Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 5,755
- 15,238
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amepatwa na nini? Mbona Bashe wa kabla ya kuteuliwa kuwa waziri alikuwa machachari sana kuliko huyu wa sasa? Mazao yote makubwa chini yake yameanguka bei ,pamba, korosha hali ni mbaya.
Kwenye tumbaku wakulima hawajalipwa hadi leo!!! Kila siku ni ahadi na ngonjera zisizo isha kabisa. Bashe wa leo yuko bize kutetea wafanyabiashara tu ambao ni matajiri tayari na hata asipowatetea hawawezi kufa na njaa, na kuacha wananchi masikini ambao usipowatetea wanatembea bila viatu.
Kitu ambacho hakijui Rais Samia au anakijua lakini ameamua kukaa kimya ni mawaziri wake kugeuka wafanyabiashara wakubwa sana. Ukiona mafuta yameadimika sababu kubwa ni kwamba viongozi wa hiyo wizara ndiyo wamiliki wa vituo vya mafuta kwa hiyo hata yakifichwa ili yapande bei hawaoni shida, pia ukiona mazao ya kilimo hayapandi bei ujue wanunuzi wakubwa wa hayo mazao ni haohao mawaziri wa rais Samia!.
Viongozi sehemu ambazo wao ni wauzaji bei zinapanda balaa eg mafuta, ila sehemu ambazo viongozi ni wanunuzi bei zinashuka kwa kasi au kudumaa palepale, eg korosho na pamba!!