Inaonesha Waziri Mkuu Majaliwa ni mwepesi wa kudanganywa au huwa anakurupuka

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
2,428
5,883
Ninajua Waziri Mkuu Majaliwa ni mmoja ya viongozi ambao huenda wakatamani kuongoza taifa hili kama Mkuu wa Nchi, lakini hata hivyo namuona akiwa na udhaifu wa ama kukurupuka, au kuwa mwepesi wa kudanganywa na labda kudanganya, ama vyote.

- Mwaka 2021 mwezi Machi, Waziri huyu, nikuamini alijua kuugua kwa Mkuu wa Nchi (Hayati Magufuli), alilitangazia taifa kuwa kiongozi huyo alikuwa mzima wa afya na alikuwa ofisini Ikulu akichapa kazi. Kumbe Mzee wa watu alikuwa hoi na alikosa hata fursa ya kuombewa na watu wake kutokana uongo huu.

Novemba Mwaka huu, akiwa eneo la ajali Precion Air, ama kwa kudanganywa, kwa kutohoji ama kuchunguza taarifa alizopewa, ama kwa kukurupuka, akatoa Taarifa kwa Raisi kuwa ndege iliyopata ajali ilifunguliwa kwa kasia la mvuvi na baadaye abiria kuokolewa na mvuvi Huyo.

Taarifa ya Waziri wa Ujenzi ambayo ni taarifa ya kiuchunguzi imebainisha kuwa wahudumu wa ndege, waliofunzwa taratibu za dharura kama Ile, ndiyo waliofungua mlango huo.

Kwa hali hii, ni wazi kuwa Waziri wetu ama huwa mwepesi kudanganyika au huwa hafanyii upekuzi taarifa anazopewa na hivyo kukurupuka kutoa maelezo.

Kama kiongozi mkubwa na muhimu kwa taifa naona hili haliko sawa kwa Waziri Mkuu wetu.
 
Rais yupo Ikulu anachapa kazi... anawasalimu sana wana Njombe
 
WALIOZEMBEA kutimiza WAJIBU wao kwenye AJALI ya Ndege "WAWAJIBISHWE" Wahusika Wangewahi Hakuna ambaye ANGEKUFA
 
Atakuwa ni aina ya viongozi wanaopenda kukaa ofisini, na kusikiliza mrejesho wa taarifa kutoka kwa wasaidizi wao!

Yaani aina ya viongozi wasiopenda kujiongeza! Wanapenda umwinyi, na umangimeza! Watu wa aina hii, kwao kudanganywa ni jambo la kawaida kabisa.
 
Back
Top Bottom