Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye kukutana na Waandishi wa Habari Desemba 04, 2019

Status
Not open for further replies.
Sumaye aliishasema, hatorudi ccm ng'o hata wafanyeje.

Mna wasi wasi gani, tulieni na subirini hiyo kesho.
 
Kesho saa tano ni mbali, alale hata nyumbani kwa waandishi wa habari, arejee ccm akaunge mkono juhudi. Aongee chochote atakacho ndani ya cdm yeye Ni useless. Na kwenye haya cdm wapate somo hii kuokota mizoga huko ccm na kuipa nafasi ya uongozi ni jambo lisilokubalika.
Du, labda mawazo yangu yameharibika sana siku hizi.

Hivi yeyote aliyeko huko CCM sasa hivi anapendezwa na yanayofanyika huko?

Na kama hapendezwi, na akaamua aondoke, hatakiwi kamwe ajiunge katika chama chochote cha siasa anachoona kuwa kinakaribia na anayoyakubali katika siasa zake?

Hapa naomba nitofautishe.

Simtetei Sumaye, na wala sijui kama hapendezwi na yanayofanyika CCM ndio maana katoka huko, au katoka kwa sababu zake binafsi zisizohusiana kabisa na msimamo wake katika anayoyaamini katika siasa. Amedumu CHADEMA sasa kwa muda wa kutosha kwa wanachama wenzake na viongozi kupima dhamira yake ndani ya chama chao. Kama hatoshi watakuwa wanalijua hilo wao vizuri zaidi ya wengine wote tuliopo nje ya chama.

Hata anachokwenda kuongea na hao waandishi hatukijui, lakini tayari tumekwishahitimisha haya, kwa nini tusiwe na subira hadi hiyo kesho!

Lakini kuchukulia mfano huu mmoja na kuwapaka rangi hiyo hiyo, woote walioko CCM sioni kwamba ni jambo la busara.

Kila mtu, awe anatokea CCM au kwingineko, apewe nafasi ndani ya chama na apimwe kama kuwepo ndani ya chama kuna manufaa na akitaka kuwania uongozi, sifa zake zichambuliwe.

Hili haliwezi kuwa swala la hukumu ya jumla jumla namna hii.
 
Kesho saa tano ni mbali, alale hata nyumbani kwa waandishi wa habari, arejee ccm akaunge mkono juhudi. Aongee chochote atakacho ndani ya cdm yeye Ni useless. Na kwenye haya cdm wapate somo hii kuokota mizoga huko ccm na kuipa nafasi ya uongozi ni jambo lisilokubalika.
Mbona kama umepanic au unajua anachoenda kuongea kesho mkuu? Relax relax
 
Acha jaji Mutungi, hata Magufuli anaruhusiwa kufuatilia ila cdm hamna kupita bila kupingwa. Na huyo jaji Mutungi akiona mkulu hafurahi akifute cdm ili mkulu afurahi zaidi. Sumaye arejee tu ccm, huko cdm anapoteza muda wake bure. Arudi ccm akateuliwe kwenye bodi za taasisi za umma.
Ndo girls za wana ccm alishafika hadi PM unadhani bodi gani inamfaa
 
Baada ya kukatwa katika uchaguzi wa ndani ya chadema na kuona dalili kwamba hawezi mshinda Mbowe kuwania uenyekiti wa chama, Sumaye aamua kurudi kundini rasmi

vyanzo vya watu wa karibu na waziri mkuu mstafu vinasema teyari Sumaye amekwishaamua kurejea CCM, akina polepole wamekubali kumpokea ili kuua upinzani hapa nchini
 
Safi sana.......Safari hii hainaga Ushemeji by F T Sumaye!
Anarudi analia eeh........
FB_IMG_1575424751050.jpeg
 
Baada ya mwaka nyalandu nae anarudi ccm.sijaelewa chadema huwa hawajifunzi kutoka kwa lowassa kuwatosa kila mwana chama wa ccm aliyekuwa na cheo serikalini akija chadema wanampokea nakumpa uongozi hawa hawamiiniki
 
Wewe huna hoja nimeamua nikupuuze rasmi sasa
Kweli sina hoja za umalaya wa kusifu na kuabudu mgonjwa. Najua ni Mungu pekee muumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana ndiye anastahili kusifiwa na kuabudiwa.
 
Self filtration for all debrils, CDM going to stabalize... Mbowe, its the time to compromise with ZZK and Mzee Maalim to have strong opposition than all the time...
Kuna wigo mpana wa mawazo ya kisiasa siyo vizuri kuyarundika kwenye kapu moja kwa sababu ya maslahi ya kupambana na CCM.
Mawaxo mbadala lazima yapewe nafasi
 
Kalamu1, Waliompora mashamba yake wanajulikana. Arudi huko huko wakamrejeshee mali zake.
Hana tofauti na yule mwingine aliyenyweshwa sumu alipoamua kurudi nyumbani alikonywea wakamtapishe au akawafie.
 
Sumaye na Lowassa walijiunga na CDM kuvuruga tu. Awe anaendelea ama kujitetenga na CDM haina madhara. Kiukwel kutoka cku nimeckia CDM wamewapokea hawa wazee wawili na kuwapa nafasi nyeti kabla ya kuwachunguza vizuri, nilipoteza imani kabisa na CDM.
 
Hang'ang'anii nyie ndio mnaye mng'ang'aniza kutokana na mafanikio yake ya kuwakabili.
Sasa anaingia kwenye awamu ya mapambano ya kiharakati ya kujibu mapigo kama wana wa CHADEMA wanavyotaka.
Kwani mkuu aliyeipokea hiyo mizoga ni nani? Si ni mbowe? Ifike mahali tufungue akili zetu tutambue upuuzi aliofanya mbowe chadema.

Msigwa, Lema n.k wote wana wadhfa wa kuongoza chama, kwanini yeye ang'ang'anie nafasi hiyo miaka yote.

Ona leo chama kimejaa mamluki, wengine akina Lowassa wamesharudi CCM, chama kwa miaka minne kilikosa hoja ya msingi kabisa ya ufisadi ambayo ndiyo iliijenga Chadema.
 
Hawa wazee wawili walikua na kiu ya madaraka tu. Hakuna walichosaidia
 
Tusikimnilie kulaumu bila ya kujua ataongea nini. Tujadili baada ya kusiiia atakachoongea.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom