Siku zote mke ni mlinzi wa mume wake na mume ni mlinzi wa mke wake. Hapa simaanishi kwamba umlinde kwa maana ya kumfuatilia kila anachokifanya isipokuwa unatakiwa kutambua mazingira hatarishi kwa mkeo/mumeo na kujaribu kumuepusha nayo. Wapo wanaume wachache wanaotoka na mabeki tatu hata kama hawaingii vyumbani mwao lakini believe me wengi wao unakuta kuna mazoea yasiyo ya kawaida baina ya mume na beki tatu ambayo yamesababishwa na mwanamke kutafuta usawa kiasi kwamba kazi zote anamuachia beki tatu.
Kwa kawaida binadamu kadri unavyomtendea wema hata kama ni wajibu wako ndipo anapoanza kukuzingatia na baade kujenga matamanio. Wanaume wengi ni dhaifu kwa wanawake jamani hili kama hamtaki kulikubali siwalazimishi. Beki tatu anakula vizuri anavaa vizuri anajua kupiga vitopu na kubinua chuchu halafu mzee anarudi usiku anafunguliwa nabeki tatu anatengewa chakula na beki tatu, ananawishwa na beki tatu hata kitanda anatandikiwa na eki tatu? mtaishia kulia na kusaga meno sana.
Ahsante sana kaka Mwita Maranya,
Naona Poti mjadala unaanza kunoga kwani hata wakongwe akina Nyamayao wako ndani ya nyumba..
Sababu zako mkee nazielewa... ila kuna nyingine bado zinanipa kigugumizi kidogo....
Una maana kwamba house girls ni hata kiasi hicho kwa ndoa??
Kwa upande wangu mie huwaona kama wanangu basi....
Na kwa vile wanangu wanaingia chumbani kwangu (kama mimi na bibi hatupo), basi hata wasaidizi hao wanaigia tu...
Ni hayo kaka,
Babu DC!!
msichana atafua tena baadhi ya nguo zetu na kazi nyingine lakinj chumba changu haikubaliki kuanzia usafi hadi kutandika
Mjenda Chilo
Ugomvi mwingine ni _______________ mtupu! I'd have sympathazied kama issue ya jamaa ingekuwa kitanda chao hakitandikwi,but not who is making the bed? Duh, kwa kweli siielewi hiyo shame unayoongelea ,kwani kazi ya mke kwenye ndoa ni kutandika kitanda:shut-mouth:!!!!???
cacico usiwe mchoyo, tunahitaji mawazo yako katika hili. Wewe ndiye untandika kitanda au ni beki tatu?kazi kwel kwel! hebu nikae kando kwanza, nione mtanange unaendeleaje??
Mzee mzima sitarajii kama ipo siku unaweza kumtamani mwanao, hata kama mama nanihino amekwenda ulaya for five years.
Lakini ukiwa mkweli utakubali kwamba mara kadhaa unakutana na wanawake wa umri sawa na binti yako na unajikuta umewatamani. Kwahiyo unaweza kuiona hiyo tofauti.
ni wajibu wala sio ombi kumshughulikia mwanamke wako!
hutaki acha njemba zikusaidie!!!
WIFE
Washing
Ironing
Food
Etcetera
(Kama ninakumbuka vizuri)
Pole zenu wenye waume wanaotumia hii definition!
WIFE
Washing
Ironing
Food
Etcetera
(Kama ninakumbuka vizuri)
Pole zenu wenye waume wanaotumia hii definition!
Kiukwel, utaratibu wa chumbani kwangu na wife, japo haujaandikwa ni kwamba wa mwisho kuamka kati yetu ndiye anayetandika kitanda.
Alafu tuna utani kuwa kila anayetandika, mwenzake akija anajitahidi kumkosoa kuwa hakutandika vizuri, anajifanya kutoa kasoro (jokes)
I just enjoy that?
Majukumu ya mwanamke halisi ni kumsaidia mumewe na si vinginevyo.
Washing- beki tatu (isipokuwa vyupi tu)
Ironing-beki tatu
Food-beki tatu
Etcetera-ufafanuzi tafadhali(kuna vitu gani humu kwenye hiki kipengele?)
Kwani mkiwa hotelini hizo taulo zenu huwa mnaziweka wapi??
Na huko hotelini huwa hampishi watu wakafanya usafi??
Naomba elimu yako Nyamayao..., hata ukitaka nilipe bill nitalipa!!
Babu DC!!
Yani nyinyi wake zetu mnatia aibu sana, nimetoka kusuluhisha ugomvi kwa jamaa yangu, ugomvi ulikuwa mkubwa sana ila source mshkaji kachoka kutandikiwa kitanda na beki tatu so akamuuliza mkewe kama huyu dada anafua, ananipikia na bado ananitandikia kitanda hv nikwanini namnyima haki yake ya unyumba? mwanamke almanusura apasuke, ugomvi umesuluhishwa ila vipande nimempa, shame on u na wewe kama ni mmoja wao.