Waziri Gwajima tengua uamuzi wako wa kuunga mkono sheria ya maadili Arusha, hili ni bomu unatengeneza

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Moja kwa moja kwenye mada,

Uongozi wa Kijiji Arumeru, Mkoa wa Arusha ulipitisha sheria ndogondogo za kukuza maadili baada ya matukio ya vijana kuuawa kwa makosa ya kuiba na mmomonyoko wa maadili ikiwemo kunyoa viduku na kuvaa vimini ndio sababu!

Waziri Dkt. Gwajima D uko serious kabisa ku endorse huu ujinga (respectfully)? Ni kweli kunyoa kidugu, kusuka nywele na kuvaa vimini ndio kunachangia mmonyoko wa maadili? Hili ni jambo ukaona uliunge mkono?

Tanzania na Afrika kwa ujumla imepambwa na tamaduni nyingi za kupendeza na baadhi ya mambo ni mitindo mbalimbali ya nywele na mavazi. Kutoka na muingiliano wa watu vitu vingine vinaenda na kubadilika mengine yakiwa sehemu ya buruduni, kama vile Ronaldo alivyoteleta kisahani na kikabamba. Sasa hii ni sababu ya kumfanya mtu atoe fine?

Huwezi kumpangia mtu cha kuvaa au mtindo wa nywele kama havunji sheria yoyote, shughulika na mzizi wa tatizo sio mambo ambayo hayana maana.

Nguo fupi au viduku vingekua ni sababu mababu zetu ndio sasa ndio watakuwa watu washenzi na waliokosa ustaarabu kuliko wote, Watindinga na Wahadzabe na wote wenye kufanana nao watakuwa hawana maana kabisa.

Vipi mwanaume akivaa bukta fupi huyu nae anaenda kulipa fine? Akiwa anapiga kazi zake huko juani shati kaliweka kiunoni anatembea kifua wazi, hapa vipi, anakuwa kamomonyoa maadili ya kijiji kizima?

Kijana akiwa kijiweni bila shughuli ya kufanya nayo fine, kwa soko gani la ajira la kuzuia vijana kuranda hovyo? Waziri Dkt. Gwajima D kuwa serious bwana, badala ya kuunga mkono hili ilitakiwa kutafuta njia ya kumaliza mzizi wa tatizo.

Vijana wanajiingiza kwenye wizi, badala ya kuweka sheria ambazo hazina maana uundwe mradi wa kuwaghulisha au wapewe ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuishia kwenye uhalifu. Wewe ni mmoja wa watu smart sana serikalini usifanye vitu vya kijinga kama hivi vikaharibu CV yako.
 
Mie naona wapo sahihi... na wanatakiwa waigwe.

Kuna vizazi vya watu wajinga wajinga sana wanakuja kutusumbua mitaani.
Kwamba mtu akinyoa kiduku basi maadili yameporomoka, halafu ukikutana na mmasai mwanaume kasuka na mapambo ya shanga utamtetea aendele na hilo sababu ni utamaduni/asili? Nguo fupi, mitindo ya nywele haijawahi kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili.

Hakuna watu smart wenye wanaovaa vizuri lakini ukifatilia wameoza kitabia?
 
Habari za mchana.

Kwanza ahsante kwa kufuatilia habari za jamii.

Halafu, mimi ningekuwa wewe nataka kutoa ushauri kwanza ningeanza hivi;

Nashukuru Mungu sasa jamii imeanza kutambua umuhimu wa kudhibiti mmomonyoko wa maadili jambo ambalo ni kilio kikubwa na walau wanakaa na kujadili hata kama mijadala yao inaweza ikawa labda ina changamoto. Hii ni hatua moja.

Halafu ningeshauri kuwa, sasa tafadhali, wataalamu wa Maendeleo na Ustawi na wengine mbalimbali waende wakae na jamii hii wawaongoze vema Ili Nia yao nzuri isiishie njiani hasa ukizingatia kwamba yako mambo mengi ya kutazama.

Hapo mm ningeona ushauri wako mzuri sana na wewe ungekuwa pengine mwanatimu hiyo, kama mwingine aliyetoa ushauri makini kwenye ukurasa wa BASATA jana sasa tunamtumia.

Hii habari ya WAKATI WOTE kuwa NEGATIVE tu na jamii na kuibua MABAYA TU mema hapana mimi binafsi nakataa na ndiyo kinachotuzamisha sisi nchi nyingi za bara letu. Lazima tujue kupokea, kushauri na kurekebisha kwa hekima na kutia moyo wengine.

Hakuna jambo gumu kama kuifanya jamii Ione wajibu wao, hivyo wanapouona ni HATUA MOJA na wanapohitaji technical support ni HATUA INGINE.

Kwa taarifa yako, sisi kupitia uzoefu huu sasa tunapeleka maelekezo kote wakae wafanye mipango chini ya wataalamu kupitia hatua hii ya kuwa, jamii IMEONA KIU ya kufanya mabadiliko.

Hata hivyo, AHSANTE SANA kwa mchango wako. Pongezi kwao SITATENGUA ila tunaenda na wataalamu huko ili twende nao kisayansi zaidi maana hii ni safari ya mabadiliko ya fikra za jamii.

Ubarikiwe.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja aje kukujibu!
Nimeshamjibu kwa kumshukuru na kumwelimisha, sijui kama atanielewa. Hebu na wewe soma uone kama naeleweka. Maana maana sasa nitoe mfano kuwa; mtu anapoanza hatua za mabadiliko anapita historia ndefu ya kuanza kutembea na kuanguka na kusimama. Sasa kama jamii yetu ndiyo inaanza jambo ambalo sijui wapi kwingine liliwahi fanyika, halafu anatoka mtu anasema halifai, maana yake tunazimisha hatua za jamii badala ya kwenda kushirikiana nao ku adjust Nia yao njema.

Hata hivyo niliamua kupongeza nikijua kabisa wako wengine wataangalia upande mmoja hasi waje waanze kuishusha chini ile jamii huku wao wenyewe wakiwa hawafanyi Chochote kwenye jamii zao waliko.

Mtihani sana ila tutashinda kwa ujasiri.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Kwamba mtu akinyoa kiduku basi maadili yameporomoka.... halafu ukikutana na mmasai mwanaume kasuka na mapambo ya shanga utamtetea aendele na hilo sababu ni utamaduni/asili? Nguo fupi, mitindo ya nywele haijawahi kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili.

Hakuna watu smart wenye wanaovaa vizuri lakini ukifatilia wameoza kitabia?
Kwenye mavazi na vyovyote vile kwa nje hakutafsiri undani wa mtu. Nje ya mtu yaweza kuwa njema sana inavutia ila ndani yake ikawa hatari sana. Ila Kila jamii inajua kuweka diagnosis yake kwa wakati wake. Na jamii hii imeanza mjadala huo hivyo, maana yake Sasa imeona tatizo, ina kiu ya kubadilika na IMEFUNGUA MLANGO WA MAJADILIANO.

Sisi sasa, ambao tunadhani tunajua Sana, tunatakiwa kutafuta BOND nao na kuzungumza Ili kufikia kile tunachodhani kuwa, hiki sasa ni community reconciliation point. Vinginevyo hata sisi tunaodhani tunajua Sana, tuna changamoto ambazo hata huko vitani kwenye kurekebisha hayo maadili hatumo.

Ahsanteni, tuendelee kujadiliana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Anakaribishwa
Tayari nime respond hapo nikiamini ni mjadala chanya utakaochangia kusukuma jamii yetu imiliki hoja zao zenye changamoto jambo ambalo ni mtihani mkubwa duniani kumfanya binadamu amiliki hoja yake na kisha aendelee kukua kutoka hatua moja kwenda ingine hadi kufikia balance chanya.

Haya karibu maana na mimi napendaga maoni mbalimbali.
 
Asante kwa kujibu Mh, nashukuru umekubali kuwa mavazi sio kigezo kwenye kuelezea tabia wala maadili ya mtu. Badala ya kusingizia mavazi yanaharibu maadili ya watu ni vema ungetafutwa mzizi wa tatizo, lakini pia kwanini uwapangie watu jinsi ya kuvaa kama hawavunji sheria? Ukiangalia picha za wazazi wetu kuanzia mitindo ya nywele mpaka mavazi haikotofauti sana na sasa tena wao ni zaidi lakini kwani wao walikuwa ni tabia chafu kupindukia? Badala ya kukwepa majukumu tuyakabili na kung'oa mzizi huo, na sio kuwaambia watu waache kuvaa jinzi sijui kunyoa viduku.

Lakini pia Mh, kuna sehemu maalumu ambako wana mavazi maalumu mfano kwenye misikiti, kanisa, ofisi za serikali nk ambako ukivunja utaratibu wao utachukuliwa hatua stahiki, sasa mnataka hata mtaani watu wasiwe huru kuwa wanavyotaka (mradi hawavunji sheria) kwa kisingizio cha maadili? Hili sawa.
 
Hbr za siku tele.

Narudia kusema kuwa, nilichopongeza ni jamii kumiliki ajenda. Kila siku tunasema kuwa community participation and ownership. Ndiyo hii sasa. Kama wamemiliki, hii ni hatua ya kwanza nzuri kabisa kama wanavyomiliki ajenda za kujenga shule, zahanati, kuchonga barabara nk. Mbona wanapomiliki wanaanza wanakosea wanarekebishwa wanaenda mbele? Hivyo hivyo, hata kwenye ajenda za jamii tuwapongeze kwa kumiliki na tuwafuatilie tuwape semina na kuwajengea uwezo Wamiliki vzr kwa tija. Sasa mkiona pongezi zimetolewa wengi mnaona negativity tu kuliko positivity. Je uta bond vipi na jamii for change ikiwa tunayaona mabaya tu pasipo mema?

Mm nawapongeza kwa kumiliki ajenda hii na ndiyo mwanzo wa safari ya mabadiliko chanya kwa msaada wa maafisa wa Maendeleo na Ustawi walioko huko.

Ahsante sana, kwa maoni tuendelee na kuelimishana....

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Kwamba mtu akinyoa kiduku basi maadili yameporomoka.... halafu ukikutana na mmasai mwanaume kasuka na mapambo ya shanga utamtetea aendele na hilo sababu ni utamaduni/asili? Nguo fupi, mitindo ya nywele haijawahi kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili.

Hakuna watu smart wenye wanaovaa vizuri lakini ukifatilia wameoza kitabia?
Ukitaka kulipima jambo lolote kama ni baya au zuri lipime Kwa watu unao wapenda mfano unajisikiaje baba Yako au mama Yako wakinyoa viduku? Vipi mama yako au dada Yako akitembea uchi?
 
Ukitaka kulipima jambo lolote kama ni baya au zuri lipime Kwa watu unao wapenda mfano unajisikiaje baba Yako au mama Yako wakinyoa viduku? Vipi mama yako au dada Yako akitembea uchi?
Naona tunachanganya kati ya kutembea uchi na mtu kuvaa nguo fupi ambayo wala haikuthiri wewe kwa lolote. Si kosa mtu kuvaa nguo fupi imani na jinsi unavyoona/kuangalia vitu ndio inakufanya utake watu wawe kwa namna fulani ambayo wewe haikupendezi.

Tatizo si nguo fupi wala kiduku, ni mambo uliyohusanisha na viduku pamoja na nguo fupi. Baba, mama, dada kunyoa kiduku au kuwa na nguo fupi wala hainipi shida, imekuwa hivyo toka enzi, wala si maajabu kuwa wameleta kitu kibaya chenye kuharibu uhai na maisha ya watu...kuna mambo mabaya ya kupiga vita viduku na nguo fupi si kati yao.
 
Hbr za siku tele.

Narudia kusema kuwa, nilichopongeza ni jamii kumiliki ajenda. Kila siku tunasema kuwa community participation and ownership. Ndiyo hii sasa. Kama wamemiliki, hii ni hatua ya kwanza nzuri kabisa kama wanavyomiliki ajenda za kujenga shule, zahanati, kuchonga barabara nk. Mbona wanapomiliki wanaanza wanakosea wanarekebishwa wanaenda mbele? Hivyo hivyo, hata kwenye ajenda za jamii tuwapongeze kwa kumiliki na tuwafuatilie tuwape semina na kuwajengea uwezo Wamiliki vzr kwa tija. Sasa mkiona pongezi zimetolewa wengi mnaona negativity tu kuliko positivity. Je uta bond vipi na jamii for change ikiwa tunayaona mabaya tu pasipo mema?

Mm nawapongeza kwa kumiliki ajenda hii na ndiyo mwanzo wa safari ya mabadiliko chanya kwa msaada wa maafisa wa Maendeleo na Ustawi walioko huko.

Ahsante Sana .. kwa maoni .. tuendelee na kuelimishana....

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Salama kabisa Mh,

Kwahivyo umepongeza wamiliki ili usubiri wafanye makosa ili warekebishwe? Kama jambo linaonekana si zuri si bora lingekemewa kutoka mwanzo? Kwenye mambo mazuri tutapongeza na mnapokosea tutasema pia, hii haikuwa good move, kidogo kidogo tutaenda kwenye ukabila, ukanda, watu fulani kuwa hivi, wengine kufata taratibu zile mwisho wa siku kutakuwa hakuna pa kurekebisha kabisa
 
Ulienda shule kusomea ujinga ndio sababu unaelimishwa unashupaza fuvu. Unashikilia kuvaa kimini badala ya kuangalia mzizi wa sheria za watu wa arumeru.
 
Tayari nime respond hapo nikiamini ni mjadala chanya utakaochangia kusukuma jamii yetu imiliki hoja zao zenye changamoto jambo ambalo ni mtihani mkubwa duniani kumfanya binadamu amiliki hoja yake na kisha aendelee kukua kutoka hatua moja kwenda ingine hadi kufikia balance chanya.

Haya karibu maana na mimi napendaga maoni mbalimbali.
Jukwaa likiwa hivi inapendeza sana mada za kujenga na kukuza fikira za watu.
 
Salama kabisa Mh,

Kwahivyo umepongeza wamiliki ili usubiri wafanye makosa ili warekebishwe? Kama jambo linaonekana si zuri si bora lingekemewa kutoka mwanzo? Kwenye mambo mazuri tutapongeza na mnapokosea tutasema pia, hii haikuwa good move, kidogo kidogo tutaenda kwenye ukabila, ukanda, watu fulani kuwa hivi, wengine kufata taratibu zile mwisho wa siku kutakuwa hakuna pa kurekebisha kabisa
Hamia Marekani. Acha kubishabisha kipuuzi. Mheshimiwa waziri kwenye uzi mmoja kajitahidi kufafanua ila wewe umeng'ang'ania kubisha. Pumbavu sana. Nadhani mimi utanielewa kwasababu kistaarabu huelewi.
 
Nimpongeze Mheshimiwa waziri kwa majibu mazuri na elimishi.

Kwa upande wangu, mporomoko wa maadili unaanzia kwenye uvaaji; akina dada nguo za kubana, vimini, mipasuo (inayoacha nje sehemu kubwa ya mapaja) na suruali(jeans) zenye chane na kwa kina kaka kuvaa mlegezo.

Uvaaji huo unaweza kupelekea msisimko wa mwili hivyo kuvuta hisia na kuhamisha akili ya mtu mwingine na kumletea mawazo hasi. Mitindo ya nywele sina tatizo nayo kwani sidhani kama ina athari zozote. Hivyo basi, jamii ielimishwe katika eneo hilo la uvaaji wa mitindo sisimuzi.

Kuhusu kukaa bila kazi nyakati za mchana, nina imani kila mtu ana kwao/ kwake eneo anapoishi. Na kuna viongozi wa mitaa, basi hao viongozi wahakikishe wanajua shughuli za kila mtu anayeishi eneo lake na sheria ndogo za kudhibiti vitendo viovu (pengine vya kuiga mitandaoni) zinatungwa na kusimamiwa ipasavyo.

Kwa sheria na adhabu nilizoziona kwenye hiyo jamii, Vijana wanaweza kutoroka taratibu na kulowea ktk miji isiyo na hizo sheria hasa miji mikubwa ambako wanaweza kuharibika zaidi.
 
Back
Top Bottom