Who was the chief policy adviser at the time? Tunajuaje kwamba yeye sio aliyemshauri Nyerere kuchochea kuvunja muungano wa Nigeria?
Well, unaweza kuwa sahihi Chadiel Mgonja aliburuzwa tu, after all, tunamjua Nyerere wetu, alikuwa ana bulldoze kila mtu na kifimbo cheusi.
Lakini hata kama Mgonja alibururwa bururwa bado tutasema yeye ndio alibeba ujumbe wa nchi.
Collin Power alienda United Nations na vichupa vya ushahidi wa silaha za Iraq. Walipotekeleza siasa ya kuvamia Iraq wakakuta silaha ni hewa Collin alipoteza credibility, na hakusema "nilitumwa na Bush," angeambiwa wewe "roboti"? Hatuwezi kuanza kuchambua ni nani alibeba ujumbe, nani alipelekeshwa ki punda punda kati ya Collin, Diki, Paulo, Donadi, Condi, na George wa Tenet, George wa Bushi, hatujui, hatujali kuanza kuchambua nani alimshawishi nini nani.
Wote walikuwa jikoni, wote walipika siasa ya nje, wakaibeba. Huko jikoni aliyekatishwa vitunguu, aliyechochea kuni, aliyetoa resapi, aliyesongeshwa ugali, wao ndio wanajua.
Kiongozi unaepinga kubururwa bururwa anajiuzulu.