Waziri Mkuu Majaliwa atoa siku 7 kwa TARURA, DAWASA kukamilisha barabara Muhimbili

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapa siku saba Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam, Godfrey Mikinga na Mkurugenzi wa Usafi wa Usimamizi wa Usafi wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingiza (DAWASA), Lydia Ndibalema wawe wamekamilisha kipande cha barabara ya Mariki kinachoingia geti kuu la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kiwango cha lami.

thumbnail.jpg

thumbnail-1.jpg
Barabara hiyo ambayo ilibomolewa kwa urefu wa mita 60 kupisha matengenezo ya bomba la maji machafu linalotoka katika hospitali hiyo ilipaswa kuwa imekamilika mwishoni wa mwezi wa sita 2023.

Majaliwa amewaagiza watendaji hao kufanya kazi usiku na mchana ili kuepusha adha kwa wagonjwa na wanafamilia wanaoitumia barabara hiyo kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Ametoa maagizo hayo leo Julai 24, 2023 alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua barabara hiyo.

thumbnail-4.jpg

thumbnail-2.jpg
Chanzo: jamhurimedia
 
Back
Top Bottom