Waziri Mkuu Majaliwa huu ni mwezi wa nane SGR kipande cha Dar-Moro kinaanza kazi lini?

Tume na misafara ya viongozi hesabu yake iko juu kuliko hasara ya tukio.
Kuhusu vichwa vya tren walisema Corona imezuia wataalam kujua kupima huku.
 
Hakuna hela Mkuu na hii susia susia ya huduma mbali mbali nchini na kutoomba risiti ukinunua kitu ili kuathiri mapato ya Serikali ikipamba moto basi hii Serikali haramu itakuwa na wakati mgumu sana kulipa hata mishahara.
Watoa risiti nao wamegoma kutoa hizo risiti. Hakuna Headmaster, Discipline master, Kiranja wala Monitor sasa hivi.

Tuko busy kukusanya misaada, kuzurula nje. Sijui uchumi umefika wapi?
 
Mkuu wacha uongo, wewe si ulisema itachukua miaka 40 kukamilika? Njoo November 2020 uone majaribio Moro - Pugu. Dar bakini na ujanja wenu. JPM alimudu zote hizo sasa wameingia watoto wa watumwa kufuja pesa zilizokusanywa na wenye uchungu wa nchi hii.

..Mwalimu Nyerere alijenga reli ya Tazara na ilimalizika ndani ya miaka mitano, toka Dar Es Salaam mpaka Kapirimposhi-Zambia.

..kwanini Magufuli na Samia wameshindwa kumaliza kipande cha Dar mpaka Morogoro kwa wakati, tunaelekea mwaka wa tano sasa?

..Na kama Dar mpaka Morogoro inachukua muda mrefu namna hii, reli itafika lini Mwanza na Kigoma?

..Ucheleweshaji huu unatokana na nini? Tatizo liko kwa mkandarasi, au serikali?
 
..Mwalimu Nyerere alijenga reli ya Tazara na ilimalizika ndani ya miaka mitano, toka Dar Es Salaam mpaka Kapirimposhi-Zambia.

..kwanini Magufuli na Samia wameshindwa kumaliza kipande cha Dar mpaka Morogoro kwa tunaelekea mwaka wa tano sasa?

..Na kama Dar mpaka Morogoro inachukua muda mrefu namna hii, reli itafika lini Mwanza na Kigoma?

Uwezo huo hawana, ndio maana wanazuia watu kuongea maana wanajua huu udhaifu utaanza kuongelea wazi wazi. Kuna mazingira makubwa hiyo reli isikamilike, na sehemu itakayofanikiwa kukamilika na hiyo treni kuanza kazi, itaendeshwa kwa kiwango duni sana. Kwa maneno marahisi nchi imeingizwa kwenye deni kubwa ili kusaka sifa za kisiasa.
 
Kama uzi huu Safari za Treni ya Mwendokasi kuanza Agosti mwaka huu, 2021 unavyojionyesha, Waziri Mkuu alisema mwezi huu wa nane SGR kipande cha Dar-Moro kitaanza kazi. Je ni tarehe ngapi treni hiyo itaanza kazi? Badala ya serikali kujifichia kwenye kesi za kubambikiziana, watuonyeshe wanavyotekeleza ahadi za maendeleo.

Tunajua waziri Mkuu huna tabia ya kusema ukweli, mfano ulisema ww na IGP utatoa ripoti ya mtu aliyejiunganishia bomba la mafuta hapa mjini, lakini mpaka leo uko kimya! Ajali ya moto wa soko la kariakoo nayo ukaahidi utatoa ripoti ndani ya siku 7, tena baada ya kuunda kamati. Lakini inaonekana hela zimeliwa na hiyo kamati yako, na uko kimya! Ulifanya hivyo hivyo kwenye ajali ya moto wa lorry la mafuta huko Morogoro. Sasa tuambie SGR inaanza kazi tarehe ngapi mwezi huu?
Mnaulizia SGR ya nini, ya kazi gani, kivipi. Si Magu mlimwambia hamtaki maendeleo ya vitu bali demokrasia na uhuru wa kujieleza. Sasa ni kwamba mtatumia demokrasia na uhuru kwenda na kurudi Morogoro
 
Hakuna hela Mkuu na hii susia susia ya huduma mbali mbali nchini na kutoomba risiti ukinunua kitu ili kuathiri mapato ya Serikali ikipamba moto basi hii Serikali haramu itakuwa na wakati mgumu sana kulipa hata mishahara.
Na hiyo ndio njia sahihi ya kuwa pararazy kabisa. Tokea mwezi jana nimeacha kutumia pesa ndugu zangu kwa mitandao kule kwetu. Yuko mfanya biashara ambaye naye ni swahiba wangu, tumekubaliana na deposit pesa nitakayo NMB acct yake namtumia slip na kumwambia hizo mpe shangazi au mjomba. Mchezo umeisha, tozo wakatozane Lumumba
 
Mkuu wacha uongo, wewe si ulisema itachukua miaka 40 kukamilika? Njoo November 2020 uone majaribio Moro - Pugu. Dar bakini na ujanja wenu. JPM alimudu zote hizo sasa wameingia watoto wa watumwa kufuja pesa zilizokusanywa na wenye uchungu wa nchi hii.

Mhandisi mbobezi wa TRC alisema walau si chini ya miaka 15 kama wakijitahidi bila changamoto kujitokeza watamaliza network ya SGR nzima ( vipande vyote) toka Dar es Salaam mpaka Mwanza. Kwa hali inavyokwenda ni dhahiri mhandisi alikuwa sahihi inaweza badala ya kuchukua miaka 15 ikawa zaidi:

Soma rejea hapa : Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

Kutoka maktaba :

February 5, 2020
Kilosa, Tanzania

Wahandisi : Reli ya kati ihamishwe toka eneo la mafuriko na pia SGR kuchukua miaka 15 kukamilisha

Wakati wa ukaguzi wa uharibifu wa njia ya reli ya kati sehemu za Gulwe na Kilosa, wataalamu wa ujenzi wa reli wamebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuitumia reli ya mkoloni kwa miaka zaidi ya 10 ijayo.

Pia Reli mpya ya SGR itachukua takriban miaka 15 kumalizwa kujengwa hilo limebainishwa ktk eneo la reli ya kati lililokumbwa na mafuriko yasiyo ya kawaida wakati jopo la wahandisi na mkurugenzi mkuu walipokuwa wanajadili athari za mafuriko na changamoto za reli ya mkoloni na reli mpya ya SGR.

TRC inapoteza zaidi ya milioni 100 kwa siku kutokana na kusitisha safari reli ya kati. Na ili kukabiliana na mafuriko inabidi reli ya kati ihamishiwe mlimani na mlima huo unahitaji kuchongwa pia .

Uharibifu ktk eneo la mto Mkondoa ni mkubwa sana na ingawa eneo hilo la Gulwe Kilosa hakuna mvua lakini mvua kubwa zinazonyesha mikoa ya Iringa na Dodoma inaingiza kiasi kikubwa cha maji mto Mkondoa.

Source: TRC Reli TV
The 1,224 km long SGR RAILWAY line construction in Tanzania
Yapı Merkezi is constructing the fastest railway in East Africa. The first phase of the 1,224 km total line, the 202 km long Dar Es Salaam - Morogoro Railway Project, is the most critical part of the project. When the 5-part line is completed, it will connect Uganda, Rwanda, Democratic Republic of Congo and Tanzania, and provide access to the Indian Ocean for all related countries.

The groundbreaking ceremony took place on on April 12, 2017 at Pugu with the participation of HE Dr. John Pombe Joseph Magufuli as President and Commander in Chief of the Armed Forces of the United Republic of Tanzania, Hon. Prof. Makame Mbarawa as Minister of Works, Transport and Communication, Mr. Yunus Belet as acting Ambassador of Republic of Turkey in Dar Es Salaam, Mr. Erdem Arıoğlu as Vice Chairman of Yapı Merkezi, Mr. Özge Arıoğlu as CEO of Yapı Merkezi, Mr. Emre Aykar as Yapı Merkezi Board Member and , Mr. Abdullah Kılıç as Yapı Merkezi East Africa Regional Manager.

All works pertaining to design, manufacture, assembly and operation startup of track superstructure, electrification, signaling, telecommunication, central control systems are being carried out by Yapı Merkezi.

202 km-long single line will be constructed at a design speed of 160 km / h between Dar Es Salaam and Morogoro. During the 30-month project, a total of 33 million cubic meters of excavation work will be undertaken; 96 pieces of 6,500 meter-long bridge and overpasses, 460 culverts, 6 stations and repair and maintenance workshops will be constructed.
Yapı Merkezi İnşaat ve Sanayi A.Ş.
 
Ikifanikiwa hii Mkuu basi hii Serikali haramu lazima ipige magoti.
Na hiyo ndio njia sahihi ya kuwa pararazy kabisa. Tokea mwezi jana nimeacha kutumia pesa ndugu zangu kwa mitandao kule kwetu. Yuko mfanya biashara ambaye naye ni swahiba wangu, tumekubaliana na deposit pesa nitakayo NMB acct yake namtumia slip na kumwambia hizo mpe shangazi au mjomba. Mchezo umeisha, tozo wakatozane Lumumba
 
Hakuna hela Mkuu na hii susia susia ya huduma mbali mbali nchini na kutoomba risiti ukinunua kitu ili kuathiri mapato ya Serikali ikipamba moto basi hii Serikali haramu itakuwa na wakati mgumu sana kulipa hata mishahara.

Hizi ndizo changamoto ambazo wanaLumumba hawataki kuzitambua kuwa zipo na kuwa miradi ya Magufuli itawatoa jasho sana kujaribu kuikamilisha yote kwa wakati mmoja.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mnaulizia SGR ya nini, ya kazi gani, kivipi. Si Magu mlimwambia hamtaki maendeleo ya vitu bali demokrasia na uhuru wa kujieleza. Sasa ni kwamba mtatumia demokrasia na uhuru kwenda na kurudi Morogoro

..kwanini CCM hamuihoji serikali yenu?

..kwanini sgr Dar to Moro haijaisha mpaka leo wakati tuliahidiwa itachukua miezi 18?

..wapinzani wanahoji kwasababu fedha za MKOPO zinazotumika kujenga sgr zitalipwa na Watz wote bila kujali vyama vyao.
 
A concern citizens wewe kweli unauchungu na hii nchi..kuliko vijana wa hovyo wanaobishana trend za youtube.

#MaendeleoHayanaChama
 
Reli ya SGR Ni usanii wa mwendazake TABOA haitaruhusu huo mradi uanze kazi.
Kwani walio ua reli ya TANGA si bado wako wanakula Bata.
 
Kama uzi huu Safari za Treni ya Mwendokasi kuanza Agosti mwaka huu, 2021 unavyojionyesha, Waziri Mkuu alisema mwezi huu wa nane SGR kipande cha Dar-Moro kitaanza kazi. Je ni tarehe ngapi treni hiyo itaanza kazi? Badala ya serikali kujifichia kwenye kesi za kubambikiziana, watuonyeshe wanavyotekeleza ahadi za maendeleo.

Tunajua waziri Mkuu huna tabia ya kusema ukweli, mfano ulisema ww na IGP utatoa ripoti ya mtu aliyejiunganishia bomba la mafuta hapa mjini, lakini mpaka leo uko kimya! Ajali ya moto wa soko la kariakoo nayo ukaahidi utatoa ripoti ndani ya siku 7, tena baada ya kuunda kamati. Lakini inaonekana hela zimeliwa na hiyo kamati yako, na uko kimya! Ulifanya hivyo hivyo kwenye ajali ya moto wa lorry la mafuta huko Morogoro. Sasa tuambie SGR inaanza kazi tarehe ngapi mwezi huu?
Tanzania Railways Corp waje watujibu hivi hii ofisi si alikwepogo Ben Mwanantala yupo wapi
 
Mbaya zaidi wako 'wajinga" ndani ya Nchi hii wanadai eti MAJALIWA (PM) anasifa za kuwa rais.

Narudia tena ni wajinga hao kwani Waziri Mkuu MAJALIWA ni Muongo na hafai hata kwenye hii Nafasi alonayo !
 
..kwanini CCM hamuihoji serikali yenu?

..kwanini sgr Dar to Moro haijaisha mpaka leo wakati tuliahidiwa itachukua miezi 18?

..wapinzani wanahoji kwasababu fedha za MKOPO zinazotumika kujenga sgr zitalipwa na Watz wote bila kujali vyama vyao.
Hapana...tuimarishe demokrasia kwanza. Libya walikuwa na kila kitu ila tu Gadaffi aliwanyima demokrasia wakamtoa. Nasi tunataka demokrasia tu, SGR na Stigla na madaraja ni maendeleo ya vitu yanaweza kusubiri vizazi vijavyo watajenga
 
..hoja yako kuhusu Gaddafi ni ya kweli.

..vilevile demokrasia na maendeleo ni mambo ambayo yanaweza kwenda kwa pamoja.
 
Kama uzi huu Safari za Treni ya Mwendokasi kuanza Agosti mwaka huu, 2021 unavyojionyesha, Waziri Mkuu alisema mwezi huu wa nane SGR kipande cha Dar-Moro kitaanza kazi. Je ni tarehe ngapi treni hiyo itaanza kazi? Badala ya serikali kujifichia kwenye kesi za kubambikiziana, watuonyeshe wanavyotekeleza ahadi za maendeleo.

Tunajua waziri Mkuu huna tabia ya kusema ukweli, mfano ulisema ww na IGP utatoa ripoti ya mtu aliyejiunganishia bomba la mafuta hapa mjini, lakini mpaka leo uko kimya! Ajali ya moto wa soko la kariakoo nayo ukaahidi utatoa ripoti ndani ya siku 7, tena baada ya kuunda kamati. Lakini inaonekana hela zimeliwa na hiyo kamati yako, na uko kimya! Ulifanya hivyo hivyo kwenye ajali ya moto wa lorry la mafuta huko Morogoro. Sasa tuambie SGR inaanza kazi tarehe ngapi mwezi huu?
Huwa natofautiana na wewe kwenye masuala mengi. Ila huli la Sgr umehoji suala la msingi. Umekosea kuongelea habari za kubambikiziana kesi.
 
Back
Top Bottom