Waziri Mkuu aelezea ubadhirifu wa mamilioni uliofanywa Bohari ya Dawa (MSD), asema ataenda akiongozana na Polisi na TAKUKURU

Waliposema kula kulingana na urefu wa kamba yako wslisahau kuwa kamba nyingine ni za nailoni, hizi zinavutika, kama mashine inauzwa shs 20,000,000/= ikinunuliwa kwa shs 100,000,000/= simbaya kulingana na kamba ya nailoni inayovutika.
 
Matumizi ya dini ndiyo kazi yenu ikitokea Rais katoka kinyume na nyie basi mnakutana kuanzia kwenye vigango tumeiona tangu kwa Mzee wa ruksa Mkwere na sasa kwa Mama hamkomi tu wadini nyie
Mlifungwa midomo watu wanaokotwa kwenye viroba kutekwa kusikoisha bado tu hamshukuru kupata nafasi ya kupumua?
Unasema uongo. Magufuli alikua hakosolewi humu? Au umejiunga na jf leo?
 
taarifa za CAG katika TPA, TANROADS na Wizara ya Ujenzi.
Taarifa za CAG sio kwamba mchakato umefika mwisho ,Bali anaibua hoja alizoziona alafu ,zinaanza kujibiwa baada ya Bunge kuzijadili, serikali wanazijibu zote ,hapo Sasa ikitokea mapungufu ndio ndio inaweza kusema kweli zimeibiwa
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amkute katika ofisi za Bohari ya Dawa (MSD) Jumatatu saa nne asubuhi, baada ya kubaini madudu katika ununuzi wa vifaa vya matibabu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo katika ufunguzi wa Wiki ya Ununuzi wa Umma jijini Arusha ambapo ametaja gharama kubwa iliyotumika kununua vifaa hivyo tofauti na bei halisi za soko, na hivyo kupoteza fedha nyingi za umma na kuwakosesha wananchi huduma kwani vifaa vilivyonunuliwa ni vichache.

Akizungumza na wataalamu wa ununuzi na ugavi, ametaja baadhi ya manunuzi hayo kama vile ununuzi wa seti moja ya vitenganishi kwa ajili ya awamu moja ya kusafisha damu kwa shilingi 65,000, lakini wakanunua kwa shilingi 189,000.

Aidha, MSD walitakiwa kununua mashine ndogo ya kipimo cha haemolojia ya mwili kwa shilingu milioni 5, lakini wakanunua kwa shilingi milioni 14,045,000.

Ametoa mfano mwingine ambao ni kipimo kikubwa cha haiemolojia ya mwili ambacho ni shilingi milioni 37, lakini MSD wamenunua kwa shilingi milioni 147.9, pia walitakiwa kununua mashine ya kuchakata maji kwa ajili ya kusafisha damu ambacho kinauzwa milioni 32 lakini wamekinunua kwa shilingi milioni 129.

"Kwanini hili linatokea? kwa maslahi ya nani?" amehoji Waziri Mkuu

Kutokana na PSPTB kuwa na jukumu la kuwachukulia hatua wataalamu wa ununuzi na ugavi wanaokiuka sheria, Waziri Mkuu Majaliwa ameiagiza kufika ofisi za MSD akisisiitiza kuwa serikali haiwezi kukubali hali hiyo kuendelea.

"Na mimi sitasita kwenda na Kamanda Sirro, na Kamanda Hamduni, ili washughulike na watu. Lazima tuanze na watu hawa wanaofanya kazi hii, wakae nje, hatua nyingine zifuate," amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa

Ameongeza kuwa pengine wasimamizi wa vitengo vya ununuzi na ugavi wanahitaji kuapishwa, kutokana na unyeti wa nafasi zao katika kutoa huduma kwa Watanzania.

Tumpe Urais huyu mwamba. Anawashulikia wahalifu, hawambembelezi.
 
Akizungumza na wataalamu wa ununuzi na ugavi, ametaja baadhi ya manunuzi hayo kama vile ununuzi wa seti moja ya vitenganishi kwa ajili ya awamu moja ya kusafisha damu kwa shilingi 65,000, lakini wakanunua kwa shilingi 189,000.

Aidha, MSD walitakiwa kununua mashine ndogo ya kipimo cha haemolojia ya mwili kwa shilingu milioni 5, lakini wakanunua kwa shilingi milioni 14,045,000.

Ametoa mfano mwingine ambao ni kipimo kikubwa cha haiemolojia ya mwili ambacho ni shilingi milioni 37, lakini MSD wamenunua kwa shilingi milioni 147.9, pia walitakiwa kununua mashine ya kuchakata maji kwa ajili ya kusafisha damu ambacho kinauzwa milioni 32 lakini wamekinunua kwa shilingi milioni 129.

"Kwanini hili linatokea? kwa maslahi ya nani?" amehoji Waziri Mkuu
Hao si wamepelekewa mkurugenzi mpya hivi karibuni tu!!!
 
Back
Top Bottom