miaka ya 60 wakati tuna uhaba wa wasomi katika taifa letu darasa la saba walikuwa mameneja, maafisa, walimu n,k katika utendaji mbalimbali katika nchi yetuJana nimemsikia waziri wa mambo ya ndani akidai wameita waliofeli katika ajira za mambo ya ndani kwa kuwa wanahitaji watu wa kubeba bunduki mtaani.
ni wazi fikra za wizara hii haziendani na kasi ya ukuaji wa sekita ya elimu katika nchi yetu kwamba nchi yetu imeongeza shule nyingi sana na vyuo vingi sana na tunakoelekea hata boda boda, mama lishe, machinga watakuwa na shahada.
hatuwezi kufanya mabadiliko makubwa katika sekita ya elimu kwa kuhakikisha watu wengi zaidi wanapata fursa za kusoma na kufikia elimu ya juu na tukabaki na dhana za zamani kuwa wasomi wanatakiwa kuwa maafisa wanaokaa maofisini tu na huku fursa za kukaa ofisini kwa wasomi wetu hatuna na wasomi wanabaki nyumbani na tukiamini kazi fulani ni kwa watu wasiosoma.
swala la kupanda vyeo au kujiendeleza litaendana na nafasi zinazopo na siyo kigezo cha ufaulu tu na kujikuta jamii ina wasomi wasio na ajira huku upendeleo ukitolewa kwa wasiosoma.
kadiri tunavyopiga hatua katika sekita ya elimu ndivyo mazingira fulani yanavyobadirika na kutoa kipaumbele kwa wanaojituma katika sekita ya elimu.
miaka ilivyopita na tukatengeneza wasomi tukasema angalau kada ya chini ni kidato cha nne.
kwa sasa tumetengeneza vyuo vingi vya elimu ya juu, vyuo vingi vya elimu ya kati ni wakati sahihi wa kusema mwenyeshahada kazi iliyopo ni kubeba bunduki ukaenda kulinda benki au kukaa nyumbani na shahada yako na uchaguzi uwe ni wake.
ni wakati sasa wa kuwaambia hawa wenye shahada kazi zilizopo kwa wingi kuendana na wingi wenu ni kazi za chini na mchague kuzifanya ama kuziacha na siyo watu wanajitahidi kusoma na kuwacheka wasiosoma na wakifika juu mnawaambia wasiosoma ndiyo wenye weledi wa kazi.
mtu anamaliza chuo miaka mitano hana ajira, yuko kwa ndugu analishwa na kupewa nauli alafu unamwambia hawezi kuchukua bunduki na kulinda benki wakati hawezi hata kujilisha.
otherwise tupunguze intake za wanafunzi katika vyuo vya elimu za juu ili waendane na udogo wa nafasi za ajira za maafisa katika jamii yetu.