Wazungu hatuwawezi na hatutowaweza

Wazungu hatuwawezi na hatutowaweza

kwenda21

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2014
Posts
3,423
Reaction score
3,415
Huu ndiyo ukweli ndugu zangu, Wazungu kamwe hatowaweza kwa lolote, wametuacha mbali sana, kwenye kila kitu. Wakitaka lolote katika nchi za Africa linakuwa, (kama waliweza Uarabuni) ukiwaletea jeuri sana wana mbinu zote za kukudhoofisha.

Kawaulize Zimbabwe, sijui wametoka sayari gani hawa watu, MTU unaweza kubisha tu kwa ujeuri ila wametuzidi; usiseme kwa kuwa walitutawala ingekuwa hivyo Ethiopia ingekuwa mbali nayo, maana haikuwahi kutawaliwa kamwe.
 
Na ili ujue na uthibitishe kuwa hatutowaweza nakuomba niondolee Herufi Z katika hili Neno Mzungu kisha niambie linabaki neno gani hapo Ndugu.
Ni kweli bro hawa ni Mungu tu ndio kiboko yao, kwa sisi binaadamu wa aina ya kuangalia na kujali leo tu, na huna plani ya kesho basi hatutawaweza.
 
Ndiyo ni watu kweli kabisa,ila hatuwawezi wazungu ni watu kweli,tatizo kuna watu hawataki kukubali uwezo walionao
Mimi naona ipo tofauti kati ya uwezo na maarifa, kila mtu anao uwezo sawa na mwingine yeyote tofauti ni namna gani unavyoyatumia maarifa. Maarifa ni uwezo Wa kutumia akili
 
Chochote unachojua Wewe hata uchawi,wenzako ndege zao tunaziona zinaruka juu,nyie huku nyungo zenu story tu,si mziweke watu wapige kazi,mwana acha ujeuri hatuwawezi
Hata wawe wamefanya au wanafanya kitu gani ,bado huwezi kuelezea mambo yatayokuja siku za baadae.
kwani hapo zamani unajua wazungu walikuwa vipi?
 
Hata wawe wamefanya au wanafanya kitu gani ,bado huwezi kuelezea mambo yatayokuja siku za baadae.
kwani hapo zamani unajua wazungu walikuwa vipi?
Wanaweza baadhi,ndo maana kuna utabiri Wa hali hewa,mwana we kubali tu kiroho safi acha chuki lazima ukubali kimaarifa wametuzidi, ona simu unayotumia, ona magari, bila wao ungetembea na mguu toka mbeya hadi Dar.

Wazanzibar wangeogelea mpaka dar,magorofa makubwa mgepandisha tofali kwa mkono,moto tungekuwa tunapikicha uwimbombo na ulindi mpaka Leo,umeme hakuna,technology ya kuongezewa damu,maji,mambo ni mengi sana
 
Huyu jamaa sijui nae katoka wapi! Kama wewe unaona wamekuumba, usituaminishe na sisi. Wachina, wakorea miaka ya 70 walikuwa na kauli kama hizo, sasa hivi hata wazungu wanawaogopa! Sasa unavyoanza kufananisha herufi kwamba inafanana na Mungu, mi naona hauko sawa kichwani!
 
Back
Top Bottom