Barua ya Wazi kwa Dkt. Dorothy Gwajima na Nape Nnauye

SYLLOGIST!

JF-Expert Member
Dec 28, 2007
7,101
6,708
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Mhe.@ Dk Dorothy Gwajima

Na...

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari

Mhe. Nape Moses Nnauye.

Wasalaam,

Poleni kwa kazi.

Ninakuandikieni barua hii ili kuwajulisha na suala linaloleta wasiwasi mkubwa ambalo limejitokeza hivi karibuni kwenye Jukwaa la mtandaoni.

Kuna Daktari mmoja (sijui ni Daktari wa matibabu au Daktari wa Shahada) alitoa dai ambalo sio tu halina msingi wa kisayansi lakini pia inakera sana, akidai kwamba "mtu mweusi popote alipo si binadamu kamili." Ni very Offensive.

Matamshi kama hayo ni ukiukaji wa kanuni za usawa na utu ambazo jamii yetu inazithamini.

Kwa kuzingatia hilo, nakuombeni mzingarie athari za kauli hizo nabjukumu ambalo Wizara ya Ustawi wa Jamii na Wizara ya habari na teknolojia wanaweza kutekeleza katika kushughulikia masuala haya.

The Media Services Act, 2016 and the Electronic and Postal Communications(Online Content) Regulations, 2020 imetoa framework ambazo hatua zinaweza kuchukuliwa dhidi ya matamshi ya chuki na maudhui amabayo yanaweza kuchochea machafuko ya Umma.

Sheria hizi ni muhimu katika kudumisha jamii yenye heshima na usawa na kuhakikisha kwamba watu wote, bila kujali rangi, wanapewa heshima wanayostahili.

Mamlaka yaliyo chini ya wataalamu kamavile madaktari na mabalozi yanakuja na wajibu wa kuzingatia viwango vya maadili. Viwango hivi vinapokiukwa, ni muhimu kwamba hatua zinazofaa zichukuliwe, bila ya kujali their Individual status.

Waheshimiwa, mtakumbuka hivi karibuni tukio la Balozi wa Romania nchini kenya aliposema "the African group has joined us" alipomwona tumbili nje ya dirisha wakati wa mkutano katika jengo la Umoja wa Mataifa mjini Nairobi mnamo tarehe 26 Aprili, 2023.

Maneno yake hayana tofauti na ya Daktari huyu kwa tafsiri.

Balozi huyo alichukuliwa hatua za kurudishwa Romania.

Tukirudi kwenye suala la Dkt huyu wa mtandaoni, yeye amekuwa akitoa matamshi kama hayo karibu kila anapopata mwanya wa kufanya hivyo na hakuna hatua zezote zinazochukuliwa na wadhibiti wa maudhui ya majukwaa

Waheshimiwa, kama viongozi katika nyanja zenu husika, mna uwezo wa kushawishi mabadiliko na kukuza utamaduni wa 'Responsible speech" na uwajibikaji.

Ninawasihi, mchukue hatua madhubuti dhidi ya tabia kama hiyo ili kudumisha uadilifu wa taaluma na usalama wa nafasi zetu mtandaoni.

Ikiwa na pamoja na kuwasiliana na uongozi wa Jukwaa husika kuchukua hatua stahiki.

Ahsanteni kwa kutumia mda wenu, thanks for your attention to this critical issue. Nina imani kwamba mtachukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kwamba Forums and Professional spaces remain free from misinformation and discrimination.

Sincerely,

SYLLOGIST!
 
Jukwaa la mtandaoni.

Kuna Daktari mmoja(sijui ni Daktari wa matibabu au Daktari wa Shahada) alitoa dai ambalo sio tu halina msingi wa kisayansi lakini pia inakera sana, akidai kwamba "mtu mweusi popote alipo si binadamu kamili." Ni very Offensive.
Jukwaa gani? Emu kua muwazi
 
Kwa hio Dokta mwenyewe ndio wewe? Wewe ndio umesema Mwafrika popote alipo sio binadamu kamili?


Mimi huwa natazama positive katika negative , siwezi kuangalia MTU kasema nini Ila uwa naangalia kwanini kasema hivyo

MTU mmoja anaweza kufanyiwa ukatili na MTU mmoja mweusi basi chuki ikaanzia hapo inkuhitaji akili za ndani kuelewa hili jambo


Sio kila tatizo lipo Kama lilivyo.
 
Mimi huwa natazama positive katika negative , siwezi kuangalia MTU kasema nini Ila uwa naangalia kwanini kasema hivyo

MTU mmoja anaweza kufanyiwa ukatili na MTU mmoja mweusi basi chuki ikaanzia hapo inkuhitaji akili za ndani kuelewa hili jambo


Sio kila tatizo lipo Kama lilivyo.
Kwa hio ilikua ni katika majibizano ndio likakutoka?
 
Kuna Daktari mmoja(sijui ni Daktari wa matibabu au Daktari wa Shahada) alitoa dai ambalo sio tu halina msingi wa kisayansi lakini pia inakera sana, akidai kwamba "mtu mweusi popote alipo si binadamu kamili." Ni very Offensive.

Matamshi kama hayo ni ukiukaji wa kanuni za usawa na utu ambazo jamii yetu inazithamini.
Tufanye yetu yaonekane yawadhihirishie kuwa tupo kamili, yawezekana mambo wanayofanya baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa ndiyo yaliwasukuma kuandika hivyo.
 
Ni kweli watu weusi siyo binadam kamili ndo maana ni dependent kila kitu wanahitaji msaada
 
Mnapoteza muda na nguvu kupambana na vitu ambavyo havina maana huku mambo ya msingi mkiyaacha.
Ati. Vitu ambavyo havina maana.

Kwa mantiki hiyo hili suala halina maana?

Sasa unafanya nini hapa na hayo maguvu yote kwenye vitu unavyoona wewe kuwa havina maana. Nini hicho kinacho kubugudhi?

Kwamba halina msingi au halina maana?

Wewe umeshwahi kuleta jambo gani au mambo gani unayoyadai ni ya msingi hapa Jukwaani,Daktari?
 
Back
Top Bottom