Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 400
- 1,004
Moja kwa moja kwenye mada,
Uongozi wa Kijiji Arumeru, Mkoa wa Arusha ulipitisha sheria ndogondogo za kukuza maadili baada ya matukio ya vijana kuuawa kwa makosa ya kuiba na mmomonyoko wa maadili ikiwemo kunyoa viduku na kuvaa vimini ndio sababu!
Waziri Dkt. Gwajima D uko serious kabisa ku endorse huu ujinga (respectfully)? Ni kweli kunyoa kidugu, kusuka nywele na kuvaa vimini ndio kunachangia mmonyoko wa maadili? Hili ni jambo ukaona uliunge mkono?
Tanzania na Afrika kwa ujumla imepambwa na tamaduni nyingi za kupendeza na baadhi ya mambo ni mitindo mbalimbali ya nywele na mavazi. Kutoka na muingiliano wa watu vitu vingine vinaenda na kubadilika mengine yakiwa sehemu ya buruduni, kama vile Ronaldo alivyoteleta kisahani na kikabamba. Sasa hii ni sababu ya kumfanya mtu atoe fine?
Huwezi kumpangia mtu cha kuvaa au mtindo wa nywele kama havunji sheria yoyote, shughulika na mzizi wa tatizo sio mambo ambayo hayana maana.
Nguo fupi au viduku vingekua ni sababu mababu zetu ndio sasa ndio watakuwa watu washenzi na waliokosa ustaarabu kuliko wote, Watindinga na Wahadzabe na wote wenye kufanana nao watakuwa hawana maana kabisa.
Vipi mwanaume akivaa bukta fupi huyu nae anaenda kulipa fine? Akiwa anapiga kazi zake huko juani shati kaliweka kiunoni anatembea kifua wazi, hapa vipi, anakuwa kamomonyoa maadili ya kijiji kizima?
Kijana akiwa kijiweni bila shughuli ya kufanya nayo fine, kwa soko gani la ajira la kuzuia vijana kuranda hovyo? Waziri Dkt. Gwajima D kuwa serious bwana, badala ya kuunga mkono hili ilitakiwa kutafuta njia ya kumaliza mzizi wa tatizo.
Vijana wanajiingiza kwenye wizi, badala ya kuweka sheria ambazo hazina maana uundwe mradi wa kuwaghulisha au wapewe ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuishia kwenye uhalifu. Wewe ni mmoja wa watu smart sana serikalini usifanye vitu vya kijinga kama hivi vikaharibu CV yako.