Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amuwakilisha Rais Samia katika Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani nchini Italia

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Oktoba 14, 2023 amewasili Rome, Italia ambapo atamuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani litakalofanyika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kuanzia Oktoba 16, 2023 hadi Oktoba 20, 2023.

Mkutano huo wa wakuu wa nchi na Serikali utaambatana na maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani pamoja na maadhimisho ya miaka 78 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO)

Jukwaa hilo linatarajiwa kuwakutanisha wadau wa kilimo wakiwemo vijana, wakulima, wazalishaji wadogo, watunga sera, wawekezaji katika kilimo na wanasayansi duniani, wote wakiwa na lengo la kuhakikisha kunakuwa na uhakika wa chakula ili kufikia mustakabali bora wa chakula kwa wote na bila kumwacha mtu yoyote nyuma.

Pia, jukwaa hilo litaweka msisitizo kwa nchi husika katika kuchukua hatua za ndani ambazo zinajikita kwenye uvumbuzi, ushirikiano, sayansi, ushirikishwaji wa vijana, wazawa, wanawake na watu walio katika mazingira magumu.

Katika jukwaa hilo la siku nne, Wakuu wa nchi na Serikali kutoka nchi shiriki takribani 31 watapata fursa ya kushiriki katika Mpango wa “Hand-in-Hand Initiative” ambapo watawasilisha mipango ya uwekezaji iliyopewa kipaumbele nchini mwao na kuonesha fursa kwenye maeneo ambayo Mpango huo wa Shirika la Chakula na Kilimo unasaidia Serikali kupunguza umaskini na njaa.

Viongozi Wakuu watakaohudhuria ni Rais wa Italia Mhe. Sergio Mattarella, Rais wa Ireland Mhe. Michael Higgine, Mfalme wa Lesotho, Viongozi wa Ujumbe kutoka Nchi Wanachama, Viongozi Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (FAO, IFAD & WFP).
IMG-20231015-WA0003.jpg
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa Oktoba 14, 2023 amewasili Rome, Italia ambapo atamuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani litakalofanyika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Oktoba 16 hadi Oktoba 20, 2023.
 
Viongozi wetu wanavyosafiri kwenda nchi zilizoendelea huwa hawajifunzi nchi hizo zimeendeleaje waje ku implement strategies zao huku?
 
siku hizi ulaya na USA zamoto siyo kama mwanzoni, uchaguzi wa 2025 tuna raisi mpya, inshallah …
 
Viongozi wetu wanavyosafiri kwenda nchi zilizoendelea huwa hawajifunzi nchi hizo zimeendeleaje waje ku implement strategies zao huku?
Mkuu, Sio kwamba hawaoni ila wanalazimika kuendesha nchi kama wananchi tutakavyo.

Nchi zote zilizoendelea zimekuwa na sera za muda mrefu karibia kila nyanja. Zimekuwa na sera ya mipango miji za miaka na miaka, sera za kuboresha elimu kwa plan ya kuangazia miaka 10,20,30 hadi 50 mbele n.k, n.k kwenye kila nyanja ya ustawi wa maisha ya wananchi wake.

Kila kiongozi anayeingia madarakani anatekeleza sera hizo haijalishi ni wa chama tawala au upinzani.

Ukija hapa kwetu bongoland hakuna hizo sera, na kama zipo basi ni kwenye makaratasi na ni chache zinatekelezwa tena kwa kusuasua.

Viongozi wetu wanawaza zaidi uchaguzi. Mustakabali wa nchi sio kipaumbele kwao. Mawaziri wanawaza nafasi zao, wakuu wa taasisi pia wanawaza nafasi zao, wabunge, wakuu wa mikoa, wilaya n.k muda wa kuwaza maendeleo ni kidogo.
 
17 October 2023

Address by the President of the Republic Sergio Mattarella at the Opening Ceremony of World Food Day​

Rome - Fao, 16/10/2023 (II mandato)

View: https://m.youtube.com/watch?v=8ptMXFaH-HQ

Transcript;

Mr. Director-General Qu,
Your Majesty,
Your Excellency the President of Ireland,
Mr. Prime Minister of the United Republic of Tanzania,
Your Royal Highness the Prince of Jordan,
Authorities,

Ladies and Gentlemen,
I am particularly grateful for the opportunity that was offered me to speak at World Food Day, a stimulating event for the whole International Community, which particularly solicits the most prosperous Countries to multiply their efforts to end hunger in the world and ensure millions of human beings an equitable access to food.

As the Director-General just reminded us, the number of people suffering from malnutrition is increasing, depicting a world that is running alarmingly late in achieving the goals of the United Nations 2030 Agenda – the framework of reference for the goals set forth by the International Community to make life on the planet sustainable.

Today, to achieve this “sustainability” not only means combating hunger at present, but also committing to eradicate the causes underlying it: I am thinking about the persisting difficulties of some of the regions in the world in halting the spiral of poverty, the numerous conflicts, with their aftermath of ever-longer humanitarian crises; the intensity and frequency of natural disasters caused by climate change, which is already conditioning every aspect of our life, devastating territories and claiming lives, as tragically testified by the recent flooding in Derna, Libya.

After all, hunger is the concurrent or triggering cause of violence and also of war, and fighting it constitutes a valuable peace endeavour.

It is a difficult and complex task that requires the awareness of decision-makers to be followed up by a coordinated effort by all.
Instead, what we are seeing is an alarming hike in international tension, a widening divide between Countries and regions of the world and the rebound of imperialistic behaviours and nationalisms.

This is the scenario that UN Secretary-General Guterres efficaciously described as a “multipolar world without multilateralism”, therefore more exposed to geopolitical tensions and an alarming tendency towards a confrontation rather than cooperation between States.

Unfortunately, we are not short of examples of this.
The Middle East is once again up in flames because of the vile attack that has managed to elevate the spiral of horror and violence to unprecedented levels.

But this is not the only case.
The war that has been sowing death and destruction in the heart of Europe over the last 20 months following Russia’s aggression against Ukraine is further evidence of the dangerous tendency to reinstate chaos.

Far from limiting its effects to the regions directly involved in the conflict, the war contributes to increase instability in vast areas of the world and prevalently in the most vulnerable Countries, thus continuing the spread of food insecurity and the lack of basic commodities.

Moscow’s rogue decision to pull out of the grain deal last July further worsens the scenario.
Weaponizing food and water in a conflict is a crime.

On the contrary, food and water are evidence of the indivisibility of the fate of humankind.
The right to food and water is enshrined in the broader right to life and supports the concept of “human security” which requires cooperation.

This is the challenge that we are called upon to meet: give life and dignity to individuals and peoples at all latitudes.

Food insecurity does not only mean food shortage: it also includes lack of access to water and this year’s World Food Day is conveniently dedicated precisely to this aspect.

The challenge posed by water security is age-old; suffice it to think of the sophisticated network of aqueducts that makes up the legacy of Ancient Rome and which won it the title of Regina Aquarum – the Queen of Water – testifying to the ingenuity and determination necessary to ensure access to this precious element.

Today, the shortage or lack of water increasingly underlies poverty and conflict, and its sustainable management needs to be tackled with as much determination and ingenuity as that of any basic commodity that is concomitantly an instrument of peace and a multiplier of wellbeing.

Access to water is a fundamental right that is currently too often at risk, also due to the climate change that causes the desertification of ever-wider areas of the planet.
The challenges that I have recalled – from climate change, to rising conflict and the ensuing food and water shortages – have a common denominator: they are all transnational.

This creates the need to combat these risks by resorting to the unique, formidable, and available instrument represented by the United Nations, making the most of its capabilities and, for what concerns agriculture and nutrition, to the UN Agencies that we proudly host here in Rome.

FAO, the World Food Program, and IFAD concur to decisively respond to the problem of food security from different perspectives.

The challenge posed by the scourge of hunger – a moral even more than socio-economic imperative – can and must be won by focusing back on the centrality of multilateral commitment and the United Nations’ capacity to effectively combine the human, technological, and financial resources of single States, allocating them where they are needed, thus creating lasting development.

It is a commitment that the Italian Republic actively supports and that has led us to co-organize with FAO the second UN Food Systems Summit here in Rome last July, turning food security into one of the priority themes of the Italian Presidency of the G7.

It is with the firm resolve to contribute to building sustainable and resilient food systems that I would like to express my gratitude to all those who work to achieve this goal at different levels and in different geographical contexts.
Thank you
 
16 October 2023
Rome, Italy

Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Italia Mh. Sergio Mattarella

1697590115080.png


Mkurugenzi Mkuu Qu,
Mheshimiwa Rais wa Ireland,
Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mtukufu mwana wa mfalme wa Jordan,


Mabibi na mabwana ,
Nashukuru sana kwa fursa niliyopewa ya kuzungumza katika Siku ya Chakula Duniani, ni tukio la kusisimua kwa Jumuiya nzima ya Kimataifa, ambayo hasa inazitaka Nchi zilizostawi zaidi kuzidisha juhudi zao za kumaliza njaa duniani na kuwahakikisha mamilioni ya watu upatikanaji wa chakula kwa usawa.

Kama Mkurugenzi Mkuu alivyotukumbusha hivi punde, idadi ya watu wanaokabiliwa na utapiamlo inaongezeka, ikionyesha dunia inachelewa sana kufikia malengo ya Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 - ramani ya maendeleo endelevu yaliyowekwa na Kimataifa kufanya maisha kwenye sayari kuwa endelevu.


Leo, kufikia "uendelevu" huu haimaanishi tu kupambana na njaa kwa sasa, lakini pia kujitolea kutokomeza sababu zinazoisababisha: Ninafikiria juu ya shida zinazoendelea za baadhi ya maeneo ulimwenguni katika kukomesha wimbi la umaskini, migogoro, pamoja na matokeo yake ya machafuko ya kudumu yanayosababishwa na binadamu; ukubwa na marudio wa majanga ya asili yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, ambayo tayari ni sehemu ya maisha yetu, yenye kuleta uharibifu na kupoteza maisha, kama ilivyoshuhudiwa kwa huzuni na mafuriko ya hivi majuzi huko Derna, Libya.

Baada ya kusema hayo , njaa pia ni sababu mojawapo ya kuchochea ya vurugu na pia vita, na hivyo ni muhimu kupigana na njaa ikiwa ni mojawapo ya jitihada muhimu za hukakikisha amani. Ni kazi ngumu na inayohitaji mwamko kwa watoa maamuzi kufuzifuatilia juhudi hizi zinazohitaji kuratibiwa na wote.

Badala yake, tunachokiona ni ongezeko la kutisha la mvutano wa kimataifa, mgawanyiko unaoongezeka kati ya Nchi na maeneo ya dunia na kurudi nyuma kwa tabia za kibeberu na utaifa.

Hii ndiyo hali ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Guterres aliielezea kwa ufasaha kuwa "ulimwengu wa pande nyingi usio na pande nyingi" (multipolar world without multilateralism), kwa hiyo uko wazi zaidi kwa mivutano ya kijiografia na hali ya kutisha kuelekea makabiliano badala ya ushirikiano kati ya Mataifa.
Kwa bahati mbaya, mifano hai ya aina hii ipo .


Mashariki ya Kati kwa mara nyingine tena moto umelipuka kwa sababu ya mashambulizi mabaya ya kinyama ambayo yameweza kuchochea hali ya kuogofya na vurugu hadi kufikia viwango vya kutisha.

Lakini hili tukio la Mashariki ya Kati siyo pekee. Vita vinavyo endelea katikati ya ulaya ambavyo vinaleta vifo na uharibifu kwa muda wa miezi 20 iliyopita kufuatia uchokozi wa Urusi dhidi ya Ukraine ni ushahidi zaidi wa mwelekeo hatari wa kurejesha machafuko.

Vita na mchafuko mbali na kuzua athari zake hasi kwa kanda zinazohusika moja kwa moja katika mzozo huo, vita vinachangia kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na utulivu katika maeneo ya bara za mbali na kwa kawaida kuziathiri pakubwa Nchi zilizo masikini zaidi, na hivyo kuendeleza kuenea kwa uhaba wa chakula na ukosefu wa bidhaa za kimsingi. Na uamuzi mbaya wa Moscow (Urusi) wa kujiondoa katika mpango wa nafaka Julai iliyopita unazidisha hali hiyo.


Kutumia chakula na maji kama silaha ya kivita ni uhalifu. Hivyo chakula na maji unatupa ushahidi wa jinsi unavyotufungamanisha katika hatima yetu moja ya ubinadamu. Kuwa Haki ya chakula na maji imeainishwa katika haki ya msingi pana ya kuishi na kuunga mkono dhana ya "usalama kwa binadamu" ambayo inahitaji ushirikiano wa wote .

Hii ndiyo changamoto ambayo tunatakiwa kukubaliana nayo: kuhakikisha uhai na utu kwa w
mtu binafsi na kwa watu katika tabaka zote.

Kukosekana kwa usalama wa chakula haimaanishi tu uhaba wa chakula: pia inajumuisha ukosefu wa maji na kuadhimisha Siku ya Chakula Duniani ya mwaka huu imefungamanishwa na kipengele hiki cha maji.

Changamoto inayoakisi usalama wa maji ni ya zamani; inatosha kuangalia mtandao wa kisasa wa mifereji ya maji ambayo tumeurithi toka enzi ya dola ya Roma ya Kale na ambayo ilipewa jina kubwa la heshima la Regina Aquarum - Malkia wa Maji - kuonyesha hekima na kutoa azimio kuhusu umuhimu katika zama zetu hizi kuhakikisha upatikanaji hiki cha thamani kwa wote yaani maji.


Leo, uhaba au ukosefu wa maji unazidi kuwa kichocheo cha kuleta umaskini na migogoro, na usimamizi wa upatikanaji maji endelevu unahitaji kushughulikiwa kwa dhamira na ustadi mwingi kama ule wa bidhaa yoyote ya msingi ambayo wakati huo huo ni chombo cha amani na kiboreshaji cha ustawi.

Upatikanaji wa maji ni haki ya kimsingi ambayo kwa sasa iko hatarini, pia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo husababisha kuenea kwa jangwa kwa maeneo mengi zaidi ya ulimwenguni.

Changamoto ambazo nimekumbuka - kutoka kwa mabadiliko ya hali ya hewa, hadi kuongezeka kwa migogoro na uhaba wa chakula na maji - zina hila moja: zote haziishii ndani ya taifa fulani, bali zinavuka mipaka ya nchi.

Hii inaleta hitaji la kupambana na hatari hizi kwa kutumia njia ya kipekee na linalowakilishwa na Umoja wa Mataifa, huku ikitumia vyema uwezo wake na, kwa azimio la leo linaloangazia kuhusu kilimo na lishe, kwa kushirikiana na maShirika ya Umoja wa Mataifa ambayo tunajivunia kuwa wenyeji hapa nchini. Roma.

Mashirika hayo FAO, Mpango wa Chakula Duniani, na IFAD wanakubaliana kwa dhati kukabiliana na tatizo la usalama wa chakula kutoka mitazamo tofauti.

Changamoto inayoletwa na baa la njaa - ni jambo la kimaadili zaidi ya masuala ya kijamii na kiuchumi - tunaweza na lazima kushinda kwa kuzingatia msingi imara wa dhamira ya kimataifa na uwezo wa Umoja wa Mataifa wa kuunganisha kwa pamoja nguvu za rasilimali watu, teknolojia na fedha pia wa Nchi moja, kuzigawa pale zinapohitajika, hivyo basi kuleta maendeleo endelevu ya kudumu.

Ni azimio ambalo Jamhuri ya Italia inaunga mkono kikamilifu na ambayo imetuongoza kuandaa na FAO Mkutano wa pili wa Mifumo ya Chakula ya Umoja wa Mataifa hapa Roma Julai iliyopita, na kugeuza usalama wa chakula kuwa moja ya mada za kipaumbele za Urais wa Italia wa G7.

Ni kwa azimio thabiti la kuchangia katika ujenzi wa mifumo endelevu ya chakula ambapo ningependa kutoa shukrani zangu kwa wale wote wanaofanya kazi ili kufikia lengo hili katika viwango tofauti na katika mazingira tofauti ya kijiografia.
Asanteni
 
Back
Top Bottom