Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusema leo siku ya 40 ya mwaka mpya anamaanisha nini?

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Natanguliza ombi la msamaha kama ilitokea nimemsikia vibaya Mhe. Waziri mkuu wakati akitoa salamu za serikali wakati wa uapisho wa viongozi, ikulu Dodoma leo.

Mhe. Waziri Mkuu amesema leo ni siku ya 40 ya mwaka mpya wakati leo ni siku ya 10 tu.

Je, Waziri Mkuu alikuwa ana maana gani? Je, nimemsikia vibaya?
 
Kama wasemavyo waswahili "siku za mwizi 40"

40 hutimia siku ya kukamatwa mwizi, inaweza ikawa hata siku ya kwanza kuiba, maybe PM kuna jambo leo amelimaliza/amelikamilisha.
Nimeshtuka sana nilivyosikia ila nahisi nimesikia vibaya. Uso wa furaha wa waziri leo sikuiona kabisa
 
Mwalimu ametumia tafsida, nadhani kuna tukio limehitimika leo,,
Natanguliza ombi la msamaha kama ilitokea nimemsikia vibaya Mhe. Waziri mkuu wakati akitoa salamu za serikali wakati wa uapisho wa viongozi, ikulu Dodoma leo.

Mhe. Waziri Mkuu amesema leo ni siku ya 40 ya mwaka mpya wakati leo ni siku ya 10 tu.

Je, Waziri Mkuu alikuwa ana maana gani? Je, nimemsikia vibaya?
 
Natanguliza ombi la msamaha kama ilitokea nimemsikia vibaya Mhe. Waziri mkuu wakati akitoa salamu za serikali wakati wa uapisho wa viongozi, ikulu Dodoma leo.

Mhe. Waziri Mkuu amesema leo ni siku ya 40 ya mwaka mpya wakati leo ni siku ya 10 tu.

Je, Waziri Mkuu alikuwa ana maana gani? Je, nimemsikia vibaya?
Huyu mtu aliwahi kusema Rais ni mzima wa afya tele anachapa kazi . Na akawadhihaki waliohoji kutoonekana kwake kuwa "wangependa wamuone kariakoo au magomeni." Wakati kesho yake msiba ulitangazwa !!

Nani wa kumuamini huyo hata akisema ni siku ya kwanza !!
 
Naona umecomment vya Arovera bila ya kutafakari.

Hivi ni kalenda gani, iwe ya kiislamu, ya kiyahudi au kibaniyani ambayo ina mwezi wa siku arubaini? Kama amefanya kosa la kutamka ndiyo ahukumiwe kwa kuwa dini fulani?

HAMUWACHI NYINYI YAKHE (kwa herufi kubwa kuweka msisitizo.

Brother K huyo ni wale wa kukurupuka
Yaani mleta mada kasema labda kasikia vibaya, mtu anakuja na hukumu kabisa
Watu kama hawa ukiwapa uhamiaji hupati pasi ukiwa dini hii
Naisikitikia nchi yangu Umasikini, ujinga, maradhi, uchawi na roho mbaya
 
Awamu hii kila mtu ana presha na kale kaogonjwa ka hofu na wasiwasi.
Kuanzia juu hadi chini wote wanafeli sana kuweka mawazo na fikra zao pamoja na mazingira waliyo.
 
Back
Top Bottom