Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete apewe maua yake kwa kupambana na wazembe na mafisadi

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
1702647567955.png

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amesema serikali imeamua kujenga Mfumo wa Kitaifa wa Kielektroniki wa Ununuzi Tanzania (NeST) ili kukabiliana na changamoto ya Rushwa katika mfumo wa manunuzi ya serikali.

Kikwete ameyasema hayo wakati akifunga Kongamano la 14 la mwaka la wataalamu wa ununuzi na ugavi zaidi ya 900, Kongamano lililofanyika Jijini Arusha, Desemba 14.2023 lenye kauli mbiu isemayo, 'Mabadiliko ya Kidijitali kwa ajili ya kuboresha Usimamizi na ugavi kuelekea Maendeleo endelevu'.

"Zaidi ya asilimia 72 ya Bajeti ya serikali inatumika kwenye manunuzi ya umma, lakini eneo hili la ununuzi wa umma limekuwa likiripotiwa kugubikwa na vitendo vya Rushwa na ubadhirifu na kutokana na uzito huo, Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao imeamua kusanifu, kujenga na kusanikisha Mfumo wa Kitaifa wa Kielektroniki wa Ununuzi Tanzania (National e-Procurement System of Tanzania- NeST) ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo" -Ridhiwani Kikwete.

Amesema mfumo huo utasaidia kuondoa mianya ya Rushwa na upendeleo na hivyo thamani ya pesa za Serikali katika bidhaa na huduma italindwa kwani kutakuwa hakuna ulazima wa watu kukutana ana kwa ana.

Jambo TV
 
Namuona dogo nyota yake iking'ara kuliko hayo mabumunda mengine yanayomtumia mange kuitukana serikali. Ridhiwani yupo makini sana na umri unamruhusu. Huyu kwangu ndio future president wa ukweli baada ya mama .Nimesimama pale.
 
Is this supposed to be a Joke ?!!!
All I can Say is....CURA TE IPSUM - (Physician Heal thyself)
 
Lini mtaielewa serikali yenu? Hapo lengo kuu ni utengenezaji wa huo mfumo na si kupambana na rushwa katika manunuzi kama ilivyosemwa.
 
Back
Top Bottom