Waziri Bashe acha kuchezea Kodi zetu kwa maono mfu! Kilimo siyo filamu

Tatizo ni Soko na watu hawana buying power;

Lakini what do ? Increase cost of Production;
Thus, unless watalima premium products ambazo watauza kwa premium prices otherwise tunaweza kufanya maigizo ya kununua hizo bidhaa ili tuonekane tumefanikiwa...

Anyway am all about sustainability ila tungewekeza zaidi kwenye kutafuta masoko kwa wale ambao wanalima sasa na hakuna masoko na kama ni issue ya elimu tuwekeza kwenye taasisi zetu za elimu ya Kilimo i.e. SUA et al
 
Tanzania tatizo la kilimo ni moja tu. SOKO LA MAZAO YA WAKULIMA.
Kaka Allen, soko la mazao sio tatizo kabisa, tatizo ni "QQC" (quality, quantity and consistence ya mazao yetu). Hatuzalishi mazao katika ubora na wingi unaowezesha economies of scale itokee na mwendelezo wa hicho kinachozalishwa na hivyo kutoa nafasi ya kutwaa soko la kimataifa.

Huwezi kuwalisha watu mchele kwa msimu. Ima uzalishe mara 3-4 kwa msimu au uzalishe kwa msimu mmoja lakini kwa kiwango kikubwa chenye kutosheleza mahitaji ya mwaka mzima. Program ya BBT ni best program ever katika nchi yetu as long uzalishaji ukifanyika bila kutegeme mvua na kwa wingi kukidhi mahitaji ya containers (sio gunia).
 
Hivi hawa waliokusanywa kama kumbi kumbi wamepatikana tokea wapi, na hiyo programme inahusisha kilio cha Mazao gani. Maana Sina hakika kama wakijichimbia dodoma tuu,, watonyesha mfano wa shamba lilioko Sumbawanga, kigoma, tanga Kilimanjaro na kadhalika. Huu ni wizi wa Fedha zetu na waeleweke ni wezi kama wezi wengine.
 
Kaka Allen, soko la mazao sio tatizo kabisa, tatizo ni "QQC" (quality, quantity and consistence ya mazao yetu).
Unapozungumzia "Quality" hapo unazungumzia Soko!!

Unapozungumzia "Quantity" hapo unazungumzia Soko!!

Na unapozungumzia "Consistence" Pia unazungumzia Soko.

Hebu tulijadili kidogo.

Unapozungumzia Ubora wa mazao moja kwa moja unazungumzia kupeleka mazao hayo kwa mteja ama kuyashindanisha na ya mwengine sokoni yakiwa na ubora unaotakiwa. Sidhani unazungumzia ubora kwa ajil ya mazao ya kutumia kwenye familia.

Tukija kwenye suala la wingi nalo ni vile vile. Inawezekana kabisa kuna hisia kwamba Tanzania tunazalisha mazao yasiyo na ubora na machache yasiyotosheleza soko. Kwa ivo unaposema tatizo la Kilimo chetu ni uchache wa mazao tunayozalisha upo sahihi, lakini hapo bado unazungumzia soko.

Na pale unapozungumzia Muendelezo, ni kwamba umeunganisha mambo mawili ya mwanzo, yaani Ubora na wingi na kuyaweka yawe ni kitu cha kudumu. Unapozungumzia uendelevu bado pia unazungumzia Soko. Yaani kitu kinachouzwa leo kiuzwe kesho kikiwa na ubora na wingi ule ule.

Sasa hapo ndiyo ujue hayo matatizo ya kutokuwa na "Quality, Quantity, Consistence" ndiyo mkulima anayosumbuliwa nayo hatimaye mazao yake yanakosa soko.

Lakini kwa Tanzania hizo zinazoitwa "Program" huwa zimejaa nadharia zaidi kuliko uhalisia na wala huwa siyo suluhu kudumu kwa matatizo yetu kwenye Kilimo. Hao waliomo kwenye hiyo BBT ni wakulima maskini waliotolewa vijijini ama ni vijana wapya wa kisiasa wanaopelekwa kutumia hizo fedha kwenye jaribio la kilimo lisilo la kisayansi??
 
Ni mara ngapi tumeona clip na picha zikionesha wakulima wakilia kwa kukosa masoko ya mazao yao.

*Tushaona nyanya zinauzwa debe sh 500/= na parachichi zikioza huko Iringa.
*Tushaona mahindi yakioza huko Songea na Katavi.
*Tushaona wakulima wa korosho wakiuza korosho kwa bei ya hasara ama kugomea masoko huko Mtwara.
*Tushaona wakulima wakikata mibuni na michai kwa bei mbaya ya mazao hayo.

Kilimo kimeshindwa kuvutia vijana kwasabb 2 tu.
1. Kukosekana kwa masoko ya uhakika ya kumfanya mkulima apate faida (sababu kubwa zaidi hii)
2. Upatikqnaji wa uhakika wa pembejeo na viwatilifu.

Kama wakulima wangekuwa wanapata faida hakuna kijana angekuwa bodaboda, machinga ama mamantilie. Wote wangejikita kwenye kilimo. Shughuli yoyote ya kiuchumi yenye faida huvutia watu.

Kwahiyo siyo kwamba vijana hawataki kilimo kwasbb ya ukosefu wa mitaji....NO.

Nani alitoa mafunzo na mitaji kwa bodaboda, mamantilie na machinga waliozagaa nchi nzima?

Wasomi wa SUA waliomaliza miaka dahali pamoja na maprofesa wao mbana hatuoni wakitumia utaalamu wao kuendesha mashamba makubwa??

Bashe ktk hili unatapanaya tu hela zetu za Kodi lkn zoezi la BBT halitafanikiwa wala halitakuwa endelevu. Kilimo hakiendeshwi hivyo.

Kazi ya serikali kupitia wizara ya kilimo iwe ni kujenga mifumo itakayoifanya shughuli ya kilimo kwenda sawa na kuvutia watu wengi zaidi.

NIMEMALIZA.
Sikia walioandaa andiko la BBT project!
 
Kaka Allen, soko la mazao sio tatizo kabisa, tatizo ni "QQC" (quality, quantity and consistence ya mazao yetu). Hatuzalishi mazao katika ubora na wingi unaowezesha economies of scale itokee na mwendelezo wa hicho kinachozalishwa na hivyo kutoa nafasi ya kutwaa soko la kimataifa. Huwezi kuwalisha watu mchele kwa msimu. Ima uzalishe mara 3-4 kwa msimu au uzalishe kwa msimu mmoja lakini kwa kiwango kikubwa chenye kutosheleza mahitaji ya mwaka mzima. Program ya BBT ni best program ever katika nchi yetu as long uzalishaji ukifanyika bila kutegeme mvua na kwa wingi kukidhi mahitaji ya containers (sio gunia).
Mwandishi wa andiko ktk ubora wako. Sasa kwann wizara isiweke nguvu ktk kuondoa hizo changamoto kwa wakulima badala yake inaanzisha BBT?
 
Unapozungumzia "Quality" hapo unazungumzia Soko!!

Unapozungumzia "Quantity" hapo unazungumzia Soko!!

Na unapozungumzia "Consistence" Pia unazungumzia Soko.

Hebu tulijadili kidogo.

Unapozungumzia Ubora wa mazao moja kwa moja unazungumzia kupeleka mazao hayo kwa mteja ama kuyashindanisha na ya mwengine sokoni yakiwa na ubora unaotakiwa. Sidhani unazungumzia ubora kwa ajil ya mazao ya kutumia kwenye familia.

Tukija kwenye suala la wingi nalo ni vile vile. Inawezekana kabisa kuna hisia kwamba Tanzania tunazalisha mazao yasiyo na ubora na machache yasiyotosheleza soko. Kwa ivo unaposema tatizo la Kilimo chetu ni uchache wa mazao tunayozalisha upo sahihi, lakini hapo bado unazungumzia soko.

Na pale unapozungumzia Muendelezo, ni kwamba umeunganisha mambo mawili ya mwanzo, yaani Ubora na wingi na kuyaweka yawe ni kitu cha kudumu. Unapozungumzia uendelevu bado pia unazungumzia Soko. Yaani kutu kinachouzwa leo kiuzwe kesho kikiwa na ubora na wingi ule ule.

Sasa hapo ndiyo ujue hayo matatizo ya kutokuwa na "Quality, Quantity, Consistence" ndiyo mkulima anayosumbuliwa nayo hatimaye mazao yake yanakosa soko.

Lakini kwa Tanzania hizo zinazoitwa "Program" huwa zimejaa nadharia zaidi kuliko uhalisia na wala huwa siyo suluhu kudumu kwa matatizo yetu kwenye Kilimo. Hao waliomo kwenye hiyo BBT ni wakulima maskini waliotolewa vijijini ama ni vijana wapya wa kisiasa wanaopelekwa kutumia hizo fedha kwenye jaribio la kilimo lisilo la kisayansi??
Bonge moja la hoja. Kongole mkuu
 
Yaani "Buying power" ndiyo huamua soko. Unaposema "SOKO" ni neno linalobeba mkurulo mzima wa biashara ya mazao na kurudi kinyume nyume mpaka kwa mzalishaji!!
Watu wanaweza wakawa wana uwezo wa kununua lakini unauza makapi no one wants it; au wanaweza wakawa wanataka hio product yako lakini uwezo wa kununua hakuna.....

Kila mtu anatamani kula Korosho ila mfukoni pesa hawana kwahio mtu kula korosho lazima awe na disposable income..., and since pesa iliyopo ni ndogo kwahio watu wanaweka kwa ajili ya necessities ikiwemo chakula cha kila siku ingawa wanatamani kula mara tatu lakini they have to settle for a single meal....

In short people can have buying power and still your product struggle to find market....
 
Tanzania tatizo la kilimo ni moja tu. SOKO LA MAZAO YA WAKULIMA.
Kabisa kabisa! Wakulima wanalazimika kuwauzia walanguzi huko mashambani kwa bei yeyote ile ndogo kwa sababu wanaogopa kuyapeleka sokoni kwa kuwa huko ndio kuna usumbufu mkubwa sana kwa madalali na hata mazao yanaweza yakaharibika akijifanya mjuaji !! Ni kweli shida kubwa ni masoko ambayo hayatakuwa na janja janja za kumpunja mkulima !
 
Back
Top Bottom