Waziri Mkuu aelezea ubadhirifu wa mamilioni uliofanywa Bohari ya Dawa (MSD), asema ataenda akiongozana na Polisi na TAKUKURU

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,267
5,366
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amkute katika ofisi za Bohari ya Dawa (MSD) Jumatatu saa nne asubuhi, baada ya kubaini madudu katika ununuzi wa vifaa vya matibabu.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo katika ufunguzi wa Wiki ya Ununuzi wa Umma jijini Arusha ambapo ametaja gharama kubwa iliyotumika kununua vifaa hivyo tofauti na bei halisi za soko, na hivyo kupoteza fedha nyingi za umma na kuwakosesha wananchi huduma kwani vifaa vilivyonunuliwa ni vichache.

Akizungumza na wataalamu wa ununuzi na ugavi, ametaja baadhi ya manunuzi hayo kama vile ununuzi wa seti moja ya vitenganishi kwa ajili ya awamu moja ya kusafisha damu kwa shilingi 65,000, lakini wakanunua kwa shilingi 189,000.

Aidha, MSD walitakiwa kununua mashine ndogo ya kipimo cha haemolojia ya mwili kwa shilingu milioni 5, lakini wakanunua kwa shilingi milioni 14,045,000.

Ametoa mfano mwingine ambao ni kipimo kikubwa cha haiemolojia ya mwili ambacho ni shilingi milioni 37, lakini MSD wamenunua kwa shilingi milioni 147.9, pia walitakiwa kununua mashine ya kuchakata maji kwa ajili ya kusafisha damu ambacho kinauzwa milioni 32 lakini wamekinunua kwa shilingi milioni 129.

"Kwanini hili linatokea? kwa maslahi ya nani?" amehoji Waziri Mkuu

Kutokana na PSPTB kuwa na jukumu la kuwachukulia hatua wataalamu wa ununuzi na ugavi wanaokiuka sheria, Waziri Mkuu Majaliwa ameiagiza kufika ofisi za MSD akisisiitiza kuwa serikali haiwezi kukubali hali hiyo kuendelea.

"Na mimi sitasita kwenda na Kamanda Sirro, na Kamanda Hamduni, ili washughulike na watu. Lazima tuanze na watu hawa wanaofanya kazi hii, wakae nje, hatua nyingine zifuate," amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa

Ameongeza kuwa pengine wasimamizi wa vitengo vya ununuzi na ugavi wanahitaji kuapishwa, kutokana na unyeti wa nafasi zao katika kutoa huduma kwa Watanzania.
 
shida kuna vikundi pale kazi yao kupeana ulaji tu kwa hiyo tabia zao ni kula tu hawasikii wengine, bado staffing haiko sawa, hakuna usawa, matabaka kimaslahi yalijiimarisha toka alipoenda victoria elangwa akaiambukiza timu yote ya menejiment imeendelea hivyo. manunuzi ya dawa pale yanawafaidisha sana baadhi ya watu trip za nje ya nchi kufatilia 10% toka enzi hizo
 
Kudeal navisivyoonekana kazi Sana
Watakamatwa leo ..kesho wapya nao wanakuwa wezi .
POWER OF IDEA Ni milele huishi.
 
Enzi zimeshapita, mkwara kama huu wakati wa JPM tayari watu wangeshakimbia nchi. Lakini huyu wa kukunwa vizuri na kupapasa ndo wamekula kwa urefu wa kamba zao.
Eti wahalifu wamsubiri aende na siro na hamduni utafikiri huko hakuna polisi wa kuwaweka ndani.
Acha aupige mwingi.
January oyeee
Nape oyeee
Riz1 oyeee
Mama wa mafao ya wake za viongozi oyeee

Haya majizi msubirini katelefone anakuja na siro na hamduni.
 
Na hatua zichukuliwe kweli-kweli otherwise haitakuwa tofauti na upepo unaovuma.
 
hapa sasa kizungumkutiiiii, MSD ni zaidi ya tuijuavyoo
nadhani hata mkurugenzi mpyaa asipojengewa mazingira mazuri ya kiutendaji (kuifumua MSD yote) hatoweza kuleta utendaji bora kutoka alikokuwepo (secta binafsi) kuja serikalini
Well said !!!
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom