Waziri wa CUF aiporomoshea CHADEMA matusi!

Waziri wa CUF aiporomoshea CHADEMA matusi!

Status
Not open for further replies.
Tatizo moja la Chadema ni kuwa wenyewe siku zote wanajiona wapo sahihi kwa kila jambo.

Mimi nimeipenda sana makala hii ya Mh Juma Duni Haji, kwani amelenga penyewe hasa kwa kuituma kwenye gazeti lao.

Hakika huo ni ujasiri mkubwa sana kwa Juma Duni.

Hongera sana Mh Juma.

Sasa na wewe Dr. Mzima unashindwa kuona mwanacuf mwenzako alivyowaaibisha? Sasa kama huyu ni waziri anaandika utumbo je itakuwaje akiandika mwakilishi wa mji mkongwe!?
Duni ana hoja duni kama lilivyo jina lake.
 
Juma Duni Haji una mawazo DUNI!!

''Tarehe 22/08/2012 Mahakama Kuu Kanda ya Tabora ilitengua matokeo ya Uchaguzi Jimbo la Igunga na kuwapa ushindi wa kesi hiyo CHADEMA. Uchaguzi utarudiwa. Je, CHADEMA wamesaidiwa na Jaji wa Serikali ya CCM na hivyo na wao ni CCM-B? ''

KUMBE MAJAJI NI WA CCM ; NA KUMBE MAHAKAMA INATOA MSAADA.....
''

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mara kadhaa kwamba Tanzania ipo kwa sababu ya Zanzibar. Msimamo wetu ni kuwa wazanzibari hawako tayari tena kufanywa koloni la Tanganyika.Msimamo wetu ni kuwa wazanzibari hawako tayari tena kufanywa koloni la Tanganyika.'''


KUMBE LENGO LAKO NI KUONGELEA MUUNGANO NA WALA SIO CHADEMA WALA U-CCM B

WEWE TULIA ULE POSHO ZA SERIKALINI NA CCM-B WENZAKO.


 
Nimeishapata nakala yangu nimeishoma ipo ukurasa wa 18 nitahifadhi kama reference itananisaidia siku za mbele.
 
Iam not into politics ila Sijaona matusi!.. napenda sana duni akiongea Ile lafudhi na maneno anavyoyapanga..
 
Yaani mengine kayamezea maana kuna mengi hao CHADEMA wamekua wakishirikiana na CCM mbona hawaambiwi wao CCMB pumbavu zao chadema
 
Sasa na wewe Dr. Mzima unashindwa kuona mwanacuf mwenzako alivyowaaibisha? Sasa kama huyu ni waziri anaandika utumbo je itakuwaje akiandika mwakilishi wa mji mkongwe!?
Duni ana hoja duni kama lilivyo jina lake.

Hakika hii makala imemvua nguo DUNI na kumuacha utupu.
 
Me naona huyu jail bird kapagawa.hivi waziri mwenye akili timamu unaweza kuandika uhoro kama huu.kweli nimeami huyu x-convict jela imemuaribu ubongo.
 
Hivi nani anaweza kusimama na Juma Duni Hassan kwenye jukwaa na kupambanua mambo?

Juma Duni mbona yuko too senior kwa hawa magwanda? Hao Jussa tu wanamtosha kwa safu nzima ya magwanda. Unakumbuka alivyowachachafya Marando na Nape kwenye mdahalo?
 
Nani “CCM–B” CHADEMA au CUF?
Juma Duni Haji


Tanzania Daima Jumatano Makala | Oktoba 10, 2012

MADHUMUNI ya Chama cha wananchi (CUF) kama yalivyo katika Katiba yake ni, “Kuwaunganisha Watanzania wakatae uonevu, kudhalilishwa, kunyanyaswa, kubaguliwa au maovu mengine yanayoweza kufanywa dhidi ya heshima ya utu wa binadamu, yawe yanayotendwa na serikali, kikundi cha watu walio na uwezo kwa ajili ya mabavu yao au kwa ajili ya kujinufaisha kwao kiuchumi au kisiasa na kiitikadi au kwa kujali dini, kabila jinsia au rangi zao”. (Kifungu cha, 6[1] Katiba ya CUF uk.12)

Kwa kiasi miaka miwili sasa ndugu zetu wa CHADEMA wamekuwa wakifanikiwa wakisambaza na kufanya siasa nyepesi nyepepi za maji taka kwa Watanzania Bara kwamba eti CUF ni “CCM-B” kwa sababu ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (Government of National Unity Zanzibar).
Dhamiri yangu leo ni kufanya uchambuzi na kuweka wazi kwamba hoja ni “U-CCM-B” au choyo na kuchukizwa kwa CHADEMA kwa Wazanzibari kusikilizana? au ni ukosefu wa dira na agenda sahihi ya kisiasa?

Hoja hii ya “U-CCM–B” imerejewa tena na viongozi wa CHADEMA pale Mheshimiwa, Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia alipokubali uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa kumteua kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba kilichopo pale Zanzibar ni Serikali ya umoja wa kitaifa si vyama vya umoja wa kitaifa.

Hakuna Chama cha CUF wala CCM ambacho kimeungana na kufanya viwili hivyo kufanya umoja unaoitwa CCM-CUF Taifa au vinginevyo.

Serikali ya umoja wa kitaifa ilipatikana baada ya kura ya maoni ya tarehe 31 Julai, 2010 kupigwa na asilimia 66.3 ya Wazanzibari bila kujali ni chama gani walikubali kuundwa Serikali hiyo ya (GNU).

Ni wananchi wa Zanzibar si wanachama wa vyama waliopiga kura ya maoni. Tunapokutana katika Baraza la Mawaziri hatukutani viongozi wa vyama, bali ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (si Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi) wanaokutana na kujadili masuala ya maendeleo ya nchi yao na wala si maendeleo ya vyama vyao.

Wakati wowote chama cha Mapinduzi wanapokutana huwa wanazungumza masuala ya chama chao na CUF huzungumza chama chao. Kwenye baraza la mawaziri tunazungumza nyaraka za wizara za Serikali siyo za idara ya chama chochote kati ya hivyo viwili. Sasa huu “U-CCM-B au A” unatoka wapi.

Hebu tuone “UCCM-B” upo wapi?
Madhumuni ya Chama cha wananchi CUF kama yalivyo katika Katiba yake kifungu cha, 6 (8) Katiba ya CUF uk.13) ni “kushika hatamu za dola ili dola au serikali itekeleze vizuri itikadi na sera za chama na ustawi wa taifa letu”.

Chama cha siasa ambacho hakina malengo ya kuunda serikali na au kuingia serikalini kuweza kusimamia utekelezaji mzuri wa sera na itikadi na badala yake inajielekeza katika kazi ya kulipua “MABOMU” na kung’ang’ania kupiga kelele za ufisadi hali chama chenyewe na watendaji wake wakiamini kuwa ufisadi ni sehemu ya njia ya kupata manufaa ya kisiasa na kiuchumi, tunavishukuru vyombo vya habari kwa kutujulisha kuhusu hali hii.

Hebu tujikumbushe tuone “UCCM-B” upo wapi? Mwaka 1991 Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi Rais wa CCM alimteua Mabere Marando (NCCR) kuwa mjumbe wa Tume ya kuratibu maoni ya wananchi juu kuanzishwa mfumo wa chama kimoja au vyama vingi chini ya Mwenyekiti Jaji Nyalali, Mwaka 2001.

Mabere Marando huyu huyu alichaguliwa na bunge kuwa Mbunge wa Bunge la EAC akiwa NCCR Mageuzi na kumshida marehemu Bob Makani aliyesimamishwa na CHADEMA, CHADEMA wakarudia, lugha hii wanayowaambia Wazanzibari kwamba NCCR Mageuzi ni CCM-B.

Leo Marando ni CHADEMA, U-CCM–B wake umeyayuka maana kaingia katika chama kitakatifu kinachopokea maono kutoka kwa Mungu?
Mwaka 2008, Rais Jakaya Kikwete alimteua Zitto Kabwe kuwa mjumbe wa Kamati ya Madini chini ya mzee Jaji Mark Bomani. Iliandikwa kuwa Mbowe amekatisha masomo yake kutoka nchini Ujerumani kuja kwenye kikao kuthibitisha uteuzi huo.

Si Zitto Kabwe wala chama cha CHADEMA kilichojitangaza kuwa wao ni CCM-B ! , Mwaka huu Rais Kikwete amemteua Profesa Mwesiga Baregu kuwa mjumbe wa Kamati ya kuratibu maoni ya uandikwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Viongozi wa CHadema, Dk. Wilbroad Slaa na Mbunge wa Singida Vijijini, Tundu Lissu, wakampongeza Rais Kikwete na Profesa Baregu, lakini muasisi wa CHADEMA akasema uteuzi huo wa Rais Kikwete una “UDINI” akimaanisha WAISLAMU WAMO KATIKA HUO UTEUZI WA KIKWETE!. Hata hivyo CHADEMA haijawa CCM-B.

John Mnyika na Tundu Lissu walikuwa na kesi za uchaguzi dhidi ya CCM kule Singida na pale Ubungo. Kesi hizi wameshinda zote chini ya utetezi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya CCM.

Hawasemwi kwamba wametetewa na mwanasheria wa serikali ya CCM na hivyo ni CCM-B!, Aprili 17, 2012 umefanyika uchaguzi mwingine wa EAC pale bungeni na CHADEMA walikuwa na wabunge 43 kati ya 48 wa chama hicho wakati kura zikipigwa.

Anthony Komu mgombea wa CHADEMA alipata kura 93, kura 50 kati ya hizo zilikua za wabunge wa CCM. CHADEMA wakaenda mahakamani ili uchaguzi urudiwe ili wapate nafasi ya kuwapata wabunge zaidi kumchagua Komu. Hapa UCCM-B. Haukuwepo?

Tarehe 22/08/2012 Mahakama Kuu Kanda ya Tabora ilitengua matokeo ya Uchaguzi Jimbo la Igunga na kuwapa ushindi wa kesi hiyo CHADEMA. Uchaguzi utarudiwa. Je, CHADEMA wamesaidiwa na Jaji wa Serikali ya CCM na hivyo na wao ni CCM-B?

James Mbatia alikuwa na kesi ya uchaguzi ya Jimbo la Kawe lakini akashindwa na Halima Mdee (CHADEMA). Mbatia akaenda Mahakamani kisheria. Viongozi wa CHADEMA wakatafuta njia za kiungwana kumaliza tatizo hilo nje ya Mahakama.

Februari 6 2012, makatibu wakuu wa NCCR-Mageuzi Samwel Ruhuza na Dk. Slaa walikubaliana kufuta kesi hiyo No.101/2010 na kumuacha Halima Mdee abaki kuwa Mbunge. Je, Halima naye ni NCCR-B au Mbatia ni CHADEMA -B?

Mwaka 2001 Rais Benjamin Mkapa, alimteua Hamad Rashid kuwa Mbunge wa Wawi (CUF), wakati huo siasa za ushabiki na mapambano zilikuwa kubwa mno na CHADEMA kilikuwepo, hoja ya CCM-B hawakuisema.

Mwaka 2009 Rais Kikwete alimteuwa Ismail Jusa kuwa mbunge, hoja za “UCCM-B” haikuwepo! Mwalimu Nyerere aliwahi kumpigia kura James Ndobho wa NCCR-Mageuzi Jimbo la Musoma Mjini na Ndobho akashinda, je, Nyerere alikuwa NCCR?

Kuna lugha ya kiswahili ya kuonewa kwa Bata kwa sababu tu ya umbo na sifa zake. Bata akitembea huambiwa anakata viuno kama mrembo wa Tanzania. Hivyo ndivyo alivyoumbwa, hakuchagua kukata viuno anapotembea na wala hajui kwamba anafanya hivyo. Bata huyu huyu anapotafuta chakula kwenye tope huambiwa anakula uchafu.

Sina hakika kwamba CHADEMA wanapokubali uteuzi wa rais huyu huyu ikawa ni sahihi chakula chao safi, lakini wengine wanapoteuliwa na rais, kwa CHADEMA huwa sawa na kula tope za choo.

Kwa CHADEMA kuku anapokwenda haja kubwa huwa anakunya, lakini bata huambiwa kaharisha, hakunya. Ukweli ni kwamba wote wamekunya, mmoja amekunya kutu ngumu mwingine kanya kutu laini, wote wamekunya mavi ya kuku na yote yananuka.

Vipi CHADEMA wao wajione watakatifu wanapopata uteuzi kwa rais wengine wawe wamekufuru, huu ni unafiki na uzandiki wa viongozi wanaotaka eti wapewe dhamana ya kuongoza nchi kwa akili kama za Panzi.

Kule Kigoma CCM na CHADEMA walikubaliana na CCM kuunda serikali ya Halmashauri ya Kigoma nusu kwa nusu ya madiwani kwa miaka mitano. Hoja ya CCM kuiona CHADEMA CCM-B haikutajwa, yaani yale kwa CHADEMA yalikuwa na mavi ya kuku CUF na CCM Zanzibar ni uharo wa bata.

Kule Arusha kulikuwa na serikali ya aina hiyo, mpaka yalipotokea malumbano na upuuzi wa wawakilishi wa wananchi madiwani walipozuiliwa na chama chao CHADEMA kuwawakilisha barazani.

Wengi tumezoeshwa kwamba siasa ni uongo na mchezo mchafu. Hapana. Moja ya suala ambalo CUF na viongozi wake tunalisimamia na kutaka watanzania waamini kuwa siasa si uongo wala si mchezo mchafu bali baadhi ya wanasiasa ndio waongo na wachafu.

Kama viongozi wanaweza kusema uongo wa kiwango cha uharo wa bata wakiwa nje ya Ikulu watakunya nini hawa wakiingia Ikulu? Kama kuna viongozi wanaweza kuiba wake za watu na kuja jukwaani kujisifu kwamba wao ni wezi wa wake za watu, je, wakiwa Ikulu watafanyaje hawa? Watawapanga foleni wanawake wote waliopo pale kwa uwezo wa madaraka yao ya urais na kuwalazimisha kufanya nao ngono.

Hivyo tunategemea hawa wakajenge nyumba ya umalaya pale Ikulu. Je, nyie ndiyo mnashangilia hayo? Eti kunja ngumi, ngumi gani ya wizi wa wake za watu? Eti kunja ngumi, ngumi ya kutengeneza vifo vya Watanzania wenzetu?

Watanzania mna kila sababu za kutafakari na kuchukua maamuzi sahihi juu ya hatima na mustakbali wa maisha yenu ya sasa na kizazi kijacho, wapi pa kuunganisha nguvu zenu ili mabadiliko ya kweli kiuchumi na kisiasa yaweze kupatikana. Siasa za milipuko na mihemuko za leo linasemwa hili na kesho linasemwa vinginevyo jambo hilo hilo hazina nafasi kwa CUF ya DIRA YA MABADILIKO.

Suala la U-A na U-B, unatoka wapi na unakujaje katika mahusiano ya chama kimoja na kingine wakati kilichojenga umoja ni ridhaa ya Wazanzibari?
Mwaka 2005 hadi 2010, wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) kiliunda kambi ya upinzani na wabunge wa CHADEMA bungeni kwa miaka mitano, na Dk. Slaa akawa Naibu Kiongozi wa kambi hiyo kwa muda wote wa miaka mitano.

Mheshimiwa Zitto na wabunge wengine wa chama hiki wakishika nyadhifa za uwaziri kivuli wa kambi hiyo. Ilikuwa ni Serikali kamili nje ya Serikali ya Muungano. Vyama viwili hivi viliendelea kubaki na shughuli zake ndani na nje ya Bunge.

Mbona hoja ya CHADEMA kujiita CUF-B haikuja wala hawakujigamba hivyo kuwa wao ni CUF-B? Chama cha wananchi CUF kilifanya hivyo kwa sababu madhumuni yake ni: “Kuwaunganisha Watanzania wakatae uonevu, kudhalilishwa, kunyanyaswa, kubaguliwa au maovu mengine yanayoweza kufanywa dhidi ya heshima ya utu wa binaadama, yawe yanayotendwa na Serikali, kikundi cha watu walio na uwezo kwa ajili ya mabavu yao au kwa ajili ya kujinufaish kwao kiuchumi au kisiasa na kiitikadi au kwa kujali dini, kabila jinsia su rangi zao”.

Muda wote huu vyama vya upinzani tumeshindwa kuungana na kukiondoa chama cha CCM kwa sababu ya udhaifu huu wa CHADEMA kujikubalisha kujigawa mafungu huku CCM ikichekelea na kutuona wajinga. Ujinga na upumbavu huu umezidi tulipogundua kwamba viongozi wa CHADEMA wanaonesha udhaifu wao kwa kukosa furaha kuwaona Wazanzibari wanasikilizana na nyinyi wananchi mnafurahia hilo kwamba tuaachwe Wazanzibari tuuane na kwamba eti hicho ndiyo chama mnachokitaka eti kiingie Ikulu.

Msimamo huu wa CHADEMA ni kuthibitisha kwamba Wazanzibari kugombana ndiyo furaha ya viongozi wa chama hicho, maana furaha na agenda ya muda mrefu ya baadhi ya viongozi watanganyika wawe wa CCM au CHADEMA ni kuhakikisha Wazanzibari tunawagawa ili tuwatawale.

Kama hivyo ndivyo wazanzibari hatuna sababu ya kushanga ya jinsi viongozi wenzetu wa Tanganyika mnavyotuona, maana sisi wazanzibari ambao wazee wetu kina mzee Karume na Mzee Thabit Kombo walimuamini Mwalimu Nyerere kwa kuunganisha nchi mbili hizi kwa faida ya pande mbili.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mara kadhaa kwamba Tanzania ipo kwa sababu ya Zanzibar. Msimamo wetu ni kuwa wazanzibari hawako tayari tena kufanywa koloni la Tanganyika. Kinachohitajika sasa ni kurekebisha makosa yaliyofanywa miaka 50 iliyopita yaliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere mwaka 1964.

Ninachotaka kuwakumbusha Watanzania ni kwamba Mimi binafsi na wenzangu wengi ni wahanga wakubwa wa siasa mbovu za zamani za Zanzibar, tuliathirika sana kwa kubambikiwa kesi za uhaini na kesi za mauaji.

Leo ni waziri wa serikali ya umoja wa kitaifa siyo umoja wa vyama vya CCM na CUF. Wazanzibar tumemaliza matatizo yetu ya ndani wenyewe, tumeamua kujenga nchi yetu, wakati nyinyi yenu mnaitayarisha ibomoke, sisi huko tumeshatoka.

Fursa ya kujenga siasa za kistaarabu, siasa za heshima, siasa zenye lengo la kuwasaidia watu wetu kuondokana na lindi la umaskini, maradhi na ujinga ipo, Hatujachelewa!

Tuutumie vema mchakato wa uratibu wa ukusanyaji maoni ya katiba, ipendekezwe uwepo wa uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa, CUF katika manifesto yetu ya mwaka 2010 tulilieleza hili. CUF chini ya dira ya mabadiliko inaamini katika mazungumzo.

Namaliza kwa kuwaambia Zanzibar kuna Serikali ya umoja wa kitaifa. Hakuna muungano wa vyama vya kitaifa, wala hakuna CCM-B wala CUF –G. Kilichopo ni serikali si vyama kuunganisha nguvu kujenga taifa letu.

Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu Ibariki Zanzibar!

Muandishi wa makala hii ni Waziri wa Afya wa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi CUF Taifa. Harakati za kisiasa zilimuweka ndani bila kuhukumiwa kwa miaka minne.
Ndoa imeharamishwa na wanauamsho!! wamepeana talaka rejea!!
 
Kama viongozi wanaweza kusema uongo wa kiwango cha uharo wa bata wakiwa nje ya Ikulu watakunya nini hawa wakingia Ikulu "Juma Duni"
 
Juma Duni mbona yuko too senior kwa hawa magwanda? Hao Jussa tu wanamtosha kwa safu nzima ya magwanda. Unakumbuka alivyowachachafya Marando na Nape kwenye mdahalo?
Kuna tofauti ya utaalamu wa fitna na kuchambua mambo! wote Duni, Jussa ni maprofesa wa fitna tu!!
 
ukisoma makala hii imeja dhambi ya ubaguzi. anawahamasisha wazanzibar wajeenge ndio msingi wa hoja. zanzibar kama munatajitoeni kweye muungano. watanganyika wataishi kwa amani sana ilia ninyi mtagombana mpaka basi. jaribuni ila hautawarudisha kaitika muungano tena,ninachoona ni udini na ukabila wa mwandishi wa makala hii
 
When all is said done bila umoja wa upinzani kuingoa ccm kwenye madaraka will remain a pleasing illusion to be pursued but never attained -borrowing Bobs words.
kwenye red...stop lying


That until that day
The dream of lasting peace,
World citizenship
Rule of international morality
Will remain in but a fleeting illusion to be pursued,
But never attained -
Now everywhere is war - war.
 
Madhumuni ya Chama cha wananchi CUF kama yalivyo katika Katiba yake ni, "Kuwaunganisha watanzania wakatae uonevu,kudhalilishwa,kunyanyaswa,kubaguliwa au maovu mengine yanayoweza kufanywa dhidi ya heshima ya utu wa binaadama, yawe yanayotendwa na Serikali, kikundi cha watu walio na uwezo kwa ajili ya mabavu yao au kwa ajili ya kujinufaisha kwao kiuchumi au kisiasa na kiitikadi au kwa kujali dini, kabila jinsia au rangi zao". (Kifungu cha, 6[1] Katiba ya CUF uk.12)

Na, JUMA DUNI HAJI

Kwa kiasi miaka miwili sasa ndugu zetu wa CHADEMA wamekuwa wafanikiwa wakisambaza na kufanya siasa nyepesi nyepepi za maji taka kwa watanzania bara kwamba eti CUF ni "CCM-B" kwa sababu ya kuunda Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar (Government of National Unity Zanzibar) Dhamiri yangu leo ni kufanya uchambuzi na kuweka wazi kwamba hoja ni "U-CCM-B" au choyo na Kuchukizwa kwa CHADEMA kwa wazanzibari kusikilizana? au ni ukosefu wa dira na agenda sahihi ya kisiasa? Hoja hii ya "U-CCM–B" imerejewa tena na viongozi wa CHADEMA pale Mheshimiwa. James Mbatia alipokubali uteuzi wa Rais Kikwete wa kumteua kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba kilichopo pale Zanzibar ni SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA SIYO VYAMA VYA UMOJA WA KITAIFA. Hakuna chama cha CUF wala CCM ambacho kimeungana na kufanya viwili hivyo kufanya umoja unaoitwa CCM-CUF Taifa au vinginevyo. Serikali ya umoja wa kitaifa ilipatikana baada ya kura ya maoni ya Tarehe 31 Julai, 2010 kupigwa na asilimia 66.3 ya wazanzibari bila kujali ni chama gani walikubali kuundwa Serikali hiyo ya GNU. Ni wananchi wa Zanzibar siyo wanachama wa vyama waliopiga kura ya maoni. Tunapokutana katika baraza la mawaziri hatukutani viongozi wa vyama , bali ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (Siyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi) wanaokutana na kujadili masuala ya maendeleo ya nchi yao na wala si maendeleo ya vyama vyao, wakati wowote chama cha Mapinduzi wanapokutana huwa wanazungumza masuala ya chama chao, na CUF huzungumza chama chao. Kwenye baraza la mawaziri tunazungumza nyaraka za wizara za Serikali siyo za idara ya chama chochote kati ya hivyo viwili. Sasa huu "U-CCM-B au A" unatoka wapi.

Kama hoja ni chama kuingia Serikalini! Hebu tuone "UCCM-B" upo wapi?
Madhumuni ya Chama cha wananchi CUF kama yalivyo katika Katiba yake kifungu cha, 6[8] Katiba ya CUF uk.13) ni "kushika hatamu za dola ili dola au serikali itekeleze vizuri itikadi na sera za chama na ustawi wa Taifa letu" Chama cha siasa ambacho hakina malengo ya kuunda serikali na au kuingia serikalini kuweza kusimamia utekelezaji mzuri wa sera na itikadi na badala yake inajielekeza katika kazi ya kulipua "MABOMU" na kung'ang'ania kupiga kelele za ufisadi hali chama chenyewe na watendaji wake wakiamini kuwa ufisadi ni sehemu ya njia ya kupata manufaa ya kisiasa na kiuchumi, tunavishukuru vyombo vya habari kwa kutujulisha kuhusu hali hii. Hebu tujikumbushe tuone "UCCM-B" upo wapi? Mwaka 1991 Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi Rais wa CCM alimteua Mabere Marando (NCCR) kuwa mjumbe wa Tume ya kuratibu maoni ya wananchi juu kuanzishwa mfumo wa Chama kimoja au vyama vingi chini ya Mwenyekiti Jaji Nyalali, Mwaka 2001, Mabere Marando huyu huyu alichaguliwa na bunge kuwa Mbunge wa Bunge la EAC akiwa NCCR na kumshida marehemu Bob Makani aliyesimamishwa na CHADEMA, CHADEMA wakarudia, lugha hii wanaowaambia wazanzibari kwamba NCCR Mageuzi ni CCM-B. Leo Mheshimiwa. Marando ni CHADEMA, U-CCM–B wake umeyayuka maana kaingia katika chama kitakatifu kinachopokea maono kutoka kwa Mungu?

Mwaka 2008 Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alimteua Zitto Kabwe kuwa mjumbe wa Kamati ya Madini chini ya Mzee Jaji Mark Bomani. Iliandikwa kuwa Mheshimiwa Mbowe amekatisha masomoni yake kutoka nchini ujerumani alikuja kwenye kikao kuthibitisha uteuzi huo, Si Zitto Kabwe wala chama cha CHADEMA kilichojitangaza kuwa wao ni CCM-B ! , Mwaka huu Rais Kikwete amemteua Prof. Mwesiga Baregu kuwa mjumbe wa Kamati ya kuratibu maoni ya uandikwaji wa katiba ya Jamhuri ya Muungano. Viongozi wa CHADEMA Mr. Slaa na Tundu Lissu wakampongeza Rais na Prof. Baregu, lakini muasisi wa CHADEMA akasema uteuzi huo wa Mheshimiwa Kikwete una "UDINI" akimaanisha WAISLAMU WAMO KATIKA HUO UTEUZI WA KIKWETE!!! HATA hivyo CHADEMA haijawa CCM-B.

John Mnyika na Tundu Lissu walikua na kesi za uchaguzi dhidi ya CCM kule Singida na pale Ubungo. Kesi hizi wameshinda zote chini ya utetezi wa mwanasheria Mkuu wa Serikali ya CCM. Hawasemwi kwamba wametetewa na mwanasheria wa serikali ya CCM na hivyo ni CCM-B!, April 17, 2012 umefanyika uchaguzi mwengine wa EAC pale bungeni na CHADEMA walikua na wabunge 43 kati ya 48 wa chama hicho wakati kura zikipigwa. Antony Komu mgombea wa CHADEMA alipata kura 93, kura 50 kati ya hizo zilikua za wabunge wa CCM. CHADEMA wakaenda mahakamani ili uchaguzi urudiwe ili wapate nafasi ya kuwapata wabunge zaidi kumchagua Komu. Hapa UCCM-B. haukuwepo? Tarehe 22/08/2012 Mahakama kuu kanda ya Tabora imetengua matokeo ya Uchaguzi Jimbo la Igunga na kuwapa ushindi wa kesi hiyo CHADEMA. Uchaguzi utarudiwa. Jee CHADEMA wamesaidiwa na Jaji wa Serikali ya CCM na hivyo na wao ni CCM-B? Mheshimiwa, James Mbatia alikua na kesi ya uchaguzi ya Jimbo la Kawe lakini akashindwa na Halima Mdee (CHADEMA). Mbatia akaenda Mahakamani kisheria. Viongozi wa CHADEMA wakatafuta njia za kiungwana kumaliza tatizo hilo nje ya Mahakama. Tarehe 6 Februari 2012 makatibu wakuu wa NCCR-Mageuzi Samwel Ruhuza na Wilbroad Slaa walikubaliana kufutwa kwa kesi hiyo No.101/2010 na kumuacha Halima Mdee abaki kuwa Mbunge. Jee Halima nae ni NCCR-B au Mbatia CHADEMA-B?

Mwaka 2001 Rais Mkapa alimteua Mh. Hamad Rashid kuwa Mbunge, wakati huo siasa za ushabiki na mapambano zilikua kubwa mno na CHADEMA kilikuwepo- hoja ya CCM-B hawakuisema. Mwaka 2009 Mheshimiwa Rais Kikwete alimteuwa Mheshimiwa, Ismail Jusa kuwa Mbunge Hoja za "UCCM-B" haikuwepo! Mwalimu Nyerere aliwahi kumpigia kura Paulo Ndorobo wa NCCR-Mageuzi jimbo la Musoma na Mheshimiwa Ndorobo akashinda Nyerere alikuwa NCCR?

Kuna lugha ya kiswahili ya kuonewa bata kwa sababu ya umbo na sifa zake. Bata akitembea huambiwa anakata viuno kama mrembo wa Tanzania. Hivyo ndivyo alivyoumbwa, hakuchagua kukata viuno anapotembea na wala hajui kwamba anafanya hivyo. Bata huyu huyu anapotafuta chakula kwenye tope huambiwa anakula uchafu sina hakika kwamba CHADEMA wanapokubali uteuzi wa Rais huyu huyu ikawa ni sahihi chakula chao safi, lakini wengine wanapoteuliwa na Rais, kwa CHADEMA hua sawa na kula tope za choo. Kwa CHADEMA kuku anapokwenda haja kubwa hua anakunya, lakini bata huambiwa kahara, hakunya: wote wamekunya mmoja amekunya kutu ngumu mwengine kanya kutu laini, wote wamekunya mavi ya kuku na yote yananuka.Vipi CHADEMA wao wajione watakatifu wanapopata uteuzi kwa Rais wengine wawe wamekufuru, huu ni unafiki na uzandiki wa viongozi wanaotaka eti wapewe dhamana ya kuongoza nchi kwa akili kama za Panzi. Kule Kigoma CCM na CHADEMA walikubaliana na CCM kuunda Serikali ya Halmashauri ya Kigoma nusu kwa nusu ya madiwani kwa miaka mitano. Hoja ya CCM kuioa CHADEMA CCM-B haikutajwa, yaani yale kwa CHADEMA yalikua na mavi ya kuku CUF na CCM Zanzibar ni uharo wa bata. Kule Arusha kulikua na Serikali ya aina hiyo, mpaka yalipotokea malumbano na upuuzi wa wawakilishi wa wananchi [madiwani] walipozuiliwa na chama chao CHADEMA kuwawakilisha barazani.

Wengi tumezoweshwa kwamba siasa ni uongo na mchezo mchafu, Hapana, Moja ya suala ambalo CUF na viongozi wake tunalisimamia na kutaka watanzania waamini kuwa Siasa si uongo wala si mchezo mchafu bali baadhi ya wafanya siasa[wanasiasa] ndio waongo na wachafu. Kama viongozi wanaweza kusema uongo wa kiwango cha uharo wa bata wakiwa nje ya Ikulu watakunya nini hawa wakiingia ikulu? Kama kuna viongozi wanaweza kuiba wake za watu na kuja jukwaani kujisifu kwamba wao ni wezi wa wake za watu, jee wakiwa ikulu watafanyaje hawa?, watawapanga foleni wanawake wote waliopo pale kwa uwezo wa madaraka yao ya urais na kuwalazimisha kufanya nao ngono. Hivyo tunategemea hawa wakajenge nyumba ya umalaya pale ikulu, je nyie ndiyo munashangilia hayo? Eti kunja ngumi, ngumi gani ya wizi wa wake za watu? Eti kunja ngumi, ngumi ya kutengeneza vifo vya watanzania wenzetu? Watanzania muna kila sababu za kutafakari na kuchukua maamuzi sahihi juu ya hatma na mustakbali wa maisha yenu ya sasa na kizazi kijacho, wapi pa kuunganisha nguvu zenu ili mabadiliko ya kweli kiuchumi na kisiasa yaweze kupatikana. Siasa za milipuko na mihemuko za leo linasemwa hili na kesho linasemwa vinginevyo jambo hilohilo hazina nafasi kwa CUF ya DIRA YA MABADILIKO.

SUALA LA U-A na U-B unatoka wapi na unakujaje katika mahusiano ya chama kimoja na kingine wakati kilichojenga umoja ni ridhaa ya wazanzibari. Mwaka 2005 hadi 2010, wabunge wa Chama cha wananchi CUF kiliunda kambi ya upinzani na wabunge wa CHADEMA bungeni kwa miaka mitano, na Dk. Slaa akawa Naibu kiongozi wa kambi hiyo kwa muda wote wa miaka mitano. MheshimiwaZitto na wabunge wengine wa chama hiki wakishika nyadhifa za uwaziri kivuli wa Kambi hiyo. Ilikua ni Serikali kamili nje ya Serikali ya Muungano. Vyama viwili hivi viliendelea kubaki na shughuli zake ndani na nje ya Bunge. Mbona hoja ya CHADEMA kujiita CUF-B haikuja wala hawakujigamba hivyo kuwa wao ni CUF-B? Chama cha wananchi CUF kilifanya hivyo kwa sababu madhumuni yake ni: "Kuwaunganisha watanzania wakatae uonevu,kudhalilishwa,kunyanyaswa,kubaguliwa au maovu mengine yanayoweza kufanywa dhidi ya heshima ya utu wa binaadama, yawe yanayotendwa na Serikali, kikundi cha watu walio na uwezo kwa ajili ya mabavu yao au kwa ajili ya kujinufaish kwao kiuchumi au kisiasa na kiitikadi au kwa kujali dini, kabila jinsia su rangi zao".

Muda wote huu vyama vya upinzani tumeshindwa kuungana na kukiondoa chama cha CCM kwa sababu ya udhaifu huu wa CHADEMA kujikubalisha kujigawa mafungu huku CCM ikichekelea na kutuona wajinga. Ujinga na upumbavu huu umezidi tulipogundua kwamba Viongozi wa CHADEMA wanaonesha udhaifu wao kwa kukosa furaha kuwaona wazanzibari wanasikilizana na nyinyi wananchi munafurahia hilo kwamba tuaachwe wazanzibari tuuwane na kwamba eti hicho ndiyo chama munachokitaka eti kiingie Ikulu. Msimamo huu wa CHADEMA ni kuthibitisha kwamba Wazanzibari kugombana ndiyo furaha ya viongozi wa Chama hicho, maana furaha na agenda ya muda mrefu ya baadhi ya viongozi watanganyika wawe wa CCM au CHADEMA ni kuhakikisha WAZANZIBARI tunawagawa ili tuwatawale (divide and rule them) Kama hivyo ndivyo wazanzibari hatuna sababu ya kushangaa ya jinsi viongozi wenzetu wa Tanganyika munavyotuona, maana sisi wazanzibari ambao wazee wetu akina mzee Karume na Mzee Thabit Kombo walimuamini mwalimu Nyerere kwa kuunganisha nchi mbili hizi kwa faida ya pande mbili, leo vijana wake waliorithi siasa zake wanaziendeleza kwa kutuambia eti Zanzibar siyo nchi. Wakati viongozi (Tundu Lissu) wanafurahia na kushikilia kwamba Zanzibar siyo nchi, chama hicho hicho kinashikilia hadharani kupitia kwa Joshua Nassari mbunge wa CHADEMA wa Arumeru Maashariki, anapendekeza na kusisitiza kuwa mikoa ya kaskazini ya Tanganyika kujitenga na kua taifa pekee. CUF hatuamini katika siasa za kikabila na kuigawa nchi mapande pande kwa siasa za itikadi za kimajimbo. Maana kama Arusha ijitenge na wasukuma wa Mwanza na Shinyanga ambao ni wengi na ni mikoa miwili tajiri kuliko mikoa yote nao pia watajitenga na wale wa Mbeya watajitenga na wale kusini kwa wamakonde nao watajitenga. Kwa hivyo hata hiyo Tanganyika pia haitokuwepo. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mara kadhaa kwamba Tanzania ipo kwa sababu ya Zanzibar. Msimamo wetu ni kuwa wazanzibari hawako tayari tena kufanywa koloni la Tanganyika. Kinachohitajika sasa ni kurekebisha makosa yaliyofanywa miaka 50 iliyopita yaliyoasisiwa na mwalimu Nyerere mwaka 1964.

Ninachotaka kuwakumbusha watanzania na Machadema, ni kwamba Mimi binafsi na wenzangu wengi ni wahanga wakubwa wa siasa mbovu za zamani za Zanzibar, tuliathirika sana kwa kubambikiwa kesi za uhaini na kesi za mauaji, leo ni waziri wa Serikali ya umoja wa kitaifa siyo umoja wa vyama vya CCM na CUF. Wazanzibar tumemaliza matatizo yetu ya ndani wenyewe, tumeamua kujenga nchi yetu, wakati nyinyi yenu munaitayarisha ibomoke, sisi huko tumeshatoka. Fursa ya kujenga siasa za kistaarabu, siasa za heshima, siasa zenye lengo la kuwasaidia watu wetu kuondokana na lindi la umasikini, maradhi na ujinga ipo, HATUJACHELEWA! Tuutumie vyema mchakato wa uratibu wa ukusanyaji maoni ya katiba, ipendekezwe uwepo wa UUNDWAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA, CUF katika manifesto yetu ya mwaka 2010 tuliieleza hili. CUF chini ya dira ya mabadiliko[vision for change] inaamini katika mazungumzo [dialogue],

Kwa hivyo CHADEMA angalieni siasa zenu kama mnataka kuendelea na siasa za kuonja umwagaji wa damu kisha ndo muamini juu ya ‘diablogue' endeleeni kujaribu, kama munaamini kuwa njia siasa hizo mnazozitaka zisizo na ushirikiano na wenzenu, siasa za nchi isitawalike, siasa za maandamano, siasa za propaganda chafu, siasa za kubaka wake za watu, siasa za kutaja mafisadi wazuri na mafisadi wabaya, kama mnaamini kufanya hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo kutoka kwa Mungu. Namaliza kwa kuwaambia Zanzibar kuna Serikali ya umoja wa kitaifa , hakuna muungano wa vyama vya kitaifa, wala hakuna CCM-B wala CUF –G. Kilichopo ni Serikali siyo vyama kuunganisha nguvu kujenga taifa letu. Na ndugu zangu watanganyika hamtaweza katu kumaliza migogoro yenu ya kisiasa na kidini kama hamukuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu Ibariki Zanzibar!

Muandishi wa makala hii ni waziri wa Afya wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar na mjumbe wa baraza kuu la uongozi CUF Taifa. Harakati za kisiasa zilimuweka ndani bila kuhukumiwa miaka mine[4]

Chanzo cha makala hii ni http://cuf2015plus.wordpress.com/2012/10/10/nani-ccm-b-chadema-au-cuf/
 
Hiyo makala ilitakiwa iishie Chumbe. Kuvuka bahari ni kujivunjia heshma na ndicho huyo Duni alichofanya. Haipendezi hata kidogo kwa mtu mzima kutoa kauli zinazokinzana kwa sababu tu ya kufarahisha watu. Duni anaongelea Tanzania ipi wakati haamini anachosema? Na bila aibu anamalizia kwa kusema 'Mungu ibariki Tanzania!

Mkuu wangu bado nasimamia maneno ya Wilcard kwamba huyu jamaa alipata hitilafu ya ubongo alipowekwa ndani na Salmin.
 
ukisoma makala hii imeja dhambi ya ubaguzi. anawahamasisha wazanzibar wajeenge ndio msingi wa hoja. zanzibar kama munatajitoeni kweye muungano. watanganyika wataishi kwa amani sana ilia ninyi mtagombana mpaka basi. jaribuni ila hautawarudisha kaitika muungano tena,ninachoona ni udini na ukabila wa mwandishi wa makala hii

You get the point.
 
CHADEMA toeni hoja wacheni kebehi na bla bla!! Juma duni katoa hoja murua na kafafanua kwa maelezo yenye kina hivyo CDM wacheni siasa uchwara na jibuni hoja kimantiki!!!!!
Wa TZ hatudanganyiki tena!!!
 
Kama viongozi wanaweza kusema uongo wa kiwango cha uharo wa bata wakiwa nje ya Ikulu watakunya nini hawa wakingia Ikulu "Juma Duni"
HUYU NDO MWONGO MKUBWA
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam hadi mikoa ya Kanda ya Ziwa - Nzega, Tabora. 2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini. 3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria – Igunga. 4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) – Shinyanga. 5. Kumaliza migogoro ya ardhi nchini – Dodoma. 6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini. 7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma. 8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi – Kagera. 9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi – Kagera. 10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini. 11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini. 12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda – Kagera. 13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme – Kagera. 14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu – Kagera. 15. Hukumu kwa waliopatikana na hatia ya kuua albino – Mbeya. 16. Kununua meli kubwa kuliko mv Bukoba – Kagera. 17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali. 18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika – Mwanza. 19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalumu chenye vifaa kupambana na wahalifu – Mwanza. 20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani – Geita. 21. Kulinda Muungano kwa nguvu zote – Pemba. 22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa – Morogoro. 23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini. 24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa 25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo – Songea. 26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira – Mbeya. 27. Kuzuia hatari ya Kisiwa cha Pangani kuzama – Tanga. 28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini – Iringa. 29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same hadi Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi-Dar es Salaam-Same mkoani Kilimanjaro. 30. Kumaliza tatizo la maji katika Wilaya ya Same - Same mjini. 31. Kuboresha barabara za Igunga-Tabora. 32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu mkubwa wa walimu - Kisesa Magu. 33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya mjini. 34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) - Hydom Manyara. 35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa – Musoma. 36. Kulinda haki za walemavu – Makete. 37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami, urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini. 38. Kujenga barabara Musoma-Mto wa Mbu Arusha – Arusha. 39. Kuanzisha Jimbo la Ulyankulu- Shinyanga mjini. 40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma-Kaliua, Tabora 41. Kukarabati barabara ya Arusha-Moshi - Arusha mjini. 42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa hadi Singida – Dodoma. 43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 – Longido. 44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji – Shinyanga. 45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini. 46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma. 47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido – Longido. 48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro. 49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara. 50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini. 51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima mwaka 2010-2015 - Babati vijijini. 52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha – Iringa. 53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika – Iringa. 54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania – Iringa. 55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi –Ifunda. 56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, Mkoa wa Mara. 57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa. 58. Ahadi kuisaidia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii – Kibandamaiti, Mjini Zanzibar. 59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar 60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada – Kibandamaiti. 61. Serikali kujenga upya Bandari ya Mbamba Bay – Ruvuma. 62. Ununuzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 – Mbamba Bay, Ruvuma. 63. Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma. 64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma. 65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi - Dar es Salaam. 66. Mtwara kuwa mji wa viwanda – Mtwara. 67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu – Kibaha. 68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa – Kibaha. 69. Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda – Kibaha.
 
cuf jifunze utii na uvumilivu kwa mme wenu la sivyo hata kile kidogo mlichonacho kitatwaliwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom