Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye kukutana na Waandishi wa Habari Desemba 04, 2019

Status
Not open for further replies.
Nadhani Sumaye anaota kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kupitia msajiri kama alivyo Lipumba jd41,
 
Kesho saa tano ni mbali, alale hata nyumbani kwa waandishi wa habari, arejee ccm akaunge mkono juhudi. Aongee chochote atakacho ndani ya cdm yeye Ni useless. Na kwenye haya cdm wapate somo hii kuokota mizoga huko ccm na kuipa nafasi ya uongozi ni jambo lisilokubalika.
Naona wanaandaa panga kumkata ng’ombe mkia!!
 
Ukitizama wachangiaji unashangaa na kujiuliza, "huyu hii comment kaitoa kichwani au makalioni? Unajikuta unacheka kwa hio njia ya pili"
 
Kesho saa tano ni mbali, alale hata nyumbani kwa waandishi wa habari, arejee ccm akaunge mkono juhudi. Aongee chochote atakacho ndani ya cdm yeye Ni useless. Na kwenye haya cdm wapate somo hii kuokota mizoga huko ccm na kuipa nafasi ya uongozi ni jambo lisilokubalika.
Kwani mkuu aliyeipokea hiyo mizoga ni nani? Si ni mbowe? Ifike mahali tufungue akili zetu tutambue upuuzi aliofanya mbowe chadema.

Msigwa, Lema n.k wote wana wadhfa wa kuongoza chama, kwanini yeye ang'ang'anie nafasi hiyo miaka yote.

Ona leo chama kimejaa mamluki, wengine akina Lowassa wamesharudi CCM, chama kwa miaka minne kilikosa hoja ya msingi kabisa ya ufisadi ambayo ndiyo iliijenga Chadema.
 
Chadema chademaaaa
Kwa nini hamstawishi democrasia?
Wananchi watatuelewaje na mfalme wetu Mbowe?
Tunazidi kuipa CCM nafasi ya ushindi kila mara.
Its very sad, wakaskazini kuumana wenyewe.
 
Hapo kwenye kujenga chama vizuri imenigusa.

Sikuwa mpenzi wa siasa maana niliamini kuwa ccm itatutawala milele, Slaa, Mbowe, Lissu, Zitto wakanifanya niipende siasa, kikubwa ni ujasiri wao.

Chadema ilicheza karata mbovu mno 2015, tulipuuza maneno ya Dkt Slaa na kumwita mnafiki ila leo nyuso zetu hatuna pa kuziweka kuhusu Lowassa.

Chama kilifungwa mdomo kabisa, tulibakiwa na mwaba mmoja tu,Tundu Lissu.

Na mimi mpaka sasa naamini mpinzani ni Lissu, natamani Chadema iongozwe na akina Lema, Msigwa, Lissu n.k

Mbowe alishateleza, anapaswa atumie hekima ya hali juu kuachia hiki kijiti kwa wale ambao wamekuwa na mchango mkubwa mno ktk kujenga chama.
 
Kukatwa kwa Mzee Sumaye kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, hakutokani na kwamba yeye ni mamluki kweli wa CCM, bali nia yake ya kutaka Kung'oa mzizi wa Mpingo, ndugu Mbowe. Itakumbukwa kuwa, kati ya watu waliokuwa wanatakwa kuweza kumrithi Mbowe kwenye nafasi ya uenyekiti wa chama, ni pamoja na Cecil Mwambe na Mh. Heche. Na wote hawa wamegaragazwa kwenye uchaguzi wa kanda. Hawajakatwa kwa sababu ya historia au muunganiko wao na chama cha Mapinduzi bali nia yao iliyoonekana tishio kwa mr. Chair na watu wake.

Ndio maana, Mh. Lazaro Nyalandu( Kiongozi mwandamizi wa CCM kuhamia Chadema), pamoja na ugeni wake kwenye chama, ameachwa apite, hii ni kwa sababu hakutishia usalama wa nafasi za watu( Mbowe). Hakuna aliyejaribu kumpinga Mbowe akabaki salama, alianza mzee Wangwe, akaja Mh. Zitto 2009 na 2014. Sasa, mara hii yaweza kuwa Zamu ya Sumaye, Mwambe na Heche.
 
Magufuli mwana wa Africa anakubalika kila kona
Hana tofauti na Mwana wa jalalani...
tapatalk_1575203964871.jpeg
 
Mwache arudi zake ccm kwao, mara ii hatufanyi makosa tena hawa ndumila kuwili huwa wanatumwa kuvuruga upinzani sasa watagonga mwamba Lowasa ndo ametuamsha.

Tulimnyima makusudi ile nafasi alikusudia kuja kutuvuruga 2020 kama anaipenda chadema abaki
Mwanachama wa kawaida tu sasa tunataka watu wasionunulika Tundu Antipas Lissu, Mbowe, Msigwa, Maalim seif wanatosha hawa ni dhamana ata jahazi ikipasuka kwa mbele hawa tunawakubali wataogelea tu waje zao juu ata kama wimbi ni babkubwa na kiza kinene hawa hawana bei.,
 
Ukisikia kuna ujinga, basi ni kama huu uliouandika.

Mtuhujui atakalosema, pengine atawaumbua wanaosema kachezewa rafu na team Mbowe, au pengine ataunga mkono uamuzi wa wapiga kura ama juhudi za chadema. Lakini wewe ushaanza kuntukana na kujiropokea.

Jamani huko ufipa katiba yenu kuna kipengele kinachosema nafasi ya mbowe ni haramu kuguswa na mtu yoyote. Fanyeni uamuzi mmoja, mbowe awe kiongozi wa daima, hakuna uchaguzi kama alivyofanya BOKASA
Kesho saa tano ni mbali, alale hata nyumbani kwa waandishi wa habari, arejee ccm akaunge mkono juhudi. Aongee chochote atakacho ndani ya cdm yeye Ni useless. Na kwenye haya cdm wapate somo hii kuokota mizoga huko ccm na kuipa nafasi ya uongozi ni jambo lisilokubalika.
 
Waambie hao wanaCDM wanaojiropokea, wanaekewa mpira golini kwao na wanajifunga magoli bila kujijua.
Ni kweli kuwa kesho atahutubia ila pamoja na mambo mengine atawakemea waandishi makanjanja waliomlisha maneno. Kama CCM mnatarajia kuwa atakuwa upande wenu basi nawashauri msihudhurie hiyo press
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom