Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba awajibu TLS kuhusu Rais Samia Suluhu kuteua Baraza jipya la Mawaziri

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
4,619
2,000
Nimesoma andiko la TLS, kwa heshima zote kwa chombo chetu hiki kilichopewa mamlaka kisheria, Nimeshtuka sana, I wish to say,

Kwanza KATIBA HAIJAVUNJWA KWA MHE RAIS SAMIA SULUHU kuapa, na wala hakuna Mkanganyiko wowote wa Kikatiba, kwa yeye kutoteua PM na Baraza jipya. Mmekaa wote kweli mkaona hivyo.

Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 42(5) kuna watu wa aina mbili wanaweza kuwa Rais. Moja, Rais Mteule ambaye anatokana na Ibara ya 42(1). Mbili, Mtu anayeshika kiti cha Rais ambaye anatokana na ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ambaye ni Makamu wa Rais. Kwa Mazingira haya, Makamu wa Rais, baada ya kifo cha Rais, anakuwa Kaimu Rais baadae ndio ameapa na kuwa RAIS wa Nchi. Rais Mteule anapatikana kutokana na uchaguzi. Hivyo basi ibara ya 57(2)(f) ya Katiba haitumiki katika mazingira haya. Kwa mjibu wa Sheria, Mhe Rais alitakiwa kutoa taarifa hii kwenye Baraza la Mawaziri baada ya kuapa na alifanya hivyo, maana yake Baraza lipo.

Hata hivyo kwa tamaduni za Kiafrika, kitanzania na Misingi ya UTU, SIONI KAMA NI JAMBO JEMA SANA KUANZA KUJADILI MGAWANYO WA MADARAKA TUNGALI HATA HATUJAMZIKA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU. HUU SIO MSIBA MDOGO, JAMBO HILI ZITO LIKO MIKONONI MWA RAIS WETU MAMA SAMIA SULUHU, HALAFU SISI TUANZE KUMPATIA MAMBO YA MARA TEUA PM, MARA VUNJA BARAZA, KATIBA INAELEKEZA RAIS KUAPA NA NAMNA YA KUMPATA MAKAMU WA RAIS.

KWA MJIBU WA KATIBA RAIS ANARUHUSIWA KUVUNJA BARAZA MUDA WOWOTE NA KUPANGA ATAKAVYO HATA SIO KWA MAZINGIRA KUAPA KWAKE,

KWANINI HATUIONI HEKIMA YAKE YA KUSHUGHULIKIA MSIBA KUMSITIRI KWANZA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU? TUNAANZA NA MAZISHI AU MIRATHI? 😭😭😭😭

Pia soma > TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14
Hajajibu kisheria kabisa!!!! Although TLS hawako sahihi Ila Mwigulu hajajibu kisheria kabisa ...Kuna umuhimu wizara hii akaishikilia Mwanasheria Msomi
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
4,026
2,000
Nimesoma andiko la TLS, kwa heshima zote kwa chombo chetu hiki kilichopewa mamlaka kisheria, Nimeshtuka sana, I wish to say,

Kwanza KATIBA HAIJAVUNJWA KWA MHE RAIS SAMIA SULUHU kuapa, na wala hakuna Mkanganyiko wowote wa Kikatiba, kwa yeye kutoteua PM na Baraza jipya. Mmekaa wote kweli mkaona hivyo.

Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 42(5) kuna watu wa aina mbili wanaweza kuwa Rais. Moja, Rais Mteule ambaye anatokana na Ibara ya 42(1). Mbili, Mtu anayeshika kiti cha Rais ambaye anatokana na ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ambaye ni Makamu wa Rais. Kwa Mazingira haya, Makamu wa Rais, baada ya kifo cha Rais, anakuwa Kaimu Rais baadae ndio ameapa na kuwa RAIS wa Nchi. Rais Mteule anapatikana kutokana na uchaguzi. Hivyo basi ibara ya 57(2)(f) ya Katiba haitumiki katika mazingira haya. Kwa mjibu wa Sheria, Mhe Rais alitakiwa kutoa taarifa hii kwenye Baraza la Mawaziri baada ya kuapa na alifanya hivyo, maana yake Baraza lipo.

Hata hivyo kwa tamaduni za Kiafrika, kitanzania na Misingi ya UTU, SIONI KAMA NI JAMBO JEMA SANA KUANZA KUJADILI MGAWANYO WA MADARAKA TUNGALI HATA HATUJAMZIKA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU. HUU SIO MSIBA MDOGO, JAMBO HILI ZITO LIKO MIKONONI MWA RAIS WETU MAMA SAMIA SULUHU, HALAFU SISI TUANZE KUMPATIA MAMBO YA MARA TEUA PM, MARA VUNJA BARAZA, KATIBA INAELEKEZA RAIS KUAPA NA NAMNA YA KUMPATA MAKAMU WA RAIS.

KWA MJIBU WA KATIBA RAIS ANARUHUSIWA KUVUNJA BARAZA MUDA WOWOTE NA KUPANGA ATAKAVYO HATA SIO KWA MAZINGIRA KUAPA KWAKE,

KWANINI HATUIONI HEKIMA YAKE YA KUSHUGHULIKIA MSIBA KUMSITIRI KWANZA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU? TUNAANZA NA MAZISHI AU MIRATHI?

Pia soma > TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14
Huyu nae ni mpuuzi,hoja hapa ni kwamba,Katiba inavunjwa kwa Samia kutokuteua Baraza jipya?
Hawa mawaziri waliapa mbele ya Raisi aliyepita,je wanaweza kuendelea na viapo vyao,kwa Raisi mpya?
Jiwe aliapa 2015,akaapa Tena 2020!kwanini ?akuendelea na kiapo chake Chake Cha 2015?kwanini alimwapisha Tena PM majariwa 2020,wakati aliisha muapisha 2015?!
 
inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
2,230
2,000
Sote tunajua Mama Samia ameshakula kiapo lakini bado hajapata makamu wake.

Je, kikatiba inachukua siku ngapi (tangu kuapishwa kwa Rais) kumpata Makamu wa Rais?
 
Mingoi

JF-Expert Member
Jul 21, 2012
11,621
2,000
Aige mfano wa Zanzibar, rais Mwinyi alimteua mkuu wa mkoa na anachapa kazi. Aachane na hawa wa makundi makundi na wenye viherehere na tamaa ya kuwa marais watamsumbua. Pale mkoa wa Simiyu ninamuona VP Eeh Mungu tusaidie...
 
Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
6,200
2,000
Aige mfano wa Zanzibar, rais Mwinyi alimteua mkuu wa mkoa na anachapa kazi. Aachane na hawa wa makundi makundi na wenye viherehere na tamaa ya kuwa marais watamsumbua. Pale mkoa wa Simiyu ninamuona VP Eeh mungu tusaidie...
Huyo jamaa kikabila ni mjita hvyo ni wakanda ya ziwa , tatizo sa hv wa kanda ya ziwa mnawananga Sana , Ila probably ndio kanda ya wachapa kazi wenye maamuz magumu ....
 
Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
201,384
2,000
Watu mnawaza Baraza la Mawaziri ukiangalia wabunge ni wale wale msiowapenda. Makamu ni mtu wa CCM basi kujitafutia maumivu tu hasa akichaguliwa msiyempenda.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,275
2,000
Aige mfano wa Zanzibar, rais Mwinyi alimteua mkuu wa mkoa na anachapa kazi. Aachane na hawa wa makundi makundi na wenye viherehere na tamaa ya kuwa marais watamsumbua. Pale mkoa wa Simiyu ninamuona VP Eeh Mungu tusaidie...
Wewe Antony Mtaka tulia! Acha kujipigia promo. Makamu wa Rais ameshapatikana kitambo tu. Tunasubiri kumuhifadhi Mzee kwanza, then tumtangaze.

Ridhika na hicho cheo ulicho nacho. Ukiendekeza tamaa, yatakukuta kama yale ya Makonda.
 
Mingoi

JF-Expert Member
Jul 21, 2012
11,621
2,000
Wewe Antony Mtaka tulia! Acha kujipigia promo. Makamu wa Rais ameshapatikana kitambo tu. Tunasubiri kumuhifadhi Mzee kwanza, then tumtangaze.

Ridhika na hicho cheo ulicho nacho. Ukiendekeza tamaa, yatakukuta kama yale ya Makonda.
Hao mnaowafikiria si bora awe Aggrey Mwanri tu tujue moja.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,275
2,000
Hao mnaowafikiria si bora awe Aggrey Mwanri tu tujue moja.
Huu ni wakati wa chama kurudishwa mikononi mwa wenye chama chao! Hivyo sahau hicho cheo kupewa mtu asiye na mizizi au CV inayo eleweka.

Usisahau CCM ASILI ina nguvu kubwa kuliko wahamiaji haramu ccm makinikia.

Hawa waliishi kwa kudra za mtu mmoja tu! Na amesha waacha njia panda! Mpaka sasa hawajui hata hatma yao tu itakuwaje ndani ya chama.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom