Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,061
- 11,667
Joint venture ili kumpata mwekezaji wa Bongo. Ndio mtindo wa kisasa Serikali yetu imejiwekea inapoingia kwenye mradi na makampuni ya kigeni.
Ni mawazo potofu kufikiri kuwa open tenda ndiyo itakayo hakikisha kupata the best. On the contrary, mara nyingi makampuni yenye uwezo hayaingii kwenye open tenda. Hii ni kutokana na ukweli kuwa ku-participate kwenye tenda ni gharama na ni kamari. Kwenye open tenda kwa vile vikampuni vya kila namna vinaweza kuingia na ku-ofa the earth basi yale makubwa hayaingii. Makampuni yanayopenda tenda hizi ni yale machanga na yale ya kitapeli. Ya kitapeli yanapenda kwa sababu kutokana na uwingi wa wazabuni basi kuna tumaini na uwezekano wa kutofanyiwa due dilligence ya uhakika. Vile vile nayo yanajua kuwa makampuni ya uhakika hayatajipeleka.
Kwenye specialised case kama hii, ni bora zaidi kufanya restricted tenda. Hii inatokana na ukweli kuwa makampuni yenye utaalamu huu yanajulikana. Ni vizuri kuyaalika ( kutoka na uzoefu wao) ili ya submit tenda. Tenda ya namna hii inakubalika nao maana wanajua kuwa wanashindana na watu wa saizi yao. Mfano rahisi. Kama unataka kuagiza simu za mkononi kwa wingi ( mamilioni), hautangazi open tenda. Unawakaribisha Nokia, Samsung, Sony Ericsson, LG, Apple, BenQ kutenda. Ukitangaza ya wazi kuna hatari ya kuingia mtu atakaekuletea product fake kwa bei ya chini kuliko ya watengenezaji wenyewe.
Kwa kuzania open tenda, siasa ilitawala kuliko ufanisi. Na hiki ndicho kilichotufikisha hapa na mwisho wa siku kutuacha na majuto.
Zoezi na mradi mzima ufutwe. Hauna maslahi kwa taifa.
Amandla......
......... Mimi si mtalaam wa sheria, lakini kwa uelewa wangu JOINT VENTURE AGREEMENT (JVA) ni muhimu sana kuliko hata Audited Financial Report ya Kampuni. JVA inaonyesha legal existence ya hiyo kampuni, sasa kama kwenye maelezo yao walisema wanashirikiana na kampuni fulani na hakuna JVA, si tutarudi kule kule kwa akina Richmond ambapo watu walipewa business card na wakaamini kwamba Richmond ilikuwa na uhusiano na hiyo kampuni nyingine na kumbe ni utapeli mtupu. Leo tunataka kurudi huko huko kwa marehemu Richmond, hivi jamani hatujifunzi kutokana na makosa yaliyopita? Financial Report inaonyesha financial status ya kampuni kitu ambacho external auditors wa kampuni wanaweza kufunika bovu na watu wakalishwa kasa.
Ukisoma barua ya Mh. Masha utagundua kwamba yeye kwa mawazo yake anaona JVA ni kitu minor sana. Tunaweza kujikuta tunaingizwa mkenge na kampuni ikidai ina ushirikiano na kampuni yenye jina kubwa na kumbe hakuna ushirikiano wowote.
Je, SAGEM walijuaje kwamba wametolewa kwenye mchakato katika hatua za awali na kiasi cha kwenda kwa waziri kulalamika? Pinda alisema Bungeni kwamba kuna swala la siri kuvuja, nani alivujisha siri? Masha akiwa kama Waziri wa Mambo ya Ndani, kwanini hakutaka kuchunguza hao SAGEM walipataje taarifa hizo ili kama wajumbe wa Bodi ya Zabuni wamevujisha basi ingekuwa nafasi yake nzuri sana kuwa-deal.
Ninachokiona hapa ni kwamba mzizi wa barua ya Masha ni utetezi baada ya kuona Bodi ya Zabuni wameshikilia msimamo wao kwamba hawaoni tatizo kwenye mchakato mzima. Kitendo cha Masha kuanza kuuliza kwanini SAGEM walitemwa kiliwapa hisia hao wana Bodi ya Zabuni kwamba huenda Masha ana nia ya kuibeba kampuni ya SAGEM. Ili kujilinda ndipo akaamua kuandika barua hiyo ambayo naona imejaa utetezi na kulalamika kwamba Luhanjo anamwingilia kwenye wizara yake. Sijaona hata sehemu moja ambayo Masha ametetea maslahi ya serikali ama taifa, kama ni nia njema hata Lowassa alikuwa na nia njema kabisa na alitupatia "BEST DEAL" ya richmond ambayo bado inaendelea kutu-deal mpaka leo hii.
Nakubilana na wewe kwamba open tenda inweza kuwakatisha tamaa "serious" companies....Lakini kama hizi "serious" companies kama zinafahamu kwamba tendering iko nayo "serious" (i.e. nepotism and corruption free) si wangeweza kuingia kwenye tenda na uhakika kwamba kampuni changa na za kitapeli zitatolewa kwenye mapema mapema kwenye beauty contest... Kutumia mfano wako juu wa simu za mkononi; Evaluation commitee si inauwezo wa kutofautisha kampuni kama "Nyantuzu Mobiles", "danganyikeni supplies" na zile zenye majina kama LG, Sony Ericsson, Samsung NK?.... La maana haswa n kwamba mwisho wa siku, kampuni kama "Nyantuzu phones" haiwezi kuwa na uwezo wa kuwasilisha hizo simu kwa bei ya chini kuliko manufacturers wenyewe kama LG au Sony Ericsson? .....Sikatai kwamba kuna vitu kama import duty kampuni kama nyantuzu phones inaweza kukwepa kujipa advantage, lakini vilevile si ni vitu ambavyo serikali inaweza kusimamia?...Tunaweza kwenda mbali na argument hii, lakini kwa ufupi ni kwamba "open tender" sio kikwazo cha kupata "best deal"...
Wote tunajua kwamba uswahili huu wa "Joint venture agreements" na local entities ni njia ya ufisadi tu, haswa kwenye area ya teknologia. Lazima nikubaliane na Masha kwamba ni "Minor issue" . JVA ni njia mojawapo ya kuwapa mamemba wa tendering board na evaluation commitee na wapambe wao njia ya kula in the long term... Mbona huu upuuzi haupo ulaya kwenye "dili ndogo" kama hii (152 mio USD)?...Sagem ikija Tanzania kuna manufaa gani ambayo wananchi/serikali haiwezi kuyapata bila kuwepo huyu local partner fisadi wa JVA?.. Nafasi za kazi kwa wananchi? Hapana, serikali inaweza kusimamia.....Ushuru? hapana, serikali inaweza kusimamia! Hayo mambo ya JVA yanaongeza mzigo kwa wananchi wote.... Haswa haswa kwenye mambo ya teknologia yanaleta expenses ambayo wananchi lazima wabebe... Uliza kampuni zozote Tanzania ambazo zimelazimishwa kuwa na JVA kama hizo JVA zimewasaidia? ... Shida ambayo naziona na kwenye kutokua na JVA ni kwenye kampuni za kichina kama Huawei ambao wanaleta wachimba mitaro na wapiga rangi toka kwao... Lakini huu sio uzembe wa serikali?... au JV partner wao ndio anawapa kifua wasiwape wananchi kazi hata za kuchimba mitaro?
Kuna taarifa zimepikana sasa hivi kuwa Masha na Wapambe wake wameisha wanunua baadhi ya waandishi wa habari wa magazeti fulani ili wamsafishe, na pia wawachafue washauri wa Mradi na Waziri mmoja, Zitto na Dr. Slaa. Majina ya waandishi hao, magazeti watakayoyatumia yametajwa na report wanayoiandaa imepatikana pia. Naifanyia kazi kabla ya kuitoa hadharani (Katika JF).
Ijumaa ya tarehe 30.01.2009, Waziri Masha alionekana akimpa "documents" mwandishi wa habari ambae ni Mhariri wa moja ya magazeti yaliyonunuliwa kufanya kazi hiyo. Inaaminika kuwa moja ya "documnts" hizo zilitmika ktk matoleo ya magazeti yalifuata, yaani kuanzia Jumatatu ya tarehe 2 February 2009 na Alhamis ya tarehe 5 February 2009.
Namalizia mchango wangu kwa kuwapa hiki hapa!
Sagem to deliver access control for Dutch government
Welcome to Security Systems News Europe
THE HAGUE--Sagem Securite subsidiary Sagem Identification has been selected by the Dutch government to provide security measures for the lower chamber and ministerial sites, the company announced Friday.
Sagem Identification will begin delivering new identity cards to government employees on April 1 of this year.
I'm out and over... for sure watu kama hawa hawezi kutoa 10% hivyo... jamaa waliokaa kwenye hiyo mikutano wangeambulia zero.
Nadhani hapa CS na genge lake walifikiri kuwa Masha ange-bow out halafu ingekuwa business as usual. Lakini kitendo cha Masha kuandika kwa PM kimewaudhi sana wakuu. Kwa hiyo kinachofanyika ni kuhakikisha wanamgeuzia Masha kibao. Trust me, kama masha angekubali kukaa kimya wala tusingejua nini kinaendelea.
Bravo Masha
Bla bla nyiiingi kama kawaida ya Mdanganyika, akijua kitu basi ndio ooh najua najua, procurement procument, jurisdiction na ma PS, kama hujui nyamaza, inaonekana hujui etc etc Kisa kuna mtu alisema kama unajua sema basi.
Sio Kwamba alikuwa hajui bali ni katika kutuliza mzuka wa kujua. Yaani imekuwa kama kwenye kijiwe cha tangawizi.
What if Masha angenyamaza na hii process fake ikaendelea? Hii skewness ili kumbomoa Masha imezidi. Punguzeni chuki na muangalie upande wa pili wa shilingi ili kuweka fair judgement.
.....hakuna cha skewness hapa......Masha anajadiliwa kulingana na kitendo alichokifanya......ukiwa Waziri/mwansheria haina maana upindishe kanuni za field usiyoifahamu..........na ndio maana tuliishia ktika UPUUZI wa RICHMOND...........
......you can say anything you want......hakuna anyemchukia Masha hapa........ni facts tu.........kama unaona ni blah blah you better go back to school..........
........siku zote hapa tunalilia utawala wa sheria....kumbe ndani ya mioyo yenu ni "MIFISI"........no wonder "WAAFRIKA NDIVYO TULIVYO"
Kwa nini unaangaliwa upande mmoja tu wa Masha, kwa hakuna mwingine anayeweza kuwa ndio root course ya hilo tatizo.
Kuna Mengi yamejificha hapa, na la kwanza ni uhusiano kati ka Masha na Katibu Mkuu wake! Inakuwaje Katibu Mkuu anamby pass Waziri wake?
Kwenye post yako moja ndugu mtaalam umesema kuwa waziri ana input kwenye cabinet paper, iweje leo katibu Mkuu wa Waziri na Katibu Mkuu Kiongozi wanafanya mawasiliano bila kumshirikisha Waziri (naomba sababu za kikanuni au kisheria tafadhali)
Kama Katibu aliona kuna mushkeli katika maagizo au maamuzi au utendaji wa waziri katika mambo ya tender, kwa nini asimtaarifu waziri mwenyewe kwamba hapa boss una/mechemsha hivyo hili suala naliforward kwa boss wangu mwingine ambaye ni Katibu Mkuu kiongozi?
Kwa vile watu wameshakariri Masha mtoto, Masha Fisadi, Masha hawezi kazi, Masha mbabe basi watu weeee watasema kila possibility hadi aonekane guilty.
Binafsi sina ubia na Masha wala mafisadi. Ningependa rule of law Tz, sio siasa za fitina, kutegena, majungu, inferiority compelexes na chuki kama wanavyomfanyia Masha.