hiyo basket inakaa laundry room) then hg afue? Hii ni katika kurahisisha kazi kwa mama.

Naelewa wapo wanaume hupenda kuona wake zao ndio wanawafanyia hivyo vyote lakini ni vema wakiwa understanding kulingana na mazingira na hali halisi. Ikiwa mama ni house wife, sioni sababu ya kushindwa kufanya hizi kazi za nyumbani.
 
Last edited by a moderator:
Duuuu ... Ni bora tulale hapo kwa kitanda bila kutandika till when I get my annual leave kuliko house girl anitandikie.

Na usafi wa rum atafanya pale tu hali yangu ya afya hairuhusu ful stop.

Babu Dark City hope ushatoa mawaidha yako hapa lol .. Hali si hali.


BY THE WAY; hiv husband akija akakuta hg yupo bize kutandika si ndo mwanzo wa kumgawia utamu wangu ..

Ngoja nikatandike mie jua lishazama sasa!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Nasema sikuungi mkono!! mama yangu alikuwa mkurungezi (BOSS) serikalini, baba nae!! but hg alikuwa haingii chumba chao!!
 
NASEMA" pamoja na ukurugenzi wa Mama, hg hakuwahi kukanyaga bedroom yao, women wa nowdays hawajitambui tu hamna jingine!
 
Back
Top Bottom