We mwanamke inakuwaje unatandikiwa kitanda?

Umeona eeh...hawa ndio wanasababisha mabinti zetu watafute wazungu kwa udi na uvumba mwisho kuolewa na wazungu zeru zeru a.k.a. wazungu koko.

Mke asipokutandikia kitanda ndio unaenda kumsemea kwa mshenga?
 
kuna wengine sie waume hawataki kusikia chakula cha kupikiwa na dada, so ni wajibu wangu kama sipo atakula anapopajua ama atapika mwenyewe, kuhusu kitanda ndio kitu ambacho nakipinga milele coz naona ntakuwa sijamtendea dada haki hata kidogo, aisee ni jukumu langu kuanzia mashuka hadi mataulo ya room kwangu,room yangu inafungwa na funguo anazo baba/mama, DC hatufichi hirizi humu ndani but dada anaingia kufanyaje haswa kama mie nafanya wajibu wangu? kwangu mie naona sio haki kabisa kwa dada kufanya usafi room kwa wanandoa,hiyo ni kwa nyamayao.

Nimekuelewa sana Nyamayao,

Hata kama tunajadili hapa, bado kila watu wana taratibu zao. Ndiyo maana mie husema kila mara kwamba ndoa ni sawa na taifa huru (sovereign state)....

Hata hivyo, mie binafsi nilitamani kupata sababu za msingi kabisa (siyo lazima ziwe za kisayansi) ambazo zinawafanya wanandoa kuamua hivyo...kwamba ni marufuku house girl kutandika kitanda chao na pia kufanya usafi wa chumba chao!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Exactly kaka Mwita Maranya,

Na binti akishaishi chini ya paa langu tayari anakuwa kama mwanangu...that's why siwezi kumtamani...

Sasa inakuwaje house girl aonekane tishio kiasi hicho???

Babu DC!!

Mkuu Dark City usiniambie hujawahi kushuhudia ndoa zikiparaganyika kwa sababu ya beki tatu; aidha kwa baba kumsarandia beki tatu ama beki tatu katumia magic power!!? hujawahi kusikia wizi wa documents muhimu sana na hivyo kusababisha matatizo kwa familia husika?

Kwa uzoefu wangu mdogo mojawapo ya matatizo makubwa kwenye ndoa zetu siku hizi ni mabeki tatu, kadri mnanavyomuachia majukumu mengi ndani ya nyumba to the extent kwamba anafanya kila kazi ndani ya nyumba hujiona kama ndiye mwenye nyumba ama anastahili kuwa mwenye nyumba, na hapo ndipo huanza kufikiria kupata hicho kimoja kilichobakia ambacho ni kumtia mume kwenye rada yake.
 
Last edited by a moderator:
Sasa hapo Bro unajisifia uchafu...mkeo akisafiri basi wewe unajilaza kwenye shuka chafu...unaona madhara ya kuwa bossy na si husband?...utaja lala njaa kisa mimi MWANAUME. Nampa pole huyo wifi. Kibarua amepata.

Binafsi sijawahi "kutandika" kitanda tangu nilipofunga pingu za maisha...!

Mke wangu akisafiri huwa anakuta mashuka yale yale aliyoyaacha yakiwa bado yapo kitandani, hata na "net" pia iko vile vile...!

Ni Fedheha na AIBU kubwa kwa mwanaume "anayelala kitanda" kimoja na mwanamke, "kumtandikia" kitanda huyo mwanamke...! Mwanamke akikufikisha hatua hiyo, kwa kisingizio cha "kusaidiana" fahamu fika kuwa kuna siku atakuachia "nguo za ndani" ufue na kukupangia zamu za kupika - SHAME...!
 
kuna wengine sie waume hawataki kusikia chakula cha kupikiwa na dada, so ni wajibu wangu kama sipo atakula anapopajua ama atapika mwenyewe, kuhusu kitanda ndio kitu ambacho nakipinga milele coz naona ntakuwa sijamtendea dada haki hata kidogo, aisee ni jukumu langu kuanzia mashuka hadi mataulo ya room kwangu,room yangu inafungwa na funguo anazo baba/mama, DC hatufichi hirizi humu ndani but dada anaingia kufanyaje haswa kama mie nafanya wajibu wangu? kwangu mie naona sio haki kabisa kwa dada kufanya usafi room kwa wanandoa,hiyo ni kwa nyamayao.

Nimekuelewa sana Nyamayao,

Hata kama tunajadili hapa, bado kila watu wana taratibu zao. Ndiyo maana mie husema kila mara kwamba ndoa ni sawa na taifa huru (sovereign state)....

Hata hivyo, mie binafsi nilitamani kupata sababu za msingi kabisa (siyo lazima ziwe za kisayansi) ambazo zinawafanya wanandoa kuamua hivyo...kwamba ni marufuku house girl kutandika kitanda chao na pia kufanya usafi wa chumba chao!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Umeona eeh hakuna kitu ambacho sijuhi kama ningeweza vumilia kama mwanaume bossy....masheria lukuki...oh siri alichopika hg....ooh nguo zangu lazima ufue; ndio maana japo hg hatandiki chumba changu siwezi shangaa hao wanaotandikiwa na hg kwani ni utaratibu tu kwani kutandika ni kazi ngumu kama kubeba zege mpaka mtu aone ameonewa?

Mi nawajua washkaji zangu fulani (yes si wa tanzania)wanafuliwa hadi kofuli na hg...na wala ha complain kwani anapata mshiko wa nguvu...mbona manesi wanashika vidonda sembuse shuka tuuuu.

Sipendi kweli hizi 'Donts'....sijuhi mke wa fulani this mke wa fulani that...

Kati ya kitu ambacho sipendi ni kuchukuliwa kama boss na familiy members. Yes, heshima ya baba inakuwepo, but sio ile iliyojaa uooga, kwamba kila ninachoongea kama kaongea Mungu. Sijawahi kufuliwa chup, isipokuwa siku moja tu, nilijisahau nilipotoka safari nikaziacha chafu kwenye begi, waifu akazikuta akafua. Sikujisikia vizuri sana.

Nawaasa wanaume tusijenge tight boundaries ya kile unachoweza kufanya na kile ambacho lazima ufanyiwe. Vile unavyofanyiwa ufanyiwe tu kama utaratibu, lakini siku siku ukifanya mwenyewe, usione umekosewa heshima.
 
asakuta same... kuna baadhi ya watu wanajadili ili kuchangamsha genge tufurahi sie (kwamba wanayoyasema hayapo wala hayawezekani).

pia nachoamini ni kuwa kama mume na mke wanapendana na kila mtu anatimiza wajibu wake kwa kadri ya uwezo wake ..hayo MALUMBANO ya kusaidiana sijui fedha (mke kusaidia mahitaji mbalimbali ya familia) au sijui kazi za ndani (baba kusaidia some stuffs za pale home) hayapo lol.

Msaada unakuja automatically, na usipokuja una uomba akikataa basiiii.. Fanya kwa kadri ya nafasi na afya yako ikishindikana fanya siku inayofuata.

tena now days na hizi digitali zinatusaidia sana (apply na hizi pia) kurahisisha mambo... si mnafanya kazi bana kwa hiyo hamna nafasi ya shughuli za nyumbani .. nunua mashine ya kufua, vimashine vingine vya kurahisisha kazi za nyumbani, weka na beki 3... Alafu nyie mnabaki na yale mambo yenu binafsi ambayo hamtaki kuyaanika hadharani. JUST SIMPLE

umesema kikubwa ,sina cha kuongezea hapo bibie.
 
Binafsi sijawahi "kutandika" kitanda tangu nilipofunga pingu za maisha...!

Mke wangu akisafiri huwa anakuta mashuka yale yale aliyoyaacha yakiwa bado yapo kitandani, hata na "net" pia iko vile vile...!

Ni Fedheha na AIBU kubwa kwa mwanaume "anayelala kitanda" kimoja na mwanamke, "kumtandikia" kitanda huyo mwanamke...! Mwanamke akikufikisha hatua hiyo, kwa kisingizio cha "kusaidiana" fahamu fika kuwa kuna siku atakuachia "nguo za ndani" ufue na kukupangia zamu za kupika - SHAME...!

Duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuhhhhhhhhhhhhh,

Hapa sasa mkuu umenipa shule mpya?

Pamoja na kwamba mimi ni mtu wa 1947, mbona sioni shida kumfulia bibi kufuli zake??

Kuna ubaya gani hapo??

Babu DC!!
 
Mi si ndio nashangaa...

Mi wangu sometimes namwambia hiyo deki anzia room tafadhali...na sijarogwa wala kupinduliwa;

Na mimi siku nime feel kupiga mzigo nadeki vyumba vyote mpaka cha HG.

Tatizo watu wanakariri sana hawataki kutumia logic. Mababu walisema... mababu walisema... tuko kwenye enzi za digitali wao wanaongelea analogia (ujima).

Sema neno basi na wewe nyumba kubwa.....

Hapa naona ngoma inogile......

House girl akifanya usafi wa bed room na kutandika kitanda mbingu inapasuka vipande??

Babu DC!!
 
Nimekuelewa sana Nyamayao,

Hata kama tunajadili hapa, bado kila watu wana taratibu zao. Ndiyo maana mie husema kila mara kwamba ndoa ni sawa na taifa huru (sovereign state)....

Hata hivyo, mie binafsi nilitamani kupata sababu za msingi kabisa (siyo lazima ziwe za kisayansi) ambazo zinawafanya wanandoa kuamua hivyo...kwamba ni marufuku house girl kutandika kitanda chao na pia kufanya usafi wa chumba chao!!

Babu DC!!

Pengine ni traditions tu. Kama ambavyo ukienda kwa wazungu, akiamua kukuonyesha nyumba yake, anakuwa free na proud kukupeleka chumbani na kukuonyesha anapo/wanapolala. Huku kwetu sina hakika kama wapo wengi ambao ukienda kwao anakuonyesha hadi chumbani.
Ndio maana nasema pengine ni traditions, maana sidhani kama kuna sababu za kisayansi. Kitanda wanacholala baba na mama inaonekana kama altare fulani... inapoadhimishiwa ibada ya ndoa...
 
Tatizo hakuna kitufe cha LIKE Tuko...you deserve one! You are a man! One does not need to fight to prove that he is a man. Lol.

Kati ya kitu ambacho sipendi ni kuchukuliwa kama boss na familiy members. Yes, heshima ya baba inakuwepo, but sio ile iliyojaa uooga, kwamba kila ninachoongea kama kaongea Mungu. Sijawahi kufuliwa chup, isipokuwa siku moja tu, nilijisahau nilipotoka safari nikaziacha chafu kwenye begi, waifu akazikuta akafua. Sikujisikia vizuri sana.

Nawaasa wanaume tusijenge tight boundaries ya kile unachoweza kufanya na kile ambacho lazima ufanyiwe. Vile unavyofanyiwa ufanyiwe tu kama utaratibu, lakini siku siku ukifanya mwenyewe, usione umekosewa heshima.
 
Pengine ni traditions tu. Kama ambavyo ukienda kwa wazungu, akiamua kukuonyesha nyumba yake, anakuwa free na proud kukupeleka chumbani na kukuonyesha anapo/wanapolala. Huku kwetu sina hakika kama wapo wengi ambao ukienda kwao anakuonyesha hadi chumbani.
Ndio maana nasema pengine ni traditions, maana sidhani kama kuna sababu za kisayansi. Kitanda wanacholala baba na mama inaonekana kama altare fulani... inapoadhimishiwa ibada ya ndoa...

Mie kwangu ni uamuzi wa mgeni tu...akitaka tutapita kila sehemu hata uvunguni....

Halafu kuna suala la watu kuwazuia watoto kuja chumbani kwa wazazi...bado pia sielewi ...ingawa kwangu wana mipaka tu. Wajue kuwa kama tuko mie na wife basi hakuna free entry and exit. Ila kama niko peke yangu au wife, kwa nini asicheze na watoto wake huko chumbani??

Bado kuna vitu sivielewi, labda wale ambao wanatunza mila!

Babu DC!!
 
Mi si ndio nashangaa...

Mi wangu sometimes namwambia hiyo deki anzia room tafadhali...na sijarogwa wala kupinduliwa;

Na mimi siku nime feel kupiga mzigo nadeki vyumba vyote mpaka cha HG.

Tatizo watu wanakariri sana hawataki kutumia logic. Mababu walisema... mababu walisema... tuko kwenye enzi za digitali wao wanaongelea analogia (ujima).

Hizi dharau zetu kwa "mababu" zetu ndizo zimetufikisha hapa tulipo leo. Watoto wa mitaani wanazidi kuongezeka, talaka zinazidi kuongezeka na mifarakano ya ndoa/familia inazidi kuongezeka kwa sababu ya the so called kuishi kidigitali.

Kwa sake ya familia yangu sioni aibu kufuata misingi muhimu ya ndoa ya kianalogia kadri nilivyorithishwa na kufundishwa na wahenga kuliko kujifanya mdigitali na kuishia kuharibu familia yangu.
 
Hizi kitchen part za siku hizi hakuna mafundisho yoyote ni zawadi tu na kumwaga radhi kanga moko.

Hata mimi sifagilii kitchen party kabisa...

Kwa wale waliokulia vijijini huko ndipo kulikuwa na mafunzo ambayo ni genuine. Kwa sasa ni uchakachuaji tu...

Babu DC!!
 
Unadhani kuonyesha upendo kwa mkeo kutafanya ubomoe nyumba yako?

Hizi dharau zetu kwa "mababu" zetu ndizo zimetufikisha hapa tulipo leo. Watoto wa mitaani wanazidi kuongezeka, talaka zinazidi kuongezeka na mifarakano ya ndoa/familia inazidi kuongezeka kwa sababu ya the so called kuishi kidigitali.

Kwa sake ya familia yangu sioni aibu kufuata misingi muhimu ya ndoa ya kianalogia kadri nilivyorithishwa na kufundishwa na wahenga kuliko kujifanya mdigitali na kuishia kuharibu familia yangu.
 
i understand ni wajibu na nitautimiza ,ila expecting me to deal with domestic issues ,,,,,hell no! na zisipotimizwa na mwingine i wont ask kwakweli ,siwezi kuwa na huo muda kama mkuu wa kaya( kichwani kwangu kutakuwa na vitu vya muhimu kuliko huo ujinga wa kuangalia kama kitanda kimetandikwa au laa)

Kwann v2 vidogodogo vikusumbue, wat z wrng wit helpng ur blovd wife wit lito hh works! Dnt b self man. If u love ur wife u'l gve ha a helpng hand hasa pale wote mnafanyakazi na kurudi ucku. Dnt b stubborn. Love Love
 
Baada ya kusoma comments za mabinti na wanawake wengi juu ya hili ndo nimegundua ugumu uliopo juu ya kupata mwanamke mwenye elements nzuri kama walizonazo mama zetu. Si ajabu namba ya wanawake wasiopata waume inaongezeka.
 
Yaani hapo jamaa akijisevia beki 3 bidada anakuwa kajitakia
 
Mie kwangu ni uamuzi wa mgeni tu...akitaka tutapita kila sehemu hata uvunguni....

Halafu kuna suala la watu kuwazuia watoto kuja chumbani kwa wazazi...bado pia sielewi ...ingawa kwangu wana mipaka tu. Wajue kuwa kama tuko mie na wife basi hakuna free entry and exit. Ila kama niko peke yangu au wife, kwa nini asicheze na watoto wake huko chumbani??

Bado kuna vitu sivielewi, labda wale ambao wanatunza mila!

Babu DC!!

Hahaha
Inawezekana mi hiyo ndiyo mila moja iliyobaki naitunza...
 
Back
Top Bottom