Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,333
- 24,227
View attachment 2933564
#Habari: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wateule kusimamia tatizo la wizi wa fedha unaofanywa na watumishi wa umma kwa kushirikiana na mitandao mingine nje ya serikali.
Rais Samia ameyasema hayo leo tarehe 13 Machi, 2024 wakati akiwaapisha viongozi wateule wakiwemo wakuu wa mikoa wapya na waliohamishwa vituo vya kazi na viongozi wengine katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
"Nataka mkasimamie pia mifumo ya ukusanyaji mapato, watu wanaiba fedha watu wote mko hapo, wakuu wa mikoa na wilaya mko hapo, kuna mitandao inachepusha fedha za halmashauri huko, kuna mtandao wa serikali na mtandao mwingine unaochepusha pesa, nashukuru Mbeya wamekuwa wa kwanza kutuambia tunafuatilia huo mtandao, na upo unaenda na wanaambizana wanachepusha pesa nyingi sana, lakini bado mnakaa huko sijui kitu gani kimeharibika mnahitaji pesa zinatoka wapi?"
Rais Samia
Dokta wa Uchumi kalewa kazi.
Amejitamba hadharahi kuwa sasa hakuna wizi wa fedha serikalini, na kwamba mama Samia kafanya makubwa kutokomeza kabisa wizi wa fedha za umma serikalini.
Mama kamgutua.
Ametoa mfano wa mtandao wa wizi wa fedha za serikali huko Mbeya.
Fedha zinaingia moja kwa moja mifukoni mwa watendaji wachache wajanja.
Dr Mwigulu Nchemba kalewa madaraka, uwaziri umemkolea hadi anasahau kazi.
Hili ni tatizo.
====
Oktoba 28, 2023 Dkt Mwigulu Nchemba alisema hakuna wizi wa fedha serikalini.