Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika ununuzi wa korosho, Bodi ya Mazao Mchanganyiko inafanya kwanza thamini na kujiridhisha kama korosho hizo zimezalishwa nchini, kuangalia ubora na kama aliyepeleka ndiye mkulima. Baada ya kujiridhisha, ndipo utaratibu wa malipo unafuata. Swahili Times on Twitter
Wanaposema kupwaya wamakusudia nini hao mkuu?Kuna uzi nimeukuta humu humu JF Greatthinker anauliza Kwanini Utawala wa Marais Waislam ndio Utawala wao hupwaya!?
Pia kabla ya kulipa tuhakiki Kama hilo shamba alilipata kihalali Au Kwa Njia Za kifisadi
Pia tujiridhishe anathamini juhudi Za Serikal katika Suala la Hilo la Korosho Au laa?
Tuhakiki jee hakushiri Kwenye Vurugu Za Gesi 2014?
Wanaposema kupwaya wamakusudia nini hao mkuu?
Korosho umegeuka pembe ža TEMBO,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika ununuzi wa korosho, Bodi ya Mazao Mchanganyiko inafanya kwanza thamini na kujiridhisha kama korosho hizo zimezalishwa nchini, kuangalia ubora na kama aliyepeleka ndiye mkulima. Baada ya kujiridhisha, ndipo utaratibu wa malipo unafuata.
Kifupi serikali haikujiandaa ilichukua maamuzi kwa pupa.Kulikuwa na haja gani ya serikali kujiingiza katika jambo ambalo hailiwezi?? Huenda sasa ndio wametambua madhara ya jambo hili walipolichukulia kisiasa. Huwezi kuchubguza ubora wa kitu huku tayari unakihifadhi wewe! Ndio kusema serikali ikisema ubora ulikuwa wa chini basi bei nayo itaanguka? Je mkulima ataruhusiwa kuchukua korosho yake kama atakataa bei mpya?
Wakulima walipwe pesa zao na polisi walinde mipaka kuzuia korosho ya nje isiingizwe nchini. Kama habari hii ni ya kweli - madhila ya jambo hili yametokea mapema kuliko wengi walivotarajia.