Philip Basiimire: Nape alisema walipoondoa VAT kwenye vifaa vya digitali, bei za vifaa vya digitali havikushuka bei

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anashiriki akiwa Mgeni Rasmi kwenye Mkutano wa 'Future Ready Summit ambao ni tukio la kila Mwaka linalowakutanisha Wadau mbalimbali wa Teknolojia na Washirika wa Kimkakati ili kutafakari suluhisho katika kuchochea maendeleo ya Teknolojia.

Waziri Mkuu, ameongozana na mawaziri kadhaa akiwemo waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Habari, Nape Nnauye. Baada ya kufungua mkutano huu kutakuwa na majadiliano yatakayoendelea kujadili masuala mbalimbali ya kiteknolojia.


Waziri ameoneshwa masuala mbalimbali ya kiteknolojia, ikiwemo Code Like A Girl, mradi unawatengeneza wasichana kutengeneza program mbalimbali na kuongeza idadi ya wanawake katika teknolojia. Mradi wa Code like a girl unafadhiliwa na Vodacom.
Waziri Mkuu Future Ready Summit.jpg
Waziri Mkuu akiwa Ukumbini​

Baadhi ya vitu alivyoongea Sofie Maddens, Chief, AI Digital Knowledge Hub Department - ITU
"Ni muhimu kuwafanya watu wasio mtandaoni wawepo mtandaoni, na waliokuwa mtandaoni wapate kuunganisha vyema. Mabadiliko ya dunia ijayo yanatarajia wanaounganishwa mtandaoni kuwa salama."
20240215_103411.jpg

"Teknolojia inatengeneza ajira, tunahitaji kuhakikisha wasichana wanakuwa na ujuzi wa kutumia. Kuna kazi zitapotea na kuna kazi zitatokea kutokana na teknolojia inayoendelea kutanuka kama AI na automation.

Kuhusu watunga sheria na wadhibiti wa mtandao wapaswa kufikiria teknolojia kwa upana wake. Watunga sera na watunga sheria wanapaswa kuwa na mawasiliano ili kuja na suala jema kuhusu teknolojia.

Sio tu kwamba tunataka watu waunganike bali pia kuwe na tija kwenye muunganiko. Tunapaswa kuangalia namna mpya na bora ya kuziwezesha taasisi za mawasiliano. Ilipokuja MPesa hakukuwa na udhibiti mkubwa walikaa na kuongea hadi Benki Kuu za maeneo mbalimbali.

Tunahitaji kuwa kimkakati ili kukuza teknolojia kama huduma ya kijamii. Tunahitaji wanadhibiti kujifunza teknolojia tunawaita wadhibiti ila walipaswa kuwa ni wawezeshaji.

Kuna wakati sheria zinapaswa kubadilika lakini zinapaswa kuwa na uwazi wakati wa mabadiliko hayo. Watu wa taaluma, watunga sera na walaji wanapaswa kushirikiana ili kuunda mifumo ya kusimamia teknolojia na digitali."

Baadhi ya mambo aliyoyaongea Mkurugenzi wa Vodacom, Phillip Basiimire.

Akiwa kwenye panel discussion. Mkurugenzi wa Vodacom, Phillipi Bassiimire amezungumzia nia ya kushusha gharama ya vifaa vya digitali ili kupambana na mgawanyo wa kidigitali. Amezungumzia ushirikiano wa wadau mbalimbali ili kupambana na suala hilo.

Ametolea mfano kuwa aliwahi kutembelea ofisi ya waziri wa Mawasiliano Nape Nnauye, ambaye alimwambia serikali iliwahi kuondoa VAT kwenye vifaa vya kidigitali lakini bei za vifaa hazikushuka. Hivyo VAT zilirudishwa.

Aliyoyasema Nape.

Waziri wa Habari na Teknolojia Habari, Nape Nnauye amesema serikali ipo tayari kupokea mabadiliko ya nne ya viwanda ambayo ni mabadiliko ya kiteknolojia. Aidha amesema unafuu wa internet ni moja kati ya msingi ambao wizara unaitambua.

Ameyasema hayo akitoa neno la kumkaribisha Waziri Mkuu ambaye ni mgeni rasmi wa mkutano wa Fyture Ready Summit.

Aliyosema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
 
Back
Top Bottom