Hongera Mchengerwa kuwa waziri TAMISEMI. Nakuomba yatazame haya, vibali vya uhamisho vina urasimu mkubwa

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
324
909
Mkuu mi Sina mashaka na utendaji wako kabla ya kuwa Waziri tangu ulipokuwa Ofisi ya mwana Sheria Mkuu wa serikali baadaye ukawa Waziri wa Utumishi kwakweli uliwafuta Watumishi machozi kwa wale walioganda daraja moja kwa miaka 6 walipata uhueni.

Siwezi kuyazungumzia mazuri yote uliyofanya Utumishi Ila Watumishi wenyewe wanajua kilichofanyika na jinsi ulivyowapa tumaini jipya.

Baadaye nyota ikang'ara ukahamishiwa wizara ya michezo na utamaduni ukaja na kauli mbiu ya kukarabati viwanja na kuhakikisha tunakuwa wenyeji wa afcon 2027 hilo halina ubishi Wala sitaki kuongeza neno kongole nyingi Sana.

Safari ikaendelea mbele ukaingia maliasili na Utalii kwanza kabisa Mambo ulikuta hayapo sawa ukarekebisha Mambo kibao maslahi, MAFUNZO, vitendea kazi na mshikamani kazini Leo ujangili umepungua Kama siyo kutokomea kabisa.

Mungu wa mbinguni anaona juhudi zako Sasa amekuleta OR-Tamisemi mojawapo ya wizara ngumu sana kwani nakumbuka kipindi Cha Hayati Magufuli aliwqhi kumuambia mhe. Jafo ugumu wa kazi ndani ya wizara hiyo kwani fedha zote za kutekeleza miradi muhimu Kama Elimu na Afya Nchini husimamiwa kwa ukaribu hapo.

Yote tisa kumi ningependa ufahamu magumu wanayopitia watumishi walioko chini ya OR-Tamisemi hususani kada za
1. Elimu
2. Afya
3. Watendaji wa Serikali za mitaa
Hawa wanapitia mateso makubwa hususani wale wa chini kwa Wakuu wa idara wao kugeuka Miungu Watu hususani Waalimu stahiki yao nimegeuzwa mitaji ya Wakuu wa idara mfano fedha za uhamisho wa ndani na hata wa nje, nauli ya likizo, kujikimu (imekua Kama hisani na siyo haki) na pale wanapokuwa na barua za maombi Kama vile kweñda masomoni kubadilishana vituo vya kazi na uhamisho wa kawaida.

Kwakua wewe ni muelewa nakuomba pitia mafaili hapo ofisini kwako inayohusu Vibali vya uhamisho wa Watumishi Mara ya mwisho kutolewa ni januari mwaka huu (yaani walioomba mwqka 2022) Sasa jiulize hii itasaidia kuleta morali ya utendaji serikalini?

Jibu ni hapana kumbuka wengine wanafata familia zao wwngine Wana matatizo makubwa ya afya lakini tangu mwqka huu uanze hakuna kibali kilichotoka yaani 2023 hakuna Mtumishi aliyepata kibali na Kama yupo anajua mwenyewe aliipataje lakini lile pdf la Wizara yako haijatoka kwa maombi ya 2023 japo wapo tunaoona wanahama.kwa haraka haraka ni kwamba Kuna Urasimu mkubwa katika uhamisho wa Watumishi Watu wanatozwa kati ya laki 5 hadi milioni moja na pointi kutegemea unapoomba kuhamia.

Mimi nimekufinya sikio sababu najua watakuzungusha kwenye miradiiii weeeee uku wao wakibaki maofisini kuendelea kukandamiza, hapa ninapokuandikia Kuna Mtumishi alifanyiwa operation ya mishipa ya Moyo JKCI juni 2022 kutoka jimboni kwako aliomba uhamisho tangu septemba 2022 barua yake alijibiwa februari 2023 wakati hadi Wakuu wa idara walimtembelea JKCI na kukiri kuwa kwa mazingira yale anastahili kuhama sababu atatumia vidonge maisha yake yote na kuhudhuria kliniki kila wiki.

Lakini Pamoja na Mtumishi huyo kujitahidi kuomba uhamisho hatimaye Aprili wali process uhamisho na kumuombea kibali TAMISEMI hadi leo anasubiri mkeka utoke lakini wapi na ana familia na kingine kibaya zaidi Kuna Watu alikua nao uko jimboni kwako juzi hapa wamehama lakini yeye Hadi l leo kibali chake hakijatoka Tamisemi naomba hili uliangalie Mkuu sambamba na fedha za nauli ya likizo, fedha za uhamisho na maombi ya kweñda masomoni.

Naomba aione Mhe Mohammed Omar Mchengerwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mbunge wa Jimbo la Rufiji.
 
Sawa, nimeyapokea. Nitayafanyia kazi

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Ajira hizi za ummah za chini ni manyanyaso tupu. Bora kujiajiri au kuiingia siasa za ccm na kupata uteuzi
Ni kweli Mtumishi wa chini Hana thamani Nchi hii kabisa lakini ndiyo watendaji Wakuu wa shughuli za Serikali na ndiyo wanaotafsiri sera na mipango ya Serikali kwa vitendo kwa Wananchi.
 
Back
Top Bottom