Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba awajibu TLS kuhusu Rais Samia Suluhu kuteua Baraza jipya la Mawaziri

Jackal

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
7,153
2,000
Nimesoma andiko la TLS, kwa heshima zote kwa chombo chetu hiki kilichopewa mamlaka kisheria, Nimeshtuka sana, I wish to say,

Kwanza KATIBA HAIJAVUNJWA KWA MHE RAIS SAMIA SULUHU kuapa, na wala hakuna Mkanganyiko wowote wa Kikatiba, kwa yeye kutoteua PM na Baraza jipya. Mmekaa wote kweli mkaona hivyo.

Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 42(5) kuna watu wa aina mbili wanaweza kuwa Rais. Moja, Rais Mteule ambaye anatokana na Ibara ya 42(1). Mbili, Mtu anayeshika kiti cha Rais ambaye anatokana na ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ambaye ni Makamu wa Rais. Kwa Mazingira haya, Makamu wa Rais, baada ya kifo cha Rais, anakuwa Kaimu Rais baadae ndio ameapa na kuwa RAIS wa Nchi. Rais Mteule anapatikana kutokana na uchaguzi. Hivyo basi ibara ya 57(2)(f) ya Katiba haitumiki katika mazingira haya. Kwa mjibu wa Sheria, Mhe Rais alitakiwa kutoa taarifa hii kwenye Baraza la Mawaziri baada ya kuapa na alifanya hivyo, maana yake Baraza lipo.

Hata hivyo kwa tamaduni za Kiafrika, kitanzania na Misingi ya UTU, SIONI KAMA NI JAMBO JEMA SANA KUANZA KUJADILI MGAWANYO WA MADARAKA TUNGALI HATA HATUJAMZIKA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU. HUU SIO MSIBA MDOGO, JAMBO HILI ZITO LIKO MIKONONI MWA RAIS WETU MAMA SAMIA SULUHU, HALAFU SISI TUANZE KUMPATIA MAMBO YA MARA TEUA PM, MARA VUNJA BARAZA, KATIBA INAELEKEZA RAIS KUAPA NA NAMNA YA KUMPATA MAKAMU WA RAIS.

KWA MJIBU WA KATIBA RAIS ANARUHUSIWA KUVUNJA BARAZA MUDA WOWOTE NA KUPANGA ATAKAVYO HATA SIO KWA MAZINGIRA KUAPA KWAKE,

KWANINI HATUIONI HEKIMA YAKE YA KUSHUGHULIKIA MSIBA KUMSITIRI KWANZA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU? TUNAANZA NA MAZISHI AU MIRATHI? 😭😭😭😭

Pia soma > TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14
 

Msukuma Original

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
928
1,000
Dah! Mwigulu kama anajua tupo kwenye msiba mzito ametoa wapi nguvu ya kuandika haya? Hapa ninachokiona ni namna ya kujipigia debe ili asiachwe kwenye baraza lijalo. Hakuna chochote cha msingi alichokiongea.

TLS wametoa mwanga kuhusu issue nzima ya kikatiba kuhusu hali iliyopo, sasa hapa Mwigulu hata haieleweki anaongea nini.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,272
2,000
Mwigulu Nchemba ! Upo? 😇 Natamani sana utumbuliwe moja kwa moja awamu hii! Sasa sijui kama MAMA yetu atapata huo ujasiri!

Wengine ni PM, yule mwenzako wa afya, Kabudi, Bashungwa (huyu hata kupiga dana dana sijui kama anaweza! Halafu eti ni Waziri wa michezo!), Kibabu George Mkuchika, Doto James, Ole Sabaya, na wengineo wengi!! Nyinyi mlikubuhu kwa unafiki, kujikomba komba na pia kumpotosha Mzee enzi za uhai wake.
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
6,200
2,000
Nimememwelewa Mwigulu, Raisi alitakiwa kutoa taarifa Kwa Baraza, ni Baraza lipi? Kwa mazingira yake hilo Baraza lilikuwepo na hivyo busara aliyotumia Rais ya kusitiri mwili Kwanza then maswala ya kuvunja Baraza yaendelee ipo poa tu. Anyway naweza kosolewa maana sio mtaalam wa Sheria Na katiba.
 

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
9,271
2,000
Mwigulu toka aliposema maiti zinatoka SA nilimpuuza sana na sintakuja kumuamini tena ukiona watu wanajifanya kuvaa bendera ya Tanzania muda mwingi jua wanafki tuu hakuna lolote. Sasa hapo anajibu kama nani Nchi ina mwanasheria Mkuu na majaji wanaotakiwa kulizungumzia hilo sio huyo asiejua kitu kabisaa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom