Hongera Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwa kutetea soko la wakulima, wanaokupinga ni wanafiki

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Dec 13, 2019
1,006
1,171
Wakuu nampongeza mh Bashe waziri wa kilimo kwa mengi aliyoyafanya kilimo, isipokuwa Kwa Leo nampongeza kwa msimamo wake wa kutetea wakulima juu kuuza mazao Yao waliyolima kwa gharama zao kuuza kwenye soko lolote Le ye tija kwao ndani na nje ya nchi.

Wakuu, lazima tutambue kwamba kwa sasa kilimo ni biashara na ni kiwanda ambacho kinahitaji gharama kubwa sana za uendeshaji pia kina kuwa na risk kubwa sana ya kupata hasara kwenye mchakato wake so ukimpa mkulima tena risk ya kupata soko unammaliza na kuua kilimo ambayo ni back bone ya uchumi wetu.

Kwa hiyo naona sera mh Bashe inaenda kuinua sekta ya kilimo ambayo ni Uti wa mgongo wa uchumi wa taifa hili, kwa sababu wakulima wana uhakika wa soko.

Pili Inakadiriwa sekta ya kilimo imeajiri zaidi ya watanzania asilimia sitini , Kwa hiyo watanzania asilimia sitini wamehakikishiwa uhakika wa ajira zao Tatu inaweza kuongeza mapato ya nje kwa sababu watanani wengi wenye akili hawataishia kulalamika ila wataona hiyo fursa na kwenda kuzalisha Kwa wingi ili kuuza kwa nje
Kwa uchache sana hizo ni faida za sera kilimo za Mh Bashe.

Wajinga ni wale ambao hawajui faida za hiyo sera wamebaki na fikra za kilimo cha miaka ya sabini. Wanafiki ni wale wanaotambua hizo faida ila wanapindisha ukwell kwa maslahi yao Wakiwemo baadhi ya wabunge waropokaji wasiopenda kupima ukweli wa mambo, mmoja nimemsikia nikashangaa sana.
 
Kama tusipokuwa na sera za kisasa za kilimo tutaendelea kufanya wakulima ambao ndio kubwa kuwa maskini
Na hatimaye kuendelea kuwa taifa maskini. Naamini kama taifa tukiweza kuwekeza kwenye kilimo kwa kuongeza uzalishaji kwenye killmo tunaweza kutoka kabisa kwenye umaskini.
 
Leo nampongeza kwa msimamo wake wa kutetea wakulima juu kuuza mazao Yao waliyolima kwa gharama zao kuuza kwenye soko lolote Le ye tija kwao ndani na nje ya nchi.
Sasa sisi consumers tonao-feel the pinch ya hilo soko huria nani anatutetea?

Kama hiyo ndiyo sera nzuri, basi na sisi consumers turuhusiwe kununua mazao toka soko huria duniani bila vikwazo. Wapo wafanyabiashara wanaoweza kuagiza vyakula na vitu vingine toka nje na kuviuza kwa bei nafuu zaidi hapa nchini, waruhusiwe kuagiza hizo bidhaa bila kuangalia wakulima wa ndani wataathiriwa namna gani.

Ule wakati wa kulinda wakulima wa ndani uishe, tuone nani ataumia zaidi! Honestly saying, hiyo siyo sera nzuri hata kidogo!
 
Anatetea wakulima au anatetea madalali?
Km hujawahi kua mkulima huwezi elewa kwa upana haya mambo.
Kwa mfumo wetu wa biashara wa sasa ,
Kuna product chain of supply,

Hii huwezi kuikwepa kirahisi kutoka Kwa mzalishaji mnunuzi wa jumla ,msafirishaji ,store muuzaji wa rejareja then mlaji. Hizo zote zinahitaji kugharama.

Hakuna namna mkulima ataweza kupeleka Moja kwa Moja kwa mlaji bila hiyo chain, either amue mwenyewe kutumia hizo gharama.

Kinachoathiri bei za hao wote mpaka kwa mkulima ni soko zuri I mean bei nzuri ya mazao. Soko linapokuwa baya linathiri chain nzima mpaka kwa mzalishaji /mkulima.
 
Sasa sisi consumers tonao-feel the pinch ya hilo soko huria nani anatutetea?
Kama hiyo ndiyo sera nzuri, basi na sisi consumers turuhusiwe kununua mazao toka soko huria duniani bila vikwazo. Wapo wafanyabiashara...
Kama tutaanza kuangalia pain kwa mlaji bila kuangalia mzalishaji,
Tutakuwa hatujatumia akili zetu vizuri , Cha kwanza ni mzalishaji alindwe na atengenezewa mazingira ya kuendelea kuzalisha kwa wingi na kwa faida nzuri ili kumuongezea motisha ili kuhakikisha costastant supply.

Kumbuka sera nzuri ni ile inayobeba watu wengi na kumbuka asilimia sitini ni wakulima, ambao kwa wakati mmoja ni wazalishaji na walaji pia.

Kila taifa linaangalia uzalendo kwanza, tunaangalia sera ipi yenye manufaaa Kwa majority sio minority, ingawa minority nao wanaweza kutafutiwa unafuu pia lakini sio kuumiza majority.
 
Mazao kama pamba,kahawa,korosho na yenyewe Bashe atasimama kidete wakulima wauze wanapotaka?.

kahawa ya Bukoba wakulima walikua wakizuiwa wasipeleke Uganda,hivyohivyo na korosho pia ilikua inazuiwa isiuzwe nchi za jirani.
Hii nalo linaweza kufanyiwa kazi endapo litakuwa na maslahi makubwa kwa wazalishaji/wakulima,
Ingawa mada inagusa zaidi mazao ya chakula
 
Jambo zuri lakini tatizo anayoongea yatabaki kuwa kauli tuu, akija waziri mwingine naye atalipuka na sera zake na hata kuzuia wakulima wasiuze nje mazao yao, apigane alete muswada upitishwe bungeni ili anayoongea ndio yawe sera na sheria za kumwongoza mkulima, tuache blah blah kama mambo muhimu Bashe anajua cha kufanya sio kauli za majukwaani tu.
 
Jambo zuri lakini tatizo anayoongea yatabaki kuwa kauli tuu, akija waziri mwingine naye atalipuka na sera zake na hata kuzuia wakulima wasiuze nje mazao yao, apigane alete muswada upitishwe bungeni ili anayoongea ndio yawe sera na sheria za kumwongoza mkulima, tuache blah blah kama mambo muhimu Bashe anajua cha kufanya sio kauli za majukwaani tuu
Nashukuru mkuu, ni kweli Kuna umuhimu wa kutanga Sheria ya kulinda mazao soko huru la wakulima,
Waziri atakayetaka anunue mazao kwa Bei ya sokoni auzie walaji kwa bei anayotaka, sio kukandamiza wakulima
 
Lazima kuwa makini hapa, kuna maslahi ya watu wengi katika swala zima la kilimo, kuna mkulima (faida), mtumiaji (bei nzuri anayomudu au ya chini kabisa), wafanyabiashara waagizaji(faida) na serikali (kodi na utulivu wa nchi), mimi naona free market iachwe ifanye kazi yake bila serikali kuingilia.

Theoretically unaweza kusema au kufikiria tukiachia waagizaji waingize wanavyotaka tutaua wakulima au tukizuia wakulima wasiuze nje bei za ndani zitashuka, au serikali ikipiga kodi za juu waagizaji itasaidia wakulima wa ndani, ukweli ni kwamba huwezi control markets.

Dawa ni kuachia watu wafanye kazi zao 100% free bila kuingiliwa, acha soko liamue mshindi, kama mchele wa nje baada ya cost zote, kodi na faida ya mwagizaji ni rahisi kuliko mchele wa mkulima tuache mshindi awe mwagizaji na mtumiaji, na kama ni vice versa basi tuache mkulima na mtumiaji wawe washindi, mara nyingi kwenye free market mshindi ni mtumiaji na ndio nia kubwa......is a dog eat dog World
 
Hamna serikali imewahi kutoboa wakati wananchi wake wana njaa. Soon, tutajua kama hizo bei tunaweza kuzihimili au la.
 
Wakuu nampongeza mh Bashe waziri wa kilimo kwa mengi aliyoyafanya kilimo, isipokuwa Kwa Leo nampongeza kwa msimamo wake wa kutetea wakulima juu kuuza mazao Yao waliyolima kwa gharama zao kuuza kwenye soko lolote Le ye tija kwao ndani na nje ya nchi.

Wakuu, lazima tutambue kwamba kwa sasa kilimo ni biashara na ni kiwanda ambacho kinahitaji gharama kubwa sana za uendeshaji pia kina kuwa na risk kubwa sana ya kupata hasara kwenye mchakato wake so ukimpa mkulima tena risk ya kupata soko unammaliza na kuua kilimo ambayo ni back bone ya uchumi wetu.

Kwa hiyo naona sera mh Bashe inaenda kuinua sekta ya kilimo ambayo ni Uti wa mgongo wa uchumi wa taifa hili, kwa sababu wakulima wana uhakika wa soko.

Pili Inakadiriwa sekta ya kilimo imeajiri zaidi ya watanzania asilimia sitini , Kwa hiyo watanzania asilimia sitini wamehakikishiwa uhakika wa ajira zao Tatu inaweza kuongeza mapato ya nje kwa sababu watanani wengi wenye akili hawataishia kulalamika ila wataona hiyo fursa na kwenda kuzalisha Kwa wingi ili kuuza kwa nje
Kwa uchache sana hizo ni faida za sera kilimo za Mh Bashe.

Wajinga ni wale ambao hawajui faida za hiyo sera wamebaki na fikra za kilimo cha miaka ya sabini. Wanafiki ni wale wanaotambua hizo faida ila wanapindisha ukwell kwa maslahi yao Wakiwemo baadhi ya wabunge waropokaji wasiopenda kupima ukweli wa mambo, mmoja nimemsikia nikashangaa sana.
Huu ni ujinga unaokaribia upumbavu.

Ni "kiwanda" gani ambacho serikali haihusiki nacho kwa njia moja au nyingine!

Ni shughuli ipi yoyote inayofanywa ndani ya taifa lolote serikali isihusike na shughuli hiyo.

Ni mkulima gani mwenye uwezo wa kusimamia uuzaji wa mazao yake popote duniani bila ya ushiriki wa serikali kwa njia moja au nyingine?
Walanguzi wa mazao ya wakulima leo Bashe anawavisha jina la wakulima?

Bashe anatafuta sifa za kijinga kwa wajinga kama nyinyi.
 
Lazima kuwa makini hapa, kuna maslahi ya watu wengi katika swala zima la kilimo, kuna mkulima (faida), mtumiaji (bei nzuri anayomudu au ya chini kabisa), wafanyabiashara waagizaji(faida) na serikali (kodi na utulivu wa nchi), mimi naona free market iachwe ifanye kazi yake bila serikali kuingilia, theoretically unaweza kusema au kufikiria tukiachia waagizaji waingize wanavyotaka tutaua wakulima au tukizuia wakulima wasiuze nje bei za ndani zitashuka, au serikali ikipiga kodi za juu waagizaji itasaidia wakulima wa ndani, ukweli ni kwamba huwezi control markets, dawa ni kuachia watu wafanye kazi zao 100% free bila kuingiliwa, acha soko liamue mshindi, kama mchele wa nje baada ya cost zote, kodi na faida ya mwagizaji ni rahisi kuliko mchele wa mkulima tuache mshindi awe mwagizaji na mtumiaji, na kama ni vice versa basi tuache mkulima na mtumiaji wawe washindi, mara nyingi kwenye free market mshindi ni mtumiaji na ndio nia kubwa......is a dog eat dog World
Sasa Bashe mwenyewe hatambui hilo.

Kwamba kama anataka serikali ijiondoe kabisa katika maswala ya wakulima, basi serikali hiyo hiyo itapashwa ijiondoe katika nyanja zingine zinazohusu maeneo mengine yanayowahusu wananchi kwa ujula (walaji/wanunuzi).

Maana yake ni kwamba serikali isiingilie wafanya biashara wanaoingiza nfaka (mahindi) toka nje, na wao wauze kwa bei ambayo wananchi/walaji wataimudu.

Lakini hapa ni lazima ujue kwamba ikiwa kama unavyosema wewe"watu waachwe wafanye watakavyo"; maana yake huyo mkulima wa ndani hana kazi. Habari yake itakuwa ni historia.
 
Lakini hapa ni lazima ujue kwamba ikiwa kama unavyosema wewe"watu waachwe wafanye watakavyo"; maana yake huyo mkulima wa ndani hana kazi. Habari yake itakuwa ni historia.
Inawezekana mkulima akashindwa kushindana na waagizaji lakini sio lazima iwe hivyo, hata hao waagizaji wana gharama kubwa pia, mkulima akipewa masoko yote free ya ndani na nje pamoja na ruzuku lakini waagizaji wakamzidi acha ashindwe tuu, atatafuta shughuli nyingine ya kufanya au atalima mazao yanayoleta faida, free market haijawahi kumwangusha mtu na inajua kubalance kila kitu
 
Kama tutaanza kuangalia pain kwa mlaji bila kuangalia mzalishaji, tutakuwa hatujatumia akili zetu vizuri, Cha kwanza ni mzalishaji alindwe na atengenezewa mazingira ya kuendelea kuzalisha kwa wingi na kwa faida nzuri ili kumuongezea motisha ili kuhakikisha costastant supply.

Kumbuka sera nzuri ni ile inayobeba watu wengi na kumbuka asilimia sitini ni wakulima, ambao kwa wakati mmoja ni wazalishaji na walaji pia.

Kila taifa linaangalia uzalendo kwanza, tunaangalia sera ipi yenye manufaaa Kwa majority sio minority, ingawa minority nao wanaweza kutafutiwa unafuu pia lakini sio kuumiza majority
Mkuu hujajibu swali lake. Soko huria maana yake ni kuruhusu pia consumers wawe na bargaining power kwa kuangalia masoko mengine duniani. Kwa mfano mchele wa Pakistan. Au mahindi ya Mexico. Unafikiri mkulima wa Tanzania ata-survive?

Watumiaji wa mazao hasa ya chakula ni watanzania pia na inabidi walindwe. Tanzania ni moja ya nchi inayoongoza kwa udumavu wa watoto duniani. Watoto wengi Tanzania hawali chakula cha kutosha.

Njaa siyo mpaka watu wafe, that's the lowest bar ever na kiongozi kuwaambia hamfi njaa ni kiongozi ambaye ame-set standards ndogo sana, he's not revolutionary. Not good enough.
 
Huu ni ujinga unaokaribia upumbavu.

Ni "kiwanda" gani ambacho serikali haihusiki nacho kwa njia moja au nyingine!

Ni shughuli ipi yoyote inayofanywa ndani ya taifa lolote serikali isihusike na shughuli hiyo.

Ni mkulima gani mwenye uwezo wa kusimamia uuzaji wa mazao yake popote duniani bila ya ushiriki wa serikali kwa njia moja au nyingine?
Walanguzi wa mazao ya wakulima leo Bashe anawavisha jina la wakulima?

Bashe anatafuta sifa za kijinga kwa wajinga kama nyinyi.
Ujinga ni kutokujua jambo katika eneo Fulani ,
Nilitegemea baada ya kuelezea hapo juu mfumo WA supply unavyogusa maeneo mengi ungesoma na kulewa hivyo kupunguza ujinga lakini umeamua TU kujibu bila kuelewa mada

Kwenye suala la uchumi sera na aina mrengo wa kiuchumi wa serikali ndo inayoamua nafasi na majukumu ya serikali

Kwenye sera soko huria serikali haipaswi kuingilia soko kwa njia ya kidikteta Bali huacha soko liamue lenyewe , yenyewe hukusanya Kodi na ushuru TU,
Kwenye sera hii serikali Ina njia Moja TU ya kuingilia kwa kununua bidhaa kwa Bei ya soko na kuziuza kwa Bei inayotaka

Unaonyesha kweli una mawazo ya miaka ya sabini ndo maana unaita kwa hasira wafanyabiashara wa kati walanguzi
Suala la middle man kwenye biashara yoyote nimelezea halikwepeki , maana hakuna mkulima anaweza kusimamia gharama na michakato yote kutoka shambani mpaka kwa mlaji peke yake , Endapo atafanya hivyo utaingia kwenye risk kubwa zaidi maana Kila mchakato unahitaji mtaji na maarifa zaidi ya kuusimamia na serikali inahitaji vibali vyake

Hivyo soko lenye bei nzuri ndilo linaamua kiwango Cha faida kwanzia muuzaji wa reja reja jumla na mkulima,
Unapoharibu soko anayeumia zaidi ni mkulima ambaye ni mzalishaji

Mfano Lini serikali ilitangaza bei elekezi kwenye viwanda vya bahresa

Achana na fikra za kizamani za kijinga na za kijamaa zilizokandamiz uchumi wa wakulima na kuua uchumi wa nchi yetu,
Kama unaona wakulima wanafaidi kuchukue hiyo fursa sio kulalamikia serikali iwapangie wakulima bei ya mazao waliyolima wenyewe kwa gharama zao Tena Kwa mitaji ya kuungaunga
 
Wakuu nampongeza mh Bashe waziri wa kilimo kwa mengi aliyoyafanya kilimo, isipokuwa Kwa Leo nampongeza kwa msimamo wake wa kutetea wakulima juu kuuza mazao Yao waliyolima kwa gharama zao kuuza kwenye soko lolote Le ye tija kwao ndani na nje ya nchi.

Wajinga ni wale ambao hawajui faida za hiyo sera wamebaki na fikra za kilimo cha miaka ya sabini. Wanafiki ni wale wanaotambua hizo faida ila wanapindisha ukwell kwa maslahi yao Wakiwemo baadhi ya wabunge waropokaji wasiopenda kupima ukweli wa mambo, mmoja nimemsikia nikashangaa sana.
Naunga mkono hoja, Bashe ni mzalendo toka zamani kabla hajawa Waziri!. Wapinzani msione aibu kushirikiana na CCM kwenye hoja zenye maslahi ya Taifa! Bashe ni mzalendo, aungwe mkono na wote!
P
 
Mkuu hujajibu swali lake. Soko huria maana yake ni kuruhusu pia consumers wawe na bargaining power kwa kuangalia masomMkko mengine duniani. Kwa mfano mchele wa Pakistan. Au mahindi ya Mexico. Unafikiri mkulima wa Tanzania ata-survive?

Watumiaji wa mazao hasa ya chakula ni watanzania pia na inabidi walindwe. Tanzania ni moja ya nchi inayoongoza kwa udumavu wa watoto duniani. Watoto wengi Tanzania hawali chakula cha kutosha.

Njaa siyo mpaka watu wafe, that's the lowest bar ever na kiongozi kuwaambia hamfi njaa ni kiongozi ambaye ame-set standards ndogo sana, he's not revolutionary. Not good enough.
Mkuu nimejibu kwamba sera nzuri ya serikali ni ile inayoangalia maslahi ya watu wengi katika nchi, Leo wakulima ni zaidi ya asilimia sitini ya watanzania achilia mbali wale wafanyakazi wanaotegemea kilimo pia kama njia nyingine ya kuongeza kipato chao

Pili suala la kuagiza nje hiyo ni sera nyingine ya mambo ya nje

kwa serikali ya taifa lolote lazima lilinde wazalishaji wake wa ndani kwanza kabla kuagiza bidhaa nje maana wazalishaji wa ndani ndio wanaoshikilia uchumi kuliko wachuuzi wa wanaogiza bidhaa nje ,
Swali je walaji wangapi wenye uwezo wa kuagiza nje kama sio kutegemea wachuuzi wachache wa kimataifa waongeze import kwa taifa

Hii ni sera ya kimapinduzi itawafanya vijana wengi wakinbilie kwenye kilimo kwa sababu wana uhakika wa soko
hivyo kilimo kuajiri mamillion ya vijana
Kuna pull and push attractive factor
serikali zilizopita zilitumia push attractive factor, mgambo na kuwafokea vijana waende kwenye kilimo kisicho na uhakika wa soko,

But akili kubwa imetumia pull attractive factor ya kutengeneza mazingira ya soko zuri hivyo vijana wengi watakimbilia fursa wenyewe ya kilimo
 
Back
Top Bottom