S.H Amon apoteza jengo la ghorofa nane Kariakoo

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,988
1,175
Mbunge wa zamani wa Rungwe, Sauli Henry Amon amepoteza jengo la ghorofa nane lililoko Kariakoo jijini hapa, baada ya Mahakama ya Rufani kueleza kuwa nyumba hiyo ilijengwa kwenye kiwanja kilichouzwa kwa mnada isivyo halali.

Uamuzi huo umeirejeshea furaha na kuipa utajiri wa ghafla familia ya Bushiri Pazi, iliyopambana kwa zaidi ya miaka 20 katika mahakama mbalimbali kupigania kile ilichoamini ilikuwa haki yake.

Jengo hilo ni nyumba namba 113, kitalu namba 4 block namba 17, lenye ghorofa nane lililopo Kariakoo, Wilaya ya Ilala.

Amon, aliyekuwa mbunge kupitia CCM mwaka 2015 -2020 anayejulikana zaidi kwa jina la biashara la S.H. Amon, anamiliki kampuni ya S.H. Amon Enterprises Co. Ltd yenye maduka ya vipodozi jijini Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha na Mbeya.

Amon aliinunua nyumba hiyo ya kawaida kwenye mnada Mei 13, 2001 kwa Sh105 milioni kupitia Kampuni ya S.H. Amon Enterprises Co. Ltd na kupewa hati namba 57275 iliyotolewa Machi 24, 2005, kwa jina la kampuni hiyo, kabla ya kuibomoa na kuporomosha ghorofa hilo.

Asili ya mgogoro

Awali kiwanja hicho kilikuwa na nyumba ya udongo ambayo iliuzwa baada ya familia ya watoto sita ya marehemu Pazi kupata fursa wakaingia ubia na mwekezaji (hakutajwa) aliyeivunja na kujenga nyumba nyingine ya kisasa kwa makubaliano ya kibiashara.

Mmoja wa wanafamilia katika nyumba ya udongo iliyovunjwa, Tatu Pazi, alikuwa anamiliki chumba kimoja alichompangisha mtu aliyetajwa kama Musa Hamisi Kazuba.

Lakini baada ya nyumba hiyo kujengwa upya, mahali ambapo palikuwa na chumba alipopanga Kazuba kwa ajili ya biashara pakageuka na kuwa njia.

Mgogoro ulianzia hapo baada ya Kazuba kung’ang’ania apewe eneo ambako chumba chake kilikuwa ili aendelee na biashara yake ya duka.Baada ya kukosekana maelewano, Kazuba alifungua shauri katika Baraza la ardhi la mkoa akidai Tatu amekiuka makubaliano.

Mdai alitaka baraza hilo liamuru arejeshewe kodi ya Sh1.8 milioni aliyokwishatoa pamoja na riba.

Kazuba pia, alitaka alipwe Sh900,000 kila mwezi kuanzia mwaka 1999 mpaka siku watakapokamilisha malipo hayo.

Baraza hilo lilimwamuru Tatu kumlipa mpangaji wake huyo riba ya Sh15 milioni zikiwa sehemu ya Sh1.8 milioni alizokuwa amelipa kodi ya pango baada ya kukubaliana na madai ya Kazuba.

Tatu hakukubaliana na uamuzi huo, aliamua kufungua shauri katika Baraza la ardhi la taifa. Hata hivyo, alishindwa baada ya Baraza hilo kuridhia uamuzi wa Baraza la mkoa.

Baada ya kuona amepata ushindi katika mabaraza yote, Kazuba alikwenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukazia utekelezaji wa hukumu.

Wakati Kazuba akifanya hayo, wanafamilia ambao hawakuwa sehemu ya mgogogo kati ya Tatu na Kazuba, ambao nao walikuwa wamiliki, waliibuka na kudai hawakuwa wakijua kilichokuwa kinaendelea mahakamani.

Walikwenda Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutambua uwepo wa mgogoro huo na kuweka mapingamizi kadhaa wakipigania haki yao.

Mnada kabla ya hukumu

Wakati mapingamizi hayo yako mahakamani, ushahidi unaonyesha kuwa madalali wa mahakama walianza kutangaza kupiga mnada nyumba hiyo siku kadhaa kabla hata ya uamuzi wa maombi ya Kazuba ya kutekeleza hukumu kuamuliwa.

Baadaye Mahakama ya Kisutu iliamuru nyumba hiyo ipigwe mnada na kutupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na wanafamilia wengine.

Hapo ndipo nyumba iliuzwa kwa S.H Amon ambaye aliibomoa na kujenga jengo jipya la ghorofa nane.

Kufuatia uamuzi huo, mwaka 2004 wanafamilia watano wa mzee Pazi walifungua kesi Mahakama Kuu (Divisheni ya Ardhi) kupinga nyumba yao kuuzwa.

Waliiomba Mahakama itamke kuwa wao ndio wamiliki halali wa kiwanja hicho na nyumba iliyokuwemo.

Waliitaka itamke pia kuwa amri ya wao kukamatwa, nyumba yao kuuzwa, wao kuondolewa na kubomolewa haikuwa halali na ilitokana na udanganyifu mkubwa.

Wagonga mwamba

Baada ya kusikiliza shauri lao hatimaye Machi 9, 2012 Jaji Kakusulo Sambo alitupilia mbali maombi hayo na kutamka kuwa S.H. Amon Enterprises Co. Ltd ndiye mmiliki halali wa jengo hilo na maendeleo yote yaliyokuwa yamefanyika.

Ilisema kuwa wadai hao hawakuwa na haki ya kuchukua mali ya mtu mwingine bila ridhaa yake.

Uamuzi huo haukuwakatisha tamaa. Kupitia wakili wao, Melchisdeck Lutema walikimbilia Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi huo mwaka 2019.

Waliokata rufaa hiyo ni Hamis Bushiri Pazi akiwa msimamizi wa mirathi na dada zake wawili, Stumai na Hatujuani pamoja na dada zake wengine wawili ambao ni marehemu, Neema na Mwajuma.

Wajibu rufani walikuwa ni S.H. Amon mwenyewe, S.H. Amon Enterprises Co. Ltd, Musa Hamisi Kazuba na Kassim Ally Omar kama msimamizi wa mirathi ya dada yake, Tatu ambaye pia ni marehemu.

Rufaa hiyo ilisikilizwa na jopo la majaji watatu, Mwanaisha Kwariko, Issa Maige na Abraham Mwampashi Aprili 13, mwaka huu.

Majaji hao walikubaliana na hoja za rufaa na kubatilisha umiliki wa eneo hilo pamoja na uwekezaji wote uliofanywa na S.H. Amon katika kiwanja hicho na kuimilikisha familia hiyo.

Majaji hao walisema ni jambo lisilobishaniwa kuwa eneo hilo na nyumba iliyokuwemo ilikuwa ikimilikiwa kwa ubia na wanafamilia sita, akiwamo mjibu rufaa wa nne (Tatu), akimiliki hisa moja kati ya saba (1/7).

Hivyo ikaona kuwa kuuzwa na kuhamishia umiliki wa nyumba hiyo kwa Kampuni ya S.H. Amon Enterprises Co. Ltd haikuwa halali na jambo lisilowezekana wakati kumbukumbu zinaonyesha S.H Amona alinunua nyumba hiyo akijua kuwa inamilikiwa na familia.

Wakaendelea kueleza kuwa kitendo cha kampuni hiyo kununua nyumba hiyo bila kutafuta na kufahamu kiwango cha umiliki wa mwanafamilia kumemfanya asiwe mnunuzi halali.

“Hii ni kwa sababu kwa mtu mwenye ufahamu katika mazingira ya kesi hii ingetegemewa kuwa kabla ya kununua mali hiyo, mjibu rufaa wa pili, S.H. Amon Enterprises alipaswa kwanza kuuliza katika mamlaka husika kuhusu kiwango cha umiliki wa (Tatu) mjibu rufani wa nne.

Mahakama hiyo imesema kwa kuwa uuzwaji wa nyumba hiyo haukuwa halali kwa upande wa wamiliki wengine waliokuwa wakimiliki hisa sita (6/7), inakubaliana na warufani kuwa Mahakama Kuu ilikosea kuamuru kuwa kampuni hiyo ilikuwa mmiliki halali na hasara inakuwa ya S.H. Amon.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili, Amon ameeleza kushangazwa na uamuzi wa kulimilikisha jengo lake katika familia ya Pazi bila kujali uwekezaji alioufanya.

Source : Gazeti la Mwananchi
 
Mjumbe hauwawi👇

Screenshot_20220428-170106.png


Screenshot_20220428-170207.png


Screenshot_20220428-170142.png
 
Mungu ni mwema sana.
Hivi ndivyo haki inavyokua haipotea, ingawa inaweza tu ikacheleweshwa.
Miaka kuanzia ya 2014 kurudi nyumba, wafanya biashara/wanasiasa walionekana kua wenye mguvu kuliko hata serikali, na hii ndio matokeo ya sheria zilizo pindishwa na wenye fedha/mamlaka enzi hizo
 
Miaka 20 mingi sana acha wafaidike,Hawa viongozi wengi wa CCM walikuwa waporaji wakiamini hawagusiki.
Miaka 20 mingi sana acha wafaidike,Hawa viongozi wengi wa CCM walikuwa waporaji wakiamini hawagusiki.
Haki huwa haipotei...

Picha tafadhali ya mjengo unaoenda badilika umiliki...
Haki huwa haipotei...

Picha tafadhali ya mjengo unaoenda badilika umiliki...
Haki huwa haipotei...

Picha tafadhali ya mjengo unaoenda badilika umiliki...
Mungu ni mwema sana.
Hivi ndivyo haki inavyokua haipotea, ingawa inaweza tu ikacheleweshwa.
Miaka kuanzia ya 2014 kurudi nyumba, wafanya biashara/wanasiasa walionekana kua wenye mguvu kuliko hata serikali, na hii ndio matokeo ya sheria zilizo pindishwa na wenye fedha/mamlaka enzi hizo

Haki huwa haipotei...

Picha tafadhali ya mjengo unaoenda badilika umiliki...

Wakuu habari. Hiyo hoja ya wanahisa 6/7 kutokushirikishwa katika uuzwaji imenipa darasa kubwa sana, hili inabidi iwe angalizo kwetu sote.
 
Kesi za Ardhi na Nyumba zimekuwa nyingi sana Kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba .
Na maamuzi huko ni Kizungumkuti wenye fedha wanapindisha sana sheria..

Hawa sijui Wenyeviti wa haya Mabaraza ni tatizo kubwa sana.

Pongezi kwa Mahakama ya rufaa kuirejeshea hii familia ya Pazi furaha..
 
Back
Top Bottom