Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,851
- 12,088
Majaliwa ametoa ahadi hiyo wakati wa ibada ya kumuaga marehemu Aziz ambapo amesema alikuwa ni moja kati ya waandishi waliokuwa wakiutangaza mkoa huo vizuri. Aziz amepumzishwa katika makaburi ya Mitandi Manispaa ya Lindi.
Aidha, kauli ya Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi, Fatuma Maumba akimzungumzia msibani hapo amesema Abdulaziz Ahmed hakuwa mtu wa kuficha mambo, alikuwa mpambanaji na alifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Wadau wengi.