Waziri wa zamani, Chadiel Mgonja afariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa zamani, Chadiel Mgonja afariki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mafuchila, Feb 1, 2009.

 1. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Date::1/31/2009
  Chadiel Mgonja afariki
  Fredy Azzah

  ALIYEKUWA Waziri katika serikali ya awamu ya kwanza, Chediel Mgonja, atazikwa siku ya Jumanne Kijijini kwake Vudee, Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro.

  Watu mbalimbali watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kesho kuanzia saa 6 mpaka saa 8 mchana, nyumbani kwa shemeji wa marehemu Ibrahim Kaduma, Makongo Juu.

  Akizungumza na gazeti hili jana, Ibrahim Kaduma ambaye ni shemeji wa marehemu, alisema shughuli zote za mazishi ya Mgonja zitafanyika nyumbani kwake, na kwamba, marehemu Chediel Mgonja ameacha mjane mmoja na watoto 10 na wajukuu 13.

  Alisema kuwa marehemu ambaye alizaliwa Desemba 31, mwaka 1934, alikuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kisukari, lakini hali ilikuwa mbaya zaidi ilipofika Desemba 13 mwaka jana.

  "Marehemu alikuwa akisumbuliwa na presha pamoja na kisukari toka siku nyingi. Lakini hali ilikuwa mbaya zaidi tarehe 13, Desemba na tulimpeleka katika Hospitali ya Lugalo, alipolazwa hadi mauti ilipomfika jana (juzi) saa 10 alasiri," alisema Kaduma.

  Alisema mjane Liliani Mgonja yuko Same, kijijini Vudee ambapo marehemu alikuwa akiishi na familia yake, na kwamba watoto wawili wa marehemu wako nje ya nchi, lakini wametoa ridhaa shughuli za mazishi ziendelee.

  Marehemu Mgonja aliongoza wizara mbalimbali katika serikali ya awamu ya kwanza, ambapo pia kwa nyakati tofauti aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Mkoa wa Tabora. Aliingia kwenye siasa mwaka 1965, akiwa Mbunge wa Same na mwaka huo huo akateuliwa kuwa Waziri wa Utamaduni, Siasa na Michezo.

  Mwaka 1966 alikuwa Waziri katika Ofisi ya Rais na Mambo ya Nje na pia mwaka 1968 alikuwa Waziri wa Elimu. Mgonja alikuwa kwenye Siasa mpaka mwaka 1995, ambapo kwa wakati wote alikuwa akiliwakilisha Jimbo la Same.

  Source: Mwananchi
   
  Last edited by a moderator: Feb 1, 2009
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu ahsante kwa taarifa.
  Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema pepo, Amina.

  Nakumbuka marehemu aliwahi kusema kuwa ingawa anataabika kwa kupata pensheni ndogo na hivyo kushindwa kuyamudu maisha, lakini alikuwa na fahari kubwa kwani yeye na wenzake walifanya kazi ya utumishi wa umma kwa uadilifu na uaminifu. Nadhani ingekuwa vizuri ujumbe huu wakepewa viongozi wa sasa, ambao badala ya kufanya kazi wanahangaika kukusanya chao mapema! Mzee mgonja amekufa masikini lakini msafi kwa kutojihusisha na ufisadi. Mungu atamlipa dhawabu yake huko peponi.
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Pole kwa ndugu na familia. Mungu ailaze roho yake mahali pema.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mungu ampumzishe mahali pema, na tunamshukuru kwa kulitumikia taifa kwa moyo
   
 5. C

  Chuma JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Una uhakika..
  .............Pole Wafiwa...?
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  RIP Mgonja. Nakukumbuka sana ulipokuwa waziri katika nyadhifa mbali mbali katika nchi hii wakati huo ikiwa Tanzania. Ulikuwa waziri wa elimu na mambo yalikuwa yakienda haswa.
  Sasa tuko katika nchi ya wadanganyika. Waliosomeshwa nawe bure leo hawasikii kilio cha wanyonge. Wanajali maslahi yao basi.
  Sijui itakuwaje wana wa wana wetu.
  Mimi nakumbuka nilikuwa sekondari wakati ukiwa waziri wa elimu.
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mchukia Ufisadi,

  Hawa wazee nao walikuwa na ufisadi wao, kwa mfano Mgonja ilikuwa kazi yake kuchukua wasichana kwenye hizo shule za secondary. Alikuwa hana tofauti na yule Mkisi wa JKT.

  Miaka hiyo watu walikuwa na uzalendo wa kulitumikia taifa ukiachia matatizo yao madogo madogo.
   
 8. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  "Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea...". Mola awape nguvu wafiwa. RIP Mgonja.
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,429
  Trophy Points: 280
  ..huyu bwana hakuwa fisadi lakini kwa zupu bwana we...,!..alikuwa akienda mikoani hafikii hotelini bali anaandaliwa malazi na ma head mistress...wa shule husika...,sasa nasikia kuna siku alienda singida headmostress alikuwa thabita siwale....akamwandalia kila kitu alafu akamletea na binti ..du mzee kuangalia binti akakuta ni binti yake[sijui cousin au wa kumzaa],alifanya makusudi kumkomoa ajuwe uchungu ambao wazazi wenzake wanaupata wanaposikia binti zao wanalazimishwa kugawa ngono....akahamaki sana..akataka kumfukuza kazi mama wa watu,mama akapiga simu ikulu akamwambia mwalimu stori nzima....kwa hasira mwalimu pale pale akatengua uwaziri wake......nadhani pia alim reward mama siwale kwa kumpandisha cheo kwa ujasiri..maana kila mara alikuwa analalamikiwa kuhusu mgonja lakini hakuna headmistress aliyekuwa na balls za kuripoti .

  .....sasa sijui kama alikuwa anachukua wanawake kwa mdomo au naye pesa yake iliishia kujengea wanawake....maana mtu huwezi kuwa waziri miaka mingi tena hadi foregn ..halafu uje uishie umaskini...lazima kuna namna alitumia kipato chake vibaya...hana tofauti na moses nnauye ...amekufa hana nyumba lakini wanawake wengi tu amewajengea nyumba...
   
 10. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 135
  RIP-Chediel Yohana Mgonja. Mfumwa akurinde uko he kaa yako shaa.
   
 11. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...Mbuzi hula mwisho wa kamba yake na unavuna unachopanda. Niliwahi kumuona huyu mzee pale same mjini mwaka 2004 alikuwa na hali mbaya sana kuanzia mavazi mpaka afya yake huwezi kuamini kama alikuwa mtumishi wa serikali mpaka katika level ya uwaziri...Ndio maishakupanga ni kuchagua!!! (RIP)
   
 12. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kushindwa kumiliki udhaifu wa kibinadanmu, viongozi wengi wa miaka hiyo walitekeleza wajibu wao kwa uadilifu.

  wale ambao walifanya makosa ya kisera walifanya si kwa nia ya ufisadi bali imani yao iliwatuma kwamba wanayoyafanya ni kwa manufaa ya taifa. wengi walitegemea kwamba baada ya kustaafu pensheni zao zingetosha kukidhi mahitaji yao hata hivyo hali ya maisha imepanda
  kiasi kwamba hiyo pensheni yao haitoshelezi hata matumizi ya siku chache. hali hii ndio maana baadhi yao (ambao hawakuweza kujiingiza kwenye shughuli za kiuchumi) wameishi maisha ya ufukara baada ya kustaafu.

  rip chadiel mgonja
   
 13. b

  bangusule Senior Member

  #13
  Feb 1, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  MFUMWA MURUNGU!! MFUMWA MURUNGU!! oooi Chedieeli 'kaghembe' watooonga!! watoooonga!! watonga Chedieli!!

  hena kintu avae, wegondie he kitabu chako nikienda nkuvwije. Kaghembe umeondoka na siri nzito moyoni. vigogo watatu waliojaribu kukuzuia usigombee ubunge mwaka 65 nani? vigogo waliokutana na wazee na kuosha mikono mbele yao, wakidai hufai kuongoza wilaya ya Pare ni nani? kijana aliyejaribu kukurubuni uende maeneo ya kinondoni kupokea zawadi ni nani? uliripoti suala hilo polisi ambao walikwenda eneo la miadi yenu na dereva wako. mtu huyo alipoliona gari lako aliamua kumshambulia dereva, mtu huyu aliuawa. umefariki bila kumtaja mhusika.

  Chedieli Yohane Mgonja 'kaghembe' ulitumikia Taifa na jimbo lako kwa uwezo wako wote katika mazingira magumu ya vita vya kisiasa. Chedieli wananchi wa Same tutakukumbuka kwa juhudi zako za kuhamasisha kazi za kujitolea 'msaragambo.' Kutokana na juhudi hizo za kupasua miamba kupitisha barabara, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alitamka kwamba "Wapare ni Wachina wa Tanzania."

  MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI CHEDIELI YOHANE MGONJA.
   
 14. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mungu akulaze mahali pema peponi na asante kwa kulitumikia taifa kwa uadilifu. Poleni sana wafiwa.

  Niliposoma mwanzo nilifikiri ni mwizi (fisadi) Gray Mgonja amefariki.
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Kafara, heshima mbele sana na hapa tupo pamoja,Mungu amuweke mahali pema, unajua huyu marehemu alisababisha matatizo makubwa kwa jamaa yangu Patric Balisidya (RIP),

  Lakini Mungu amarehemu na wote tuko njiani.
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  RIP-Chediel Yohana Mgonja. Mfumwa akurinde uko he kaa yako shaa.
  __________________
  what???kana ka kansungu tufafanulie tusije ongezea tukakuta tunamtukana marehemu hapa tukapata dhambi ya maisha!!1
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  RIP mgonja!!!hongera kwa kutofanikiwa kujiingiza kwenye ""UFISADI"" muombee mwanao/nduguyo Gray mgonja amalize salama kesi yake na yeye atubu siku ya mwisho kwa kulifikisha taifa hapa tulipo na ""EPA""..na nyie ndugu zetu mnaoandika ukabila jitahidini kuandika maombi kwa mzee wetu amkumbuke ndugu yenu GREY MGONJA
  natumaini mlishiriki kumsaidia kwenye dhamana si kusubiri wafe tuwapongeze humu ndani na kama aliaribu tupen data za huyu ""FISADI -GREY MGONJA"" Kabla hatujaja kupeana pole humu ndani!!!!!!
  Narudia tena mzee wetu hongera kwa kutoshiriki kwenye ufisadi wa serikali,,ioombee sana serikali ulioiacha duniani haifai,chafu inanuka na ya kuwek maombini.twaamini ulikuwa ukiiiombea kabla ujafa...kama ni kuchapa toto's za watu mzee natumaini ulitubu kwa hili vinginevyo !!!!mmmmh!!!!!
  chedi!!1
   
 18. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  haya mambo ya mtu muovu mna sema aresti ini pisi yananikera.....hata leo Chenge etal wakifa mtasema resti ini pisi....hakuna cha RIP kwa Chedieli alituharibia dada zetu....akakae motoni huko.....
   
 19. O

  Ogah JF-Expert Member

  #19
  Feb 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  RIP Chediel Mgonja...........Poleni sana wafiwa
   
 20. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 135
  Mungu akulinde huko kwenye makao yako mapya, sidhani kuna haja ya kutafsiri hako kapande ka kimombo!
  Mzee wangu alikuwa mwajiriwa wa serekali na enzi hizo za ubunge wa marehemu, kituo chake cha kazi kilikuwa Same na nina good memories za huyu bwana na wilaya ile kwa ujumla and my Pare is still at a satisfactory level!
   
Loading...