Taarifa ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum kwa Jamii Kuzingatia Sheria ya Mtoto kudhibiti Mmomonyoko wa Maadili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, leo Septemba 12, 2023 amezungumzia wajibu wa familia na jamii kwenye kudhibiti mmomonyoko wa maadili dhidi ya watoto kupitia Sheria ya Moto, Sura ya 13 mahsusi kifungu cha 158 cha Katazo la Jumla.

Dkt. Gwajima amesema kumekuwa na matukio ya uvunjaji wa sheria ya moto ambayo wizara imekuwa ikichukua hatua mbalimbali.

Hivi karibuni pia, imeonekana video fupi ikizunguka mitandaoni inayoonesha watoto wawili wa kike wakiwa wanashiriki kwenye shughuli ya maonesho katika harusi wakicheza wimbo usio na maudhui mazuri na staili isiyo na maadili kwa watoto wa umri wao kinyume na kifungu cha 158(1)(b) cha Sheria ya Moto na nuku kifungu hicho "No person shall- use a child in a wedding show, fashion show or any other similar shows performed during the night"

Pia, imeibuka tabia ya baadhi ya familia na wanajamii kuwatumia watoto kwenye shughuli za maonesho ya harusi, maonesho ya mitindo au maonesho mengine yoyote yanayofanana na hayo katika maeneo yasiyoruhusiwa hasa nyakati za usiku kinyume na kifungu hicho cha 158(b) cha Sheria ya Mtoto.

Matukio hayo kwa kiwango kikubwa huongozwa na washereheshaji kwa jina maarufu ma MC wakishirikiana na waongoza muziki maarufu kwa Ma DJ. Ni dhahiri kuwa kwenye shughuli za namna hiyo, waongozaji pamoja na wasimamizi wa watoto kwenye shughuli hizo hawazingatii takwa la kisheria la kutowaruhusu watoto kushiriki katika shughuli hizo nyakati za usiku wala kulinda maadili ya kitanzania kwa watoto.

Hali hii haikubaliki. Ikumbukwe, hata nyakati za mchana, haistahili kumweka mtoto kwenye mazingira yasiyo rafiki kwa ustawi wake.

Ameyakumbusha makundi yote katika jamii kuzingatia malezi na makuzi ya watoto kwa mujibu wa Sheria ya Moto na Sheria nyingine za nchi. Sheria ya Mtoto iko kwenye m a n d a o vema jamii ijishughulishe kuisoma, kuielewa na kuitekeleza.

Aidha, ameelekeza yafuatayo;
  1. Maafisa Ustawi wa Jami a Maafisa Maendeleo ya Jami katika ngazi za Mikoa na Halmashauri kwa kushirikiana na Wadau a Maendeleo na vyombo vya habari, polisi jamii na madawati ya jinsia ya wanawake na watoto ya jeshi la polisi kutekeleza mpango wa elimu kwa jami kuhusu Sheria ya Mtoto.
  2. Sambamba na elimu kwa jamii, naelekeza Maafisa Ustawi wa Jami na Maafisa Maendeleo ya Jami katika ngazi za Mikoa na Halmashauri wekeni mpango wa ufuatiliaji kuhakikisha kuwa hakuna Mwongoza Sherehe (MC) au Mwongoza Burudani ya Muziki (DJ) kwenye tukio lolote anayevunja Sheria ya Mtoto na Sheria nyingine za nchi;
  3. Wasanii wa Sanaa za aina zote kuanzia filamu, muziki wa aina mbalimbali nawakumbusha kuandaa maudhui ya kazi zenu yenye kulinda maadili na kuzingatia Sheria zinazomlinda Mtoto. Vilevile, watumiaji wa mitandao ya kijamii ya aina zote lindeni maadili na kutekeleza Sheria ya Moto;
  4. Naelekeza familia na jamii kwa ujumla kuhakikisha kwamba watoto wanalelewa na kukuzwa kwa kuzingatia Sheria zinazowalinda watoto na Sheria nyingine za chi ili watoto wake wakiwa salama na wenye maadili mema.
  5. Mtu yoyote atakayeona matendo yanayofanywa kwa watoto yanayovunja Sheria ya Mtoto na Sheria nyingine za chi, atoe taarifa kwenye Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi au apige simu bila malipo kwa namba 116 inayopatikana masaa 24 kila siku. Vilevile, kwa masaa ya kazi za ofisi kuna simu ya Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Wizara yetu namba 0734 986503 au 026 2160250.
Endapo kutakuwa na haja ya rufaa kwamba, labda kumekuwa na changamoto kwenye huduma hizo, tuma ujumbe kwake Waziri mwenye dhamana ya watoto kwenye namba 0765 345777 na kopi 0734 124191. Tunahitaji kutumia kila aina ya ubunifu katika kuwalinda watoto wetu.

IMG_8473.jpeg
IMG_8474.jpeg
IMG_8475.jpeg
IMG_8476.jpeg
 
Amesubiri mpaka Rais jana akumbushe wajibu wa Wizara hii ndiyo atoe tamko? Anyways, ndiyo baadhi ya viongozi wetu walivyo. Imenikumbisha enzi za kujifukizia.
 
Amesubiri mpaka Rais jana akumbushe wajibu wa Wizara hii ndiyo atoe tamko? Anyways, ndiyo baadhi ya viongozi wetu walivyo. Imenikumbisha enzi za kujifukizia.

Ulitaka Rais asikumbushe?
Ni Waziri gani unayemjua kwenye nchi Hii ambaye anawajibika kujibu hoja za wananchi hata humu JF zaidi ya huyo unayesema Kakumbushwa?

Je ni kosa kukumbushwa?
 
Hata tamko letu ukilisoma ndani utaona limesema kama ulichosema. Aya ya pili nadhani. Ahsante Sana kwa kufuatilia taarifa zetu, ubarikiwe, wahamasishe na wengine
Wanaoongoza haribu watoto ni wasanii na redio na TV. Nyimbo zao ni hatari sana kwa watoto. Embu imagine mtoto anaimba nyimbo za Diamond au Zuchu au sijui nani? Na hizi nyimbo zinapigwa kwenye mabaa yaliyojaa mitaani kwa sauti juu hata mzazi ukijitahidi mtoto asiyasikilize au kuyaangalia hayo manyimbo nyumbani, mtaani ni shida. TV na redio ni shida. Liangalieni hili. Wekeni usimamizi mzuri wa maudhui katika radio na TVs. La sivyo tunajidanganya na tutakuwa tunawaonea watoto bure.
 
Amesubiri mpaka Rais jana akumbushe wajibu wa Wizara hii ndiyo atoe tamko? Anyways, ndiyo baadhi ya viongozi wetu walivyo. Imenikumbisha enzi za kujifukizia.
Ni vizuri pia kufahamu kuwa kumbe na ww chanzo chako cha taarifa zetu ni hapa tu. Uwe basi unatembelea na kurasa za wizara na hata mm Instagram, FB, Twitter, TikTok. Lakini pia jiunge basi na mtandao wa SMAUJATA pita hapo page yao Instagram kisha urejee twende sawa. Nashukuru kupata fursa ya kutangaza na mitandao yetu kupitia hoja yako. Ubarikiwe
 
Amesubiri mpaka Rais jana akumbushe wajibu wa Wizara hii ndiyo atoe tamko? Anyways, ndiyo baadhi ya viongozi wetu walivyo. Imenikumbisha enzi za kujifukizia.
Juzi hapa alitoa taarifa kuhusu hili suala humu JF even before rais hajatoa tamko.
Humu jukwaani anajitahidi sana, na pia anajibu hoja kwA wakati.
Aendelee kukomaa, muhim asikimbie jukwaa huko mbeleni kama ma-diluu
 
Juzi hapa alitoa taarifa kuhusu hili suala humu JF even before rais hajatoa tamko.
Humu jukwaani anajitahidi sana, na pia anajibu hoja kwA wakati.
Aendelee kukomaa, muhim asikimbie jukwaa huko mbeleni kama ma-diluu
pigeni tu mishale yote mm nipo pamoja nanyi hadi ukamilifu wa kazi niliyopewa. Ili mradi na maandiko yangu na nyie myasome na mtoe maoni, maana nikikimbia saiti yangu naenda wapi Sasa wakati hao ndiyo nawahitaji. Ila nimecheka kwa sauti.
 
Back
Top Bottom