Waziri Mkuu Majaliwa huu ni mwezi wa nane SGR kipande cha Dar-Moro kinaanza kazi lini?

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
58,651
102,679
Kama uzi huu Safari za Treni ya Mwendokasi kuanza Agosti mwaka huu, 2021 unavyojionyesha, Waziri Mkuu alisema mwezi huu wa nane SGR kipande cha Dar-Moro kitaanza kazi. Je ni tarehe ngapi treni hiyo itaanza kazi? Badala ya serikali kujifichia kwenye kesi za kubambikiziana, watuonyeshe wanavyotekeleza ahadi za maendeleo.

Tunajua waziri Mkuu huna tabia ya kusema ukweli, mfano ulisema ww na IGP utatoa ripoti ya mtu aliyejiunganishia bomba la mafuta hapa mjini, lakini mpaka leo uko kimya! Ajali ya moto wa soko la kariakoo nayo ukaahidi utatoa ripoti ndani ya siku 7, tena baada ya kuunda kamati. Lakini inaonekana hela zimeliwa na hiyo kamati yako, na uko kimya! Ulifanya hivyo hivyo kwenye ajali ya moto wa lorry la mafuta huko Morogoro. Sasa tuambie SGR inaanza kazi tarehe ngapi mwezi huu?
 
Majaliwa naye kilaza tu, ni muongomunkgo fulani.Walisema treni imekamilika wakati dar hata daraja la juu bado.Wanasiasa ni waongo waongo

Tunataka wananchi waone kwa usahihi tunaongozwa na serikali ya aina gani. Wamegundua hawana uwezo wa kutekeleza ahadi zao, sasa wanajifichia kwenye siasa chafu za ugaidi wa kutunga. Mambo haya ndio yanatusukuma kutaka katiba mpya itakayoiwajibisha serikali.
 
Mkuu usisahau huyu huyu Waziri Mkuu Majaliwa aliutangazi ulimwengu kuwa hiyo treni ya sgr ingeanza kutoa huduma Nov. 2019.

Inaonekana uongo upo ndani ya DNA yake
 
Hii reli nadhani hadi mwisho wa huu mwaka maana kipande cha pugu Posta bado hakijakamilika.

Basi waziri Mkuu ajitokeze hadharani atangaze kwamba haitaanza kazi mwezi huu tena. Hapo itatusaidia kuuona serikali yetu inasema ukweli kwa kiasi gani.
 
Mkui usisahau huyu huyu PM Majaliwa aliutangazi ulimwengu kuwa hiyo treni ya sgr ingeanza kutoa huduma Nov. 2019.

Inaonekana uongo upo ndani ya DNA yake

Kabisa, mpaka yale mambo marahisi ya ajali kadhaa za moto alikuwa anatoa siku 7 atatoa ripoti huku akikaa kimya. Inaonekana yeye ni muongo wa hali ya juu. Kwa maneno marahisi hii ni serikali ya waongo.
 
Kama uzi unavyojionyesha, Waziri Mkuu alisema mwezi huu wa nane SGR kipande cha Dar-Moro kitaanza kazi. Je ni tarehe ngapi treni hiyo itaanza kazi? Badala ya serikali kujifichia kwenye kesi za kubambikiziana, watuonyeshe wanavyotekeleza ahadi za maendeleo.

Tunajua waziri Mkuu huna tabia ya kusema ukweli, mfano ulisema ww na IGP utatoa ripoti ya mtu aliyejiunganishia bomba la mafuta hapa mjini, lakini mpaka leo uko kimya! Ajali ya moto wa soko la kariakoo nayo ukaahidi utatoa ripoti ndani ya siku 7, tena baada ya kuunda kamati. Lakini inaonekana hela zimeliwa na hiyo kamati yako, na uko kimya! Ulifanya hivyo hivyo kwenye ajali ya moto wa lorry la mafuta huko Morogoro. Sasa tuambie SGR inaanza kazi tarehe ngapi mwezi huu?
Haitambui serkali ila manataka SGR mmerogwa nyie

USSR
 
Hakuna hela Mkuu na hii susia susia ya huduma mbali mbali nchini na kutoomba risiti ukinunua kitu ili kuathiri mapato ya Serikali ikipamba moto basi hii Serikali haramu itakuwa na wakati mgumu sana kulipa hata mishahara.
Kabisa, ndio maana wameanzisha tozo kandamizi ili kupata pesa za kulipa mishahara. Cha ajabu rais kila siku anasafiri na ndege kwa safari zisizo na tija.
 
Mambo mazito, mamiradi mengi mno ya bajeti ya kufa mtu ya Magufuli alioyaanzisha kwa mpigo ni mzigo mzito kwa taifa na walipa kodi.
Mkuu wacha uongo, wewe si ulisema itachukua miaka 40 kukamilika? Njoo November 2020 uone majaribio Moro - Pugu. Dar bakini na ujanja wenu. JPM alimudu zote hizo sasa wameingia watoto wa watumwa kufuja pesa zilizokusanywa na wenye uchungu wa nchi hii.
 
Sio kweli usitake kutufanya hatujui ukweli, Magufuli alitangaza kwa mbwembwe kuwa SGR kipande cha Dar-Moro kitaanza kazi Nov 2019. Kimsingi huu mradi ulikwama wakati wake.

Tulisema serekali hii haina uwezo wa kutekeleza miradi ya karibia 20t kwa wakati mmoja. Na ukweli huo ulianza kudhibitika toka Magufuli mwenyewe akiwa hai.
 
45 Reactions
Reply
Back
Top Bottom