Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba awajibu TLS kuhusu Rais Samia Suluhu kuteua Baraza jipya la Mawaziri

Josh J

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
1,915
2,000
Ili mama afanye Kazi yake vizuri ni lazima avunje kivuli cha Magu na hii ndio changamoto yake kubwa kwa sasa vinginevyo hilo genge litataka kumfanya kwamba yeye hana akili na Urais ameupata kwa hisani sasa hapo Kazi kwake.

Huwezi endesha nchi kwa kufuata genge la mtangulizi,kila Rais ana utashi wake,ndio maana Magu alienda kinyume na JK nk nk

Katiba inampa Rais uamzi huo ,so kwa maoni yangu lazima atimue genge la Chato lote na aweke watu wake royal
Akili yako Haina Akili
 

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,546
2,000
Rais ni taasisi akifa na baraza la mawaziri linakufa automatically!

Hili hata Prof wa sheria Palamagamba analielewa vizuri.
Hapo mwisho "...leo amevaa barakoa!!" Ina maana ile taasisi aliyoitii sasa haipo kwa hiyo ame...
Misimamo ile aliyokuwa nayo sijui ataiendeleza au anarudi "majalalani!?"
Tutamkumbuka JPM R.I.P
 

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,546
2,000
Ili mama afanye Kazi yake vizuri ni lazima avunje kivuli cha Magu na hii ndio changamoto yake kubwa kwa sasa vinginevyo hilo genge litataka kumfanya kwamba yeye hana akili na Urais ameupata kwa hisani sasa hapo Kazi kwake.

Huwezi endesha nchi kwa kufuata genge la mtangulizi,kila Rais ana utashi wake,ndio maana Magu alienda kinyume na JK nk nk

Katiba inampa Rais uamzi huo ,so kwa maoni yangu lazima atimue genge la Chato lote na aweke watu wake royal
Kwa nyongeza "MAMA AKAE CHONJO SANA NA YALE MAJAMBAZI "WAZALENDO MASLAHI" WANAOTUMIA MGONGO WA CHAMA KUJINUFAISHA HUKU WAKIMSIFU NA KUMTUKUZA BADALA YA KUMSAIDIA NJIA SAHIHI
 

1954

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
9,721
2,000
Yaani wapinzani kulalamika ni jadi yao! Mnadhani kuna kupumua hapa? Magu spirit will prevail
Tena zaidi...tusubiri tuone...Magu aliweka standards za utendaji, Sasa atakayekwenda kinyume yatamtokea..
 

Chendembe

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
263
500
Angekuwa yeye angeendelea na watu ambao hajawateua?
Ajuwi madhara kiutawala kufanya hivyo?
Uku ni kukurupukaaaa
 

aloycious

JF-Expert Member
Dec 17, 2012
6,021
2,000
Huyu jamaa ndio alipata first class UDSM? Kweli msiba "mkubwa" ndio uvunje katiba?
 

aloycious

JF-Expert Member
Dec 17, 2012
6,021
2,000
Kiwewe hawana utulivu kabisa. Dereva amekufa. Tingo amekuwa dereva,abiria wamekuwa matingo. Abiria wanamuelekeza dereva ambae kiuhalisia ni tingo.
 

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
1,562
2,000
Nimesoma andiko la TLS, kwa heshima zote kwa chombo chetu hiki kilichopewa mamlaka kisheria, Nimeshtuka sana, I wish to say,

Kwanza KATIBA HAIJAVUNJWA KWA MHE RAIS SAMIA SULUHU kuapa, na wala hakuna Mkanganyiko wowote wa Kikatiba, kwa yeye kutoteua PM na Baraza jipya. Mmekaa wote kweli mkaona hivyo.

Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 42(5) kuna watu wa aina mbili wanaweza kuwa Rais. Moja, Rais Mteule ambaye anatokana na Ibara ya 42(1). Mbili, Mtu anayeshika kiti cha Rais ambaye anatokana na ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ambaye ni Makamu wa Rais. Kwa Mazingira haya, Makamu wa Rais, baada ya kifo cha Rais, anakuwa Kaimu Rais baadae ndio ameapa na kuwa RAIS wa Nchi. Rais Mteule anapatikana kutokana na uchaguzi. Hivyo basi ibara ya 57(2)(f) ya Katiba haitumiki katika mazingira haya. Kwa mjibu wa Sheria, Mhe Rais alitakiwa kutoa taarifa hii kwenye Baraza la Mawaziri baada ya kuapa na alifanya hivyo, maana yake Baraza lipo.

Hata hivyo kwa tamaduni za Kiafrika, kitanzania na Misingi ya UTU, SIONI KAMA NI JAMBO JEMA SANA KUANZA KUJADILI MGAWANYO WA MADARAKA TUNGALI HATA HATUJAMZIKA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU. HUU SIO MSIBA MDOGO, JAMBO HILI ZITO LIKO MIKONONI MWA RAIS WETU MAMA SAMIA SULUHU, HALAFU SISI TUANZE KUMPATIA MAMBO YA MARA TEUA PM, MARA VUNJA BARAZA, KATIBA INAELEKEZA RAIS KUAPA NA NAMNA YA KUMPATA MAKAMU WA RAIS.

KWA MJIBU WA KATIBA RAIS ANARUHUSIWA KUVUNJA BARAZA MUDA WOWOTE NA KUPANGA ATAKAVYO HATA SIO KWA MAZINGIRA KUAPA KWAKE,

KWANINI HATUIONI HEKIMA YAKE YA KUSHUGHULIKIA MSIBA KUMSITIRI KWANZA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU? TUNAANZA NA MAZISHI AU MIRATHI? 😭😭😭😭

Pia soma > TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14
Miluzi imeshaanza tayari Mama wa watu wakimtafutia upenyo wa mgogoro, majitu yenye tamaa za madaraka hayaishi kufanya uchonganishi
 

Natena wiza

JF-Expert Member
Mar 13, 2021
310
500
Acha kihele hele we mtesi wa ndugu zetu, vip kama rais atafata ushauri wa TLS?? utaficha wapi aibu yako?? Lakini mijitu kama wewe haina kabisa mishipa ya aibu!! Juzi umeaibika!! lakini hujakoma tu!!
Acheni kujipendekeza, et mama.Mwendo ni uleule na mfunge na kuomba sana VP aisiwe kichaa BASHIRU.
 

Natena wiza

JF-Expert Member
Mar 13, 2021
310
500
Maono ya Magufuli hayafi! Yanatimizwa kwa kasi kubwa kupitia Mama Samia! Baraza la mawaziri ndio hilo sasa lipo! Mmeula wa chuya!
Naona wanajipendekeza tu, et oooh "Mama yetu".Ili Samia ayamalizie haya yaliyoanzishwa na mtangulizi wake, inatakiwa aingie na gia nzito.Hili Taifa limekuwa na wajuaji wengi sana, na akisema awasikilize hatafanya chochote.Leo wanakuja na hili kesho lile, azibe masikio kazi iendelee maana hawezi pendwa na wote.

Na kwenye u'VP asiweke mtu wa kuchekacheka, atembee na BASHIRU,uone kelele zao sasa.
 

Natena wiza

JF-Expert Member
Mar 13, 2021
310
500
Kati ya watu ambao hawatarudi kwenye nafasi zao za mawaziri Mwigulu ni mmoja wapo
Msiwe na matazamio makubwa sana, hiki ndo huwa kinawafanya mjae hasira mwisho wa mambo. Kwamba wewe tayari unajua kabisa mipango ya SAMIA au ndo mnajaza upepo, et moja Kati ya watu ambao hawatakuwepo kwenye Baraza,haya tutajie atakaeziba pengo lake.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
24,602
2,000
Nimememwelewa Mwigulu, Raisi alitakiwa kutoa taarifa Kwa Baraza, ni Baraza lipi? Kwa mazingira yake hilo Baraza lilikuwepo na hivyo busara aliyotumia Rais ya kusitiri mwili Kwanza then maswala ya kuvunja Baraza yaendelee ipo poa tuuu...anyway naweza kosolewa maana sio mtaalam wa Sheria Na katiba ....

..tangu lini kusitiri mwili kukawa muhimu kuliko KATIBA?

..you can do both, unafuata Katiba, na unasitiri mwili.
 

Natena wiza

JF-Expert Member
Mar 13, 2021
310
500
Wakati huo huo wewe hata mlo wa siku hauna uhakika nao
Tunataka mpunguze nyuzi na comment za kulia maisha magumu Sasa, au lasivyo mtafute chaka jingine la kuuficha uvivu wenu, maana aliewazuia kuwa matajiri ndani ya hii miaka sita hayupo tena.
 

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,780
2,000
Naona wanajipendekeza tu, et oooh "Mama yetu".Ili Samia ayamalizie haya yaliyoanzishwa na mtangulizi wake, inatakiwa aingie na gia nzito.Hili Taifa limekuwa na wajuaji wengi sana, na akisema awasikilize hatafanya chochote.Leo wanakuja na hili kesho lile, azibe masikio kazi iendelee maana hawezi pendwa na wote.

Na kwenye u'VP asiweke mtu wa kuchekacheka, atembee na BASHIRU,uone kelele zao sasa.
Ni kweli nimekuwa nataka nimuambie mama Samia avae sura ya kazi, asicheke na nyani ili kuepuka kuvuna mabua! Lazima awe 'tough' ili mambo yaende! Watakuja kiukanda, kidini, na nk! Akiwachekea tu twafwa!
 

Phoenix

JF-Expert Member
Sep 6, 2012
10,428
2,000
Mwigulu akija kupata madaraka makubwa, ataumiza na kuua watu mnoooo.

Narudia tena mnooooooooooooooooooo.

Weka madaraka makubwa mbali na Mwigulu. Siyo binadamu kabisa.

Na kibaya zaidi ni bingwa wa uchawa ili apewe vyeo. Kwa mfumo mbovu tulionao, no wonder huyu mtu akaja kuleta maafa tena makubwa mnoo.
Naunga mkono hoja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom