Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 47,774
- 68,858
Marekani hata hakuna tume ya uchaguzi, Serikali za majimbo ndizo zinasimamia mchakato mzima wa kupiga na kuhesabu kura laki hakuna Katibu wa jimbo awe Republican au Democrat anayeiba kura za wapinzani wake. Ila voter suppression kwa sehemu inawalenga watu weusi!
Uingereza hakuna tume ya uchaguzi ya kusimamia upigaji na kuhesabu kura, hii kazi yote inafanywa na serikali za mitaa. Tume yao ya uchaguzi ni kwa ajili ya kuhakikisha mchakato na sheria za uchaguzi tu zimezingatiwa. Uchaguzi wao pia haujawahi kuwa na shida, hakuna wizi wa kura.
Ufaransa kura zinahesabiwa na watu wa kujitolea kisha serikali za mtaa zinathibitisha na kutangaza matokeo, kama huwezi kwenda kituoni kupiga kura unaweza kumtuma mtu akupelekee kura yako polisi. Uchaguzi wao hauna shida pia.
Makaburu wa Africa Kusini wakati wanawazuia watu weusi kupiga kura wao wenyewe walikuwa wanaheshimu uchaguzi wao na hawabiani kura!
Sisi Waafrika lazima tuna shida mahali, tuna sheria na miongozo chungu nzima ya uchaguzi ila chaguzi zetu zina matatizo makubwa na mara zote hakuna anayekubali kushindwa na wengine wanaishia katika kukataa uchaguzi, kufungua kesi, maandamano au kupigana vita za kuuana kabisa!