Waziri wa Fedha ameudanganya umma, si kweli kwamba hawezi kutengua tozo

Jerlamarel

JF-Expert Member
Sep 14, 2021
843
2,517
Jamani eeh, hivi hawa viongozi siku hizi wanatuonaje wananchi? Wanadhani kwamba tuko mambumbumbu kiasi hiko?

Iko hivi, siku zote muswada wa sheria hutungiwa nje ya bunge, kisha Bunge hutunga SHERIA MAMA, na baada ya hapo zinatungwa KANUNI na wizara husika.

Hivyo kwenye suala la tozo, Bunge halihusiki kuweka viwango vya tozo, lenyewe lilitunga sheria ya kwamba kutakuwa na "Government Levy" kutoka kwenye Electronic Money Transactions.

Baada ya hapo sasa Waziri husika anakaa na wataalamu wanaohusika kisha wanatunga kanuni. Sasa kwenye suala la tozo, ni kwamba Mwigulu asitake kulitupia mzigo Bunge maana lenyewe halitungi kanuni.

Na Waziri halazimiki kuweka rate kubwa, hata akiweka kanuni ya ZERO (0) AMOUNT still bado ni significant ama inakubalika kimahesabu. Hata akiweka senti kadhaa bado sawa tuu. Sasa kwa nini watuwekee tozo ya maelfu ilihali hali ya uchumi kwa sasa ni mbaya?

Hivyo hili likae sawa, Waziri aliyetunga kanuni hawezi kusema hili haliko ndani ya uwezo wake wakati ni yeye ndiye mtunga kanuni. Hata kama ni kuwapiga wananchi fix hizi ni fix za kijima, acheni siasa mpaka kwenye mambo ya msingi.
 
Tumkatae mtu huyu kwa nguvu zote
 
Back
Top Bottom