Hongera sana Waziri Mkuu kwa kuwachukulia hatua waliohusika na ubadhirifu wa fedha za Halmashauri

usiue ALBINO

Member
Aug 14, 2023
73
64
Kitendo cha Waziri mkuu kutoa amri ya kuchukuliwa hatua wote waliohusika na ubadhirifu wa fedha za halmashauri, kinatia moyo ingawa bado tungefurahi zaidi tutakapopata mwendelezo wa hatua hiyo.

Matamko yasiishie kwenye vyombo vya habari.

Baada ya hapo tuanze kuona hatua zikichukuliwa pia kwa wale wote waliotajwa kwenye waraka wa CAG
Endapo viongozi wa serikali hawatakuwa na mizaha na kuleana basi walau wananchi watarejesha imani kwa serikali yao.

Mara nyingi amelaumiwa Rais kwa uzembe unaofanywa sehemu mbali mbali kwenye taasisi za umna, wakati kuna watendaji ambao wamepewa dhamana kusimamia idara au taasisi hizo jambo ambalo limepelekea katibu mwenezi wa chama cha ccm kuonekana kuwa anaingilia madaraka yasiyo yake.

Kwa upande wa waandishi wa habari,tunaomba wawe na mwendelezo wa kufuatilia habari wanazo zitoa kwa wananchi badala ya kufanya mambo kwa mihemko na upendeleo kwa baadhi ya taarifa.
 
Inasikitisha sana hawa watendaji wa chini walikuwa wapi mpaka Waziri Mkuu anatoa amri ya mhasibu kukamatwa na kupelekwa mahabusu
 
Kiongozi angekuwa hana Chama
Sasa hapo wanabebana tu
Mbele ya watu viroja vingi na biti za uhakika
Ila hutasikia mtu kafungwa miaka 30
 
Back
Top Bottom