Waziri Mkuu Musalia Mudavadi aonya Wakenya kuvuka mipaka kushiriki siasa za nchi jirani

Waziri Mkuu Musalia Mudavadi aonya Wakenya kuvuka mipaka kushiriki siasa za nchi jirani

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Waziri Mkuu wa Baraza la Mawaziri, Musalia Mudavadi, amewataka Wakenya kuepuka kuvuka mipaka ya nchi kwa ajili ya kutafuta haki au kushiriki katika siasa za mataifa jirani, akionya kuwa uhuru wanaoufurahia nyumbani, hususan uhuru wa kujieleza, haupo kila mahali. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kenya Software AI Summit 2025 uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Moi, Shule ya Sheria mjini Eldoret, Mudavadi alisema kumekuwepo na ongezeko la Wakenya wanaosafiri kwenda nchi za karibu bila kuelewa mifumo ya kisheria na kikatiba inayotofautiana na ile ya Kenya.

Mudavadi pia aliwataka vijana kuwa waangalifu na mwenendo wao mtandaoni, akibainisha kuwa tabia za watumiaji wa mitandao ya kijamii sasa zinachunguzwa na serikali za kigeni kabla ya kupewa visa. “Sasa kuna mwelekeo mpya ambapo maombi ya visa yanahusisha ukaguzi wa mitandao ya kijamii. Wale wanaopatikana na maudhui hasi wanaweza kupoteza fursa za kusafiri au kufanya kazi nje ya nchi,” alisema. Alisisitiza umuhimu wa kutumia mitandao kwa njia chanya na yenye kujenga ili kuboresha taswira na kuongeza nafasi za mafanikio.

Kauli ya Mudavadi imekuja kufuatia matukio ya hivi karibuni ambapo Wakenya wamejikuta wakikumbwa na matatizo katika nchi jirani. Wiki iliyopita, Wakenya wawili, Bob Njagi na Nick Oyoo, waliripotiwa kukamatwa nchini Uganda baada ya kujiunga na kampeni za mgombea urais Bobi Wine. Wengine kadhaa walikamatwa nchini Tanzania wakati wa uchaguzi uliopita, wakieleza kukumbana na mazingira magumu wakati wa mahabusu. Mudavadi alisisitiza umuhimu wa kujua sheria za kikanda na kuepuka vitendo vinavyoweza kuwaweka Wakenya hatarini nje ya mipaka ya nchi

1762851395267.png
 
Back
Top Bottom