Mkuu, hoja ya Madam SSH kumwondoa seating PM kufuatia yeye kula kiapo ingewezekana au pia ilitakiwa iwe kama ilivyotokea.
Kwanza, katiba haijaweza utaratibu ikitokea VP amerithi Urais kufuatia Rais kuijiuzulu au kufariki. Katiba iko wazi tu, VP atakula kiapo kuwa CinC kufuatia kifo kama ilivyotokea.
Bila shaka SSH alikuwa na imani na seating PM na hakuona haja kumwondoa ili apeleke upya jina lake bungeni kwa kuzingatia PM ndie alikua msimamizi mkuu wa msiba.
Kingine, Rais alikuwa bado na majonzi ya msiba na bila shaka akaamua kuendelea na mawaziri wote mwanzoni ila akaamua tu kuwabadilisha na kuongeza wengine kundini.
Miezi hii iliyopita umetengeneza "national healing from mourning" na mpaka watu wamesahau "yaliyopita" na wameanza kujipanga. Bila shaka pia kwa madam SSH kuwa na access na taarifa zote za kiusalama na kumjua nani ni nani anafanya nini, anakutana na nani, ana "mitikasi" gani, sio mbaya kuja na baraza jipya.
Mzee Ruksa mwaka tisini mwezi march, aliwataka mawaziri wote wajiuzuru akiwomo aliekuwa PM na Makamu wa kwanza wa Rais Joseph Sinde Warioba. Then akamrejesha tena kama PM na wakauda serikali.
Hata sasa madam anaweza kuwataka cabinet members wote wawasilishe barua mezani za kujiuzuru akiwamo PM, then akaja na jina la kupeleke mjengoni kama ili apitishwe kuwe PM na akamuapisha then wakasuka cabinet. Na kuwa kuwa PM wa sasa ni mbunge wa jimbo, ana nafasi ya kuteuliwa tena au akakalia bench kama mzee Msuya, Mzee John Malecela, Mzee EL; wote hawa walipoteza waliwahi kukaa bench bungeni.
Tumtakie heri madam SSH kwenye maamuzi atakayofanya; hii homa ya uchaguzi wa 2025 isifanya lengo la kuwatumikia wananchi likapotea.
Maombi yetu kwa Mungu asaidie tupate viongozi ambao hawako driven na next election, Mungu saidia tupate viongozi wenye shauku na kuwa driven na nini tufanye leo kwa Watanzania ambacho kina-serve purpose kwa kizazi cha leo na vizazi vijavyo.