Per Diem
JF-Expert Member
- Mar 28, 2018
- 2,191
- 3,711
Nimeona mipango ya waziri bashe, mipango imejaa maneno matamu na porojo nyingi. Bahati mbaya wengi hupenda hizi porojo kuliko uhalisia.
Bashe kwenye mipango yake kufikia 2025 wizara imepanga kuwapatia vijana heka milioni 1. Katika hesabu zake bashe anasema kuhudumia heka 1 itagharimu mil 16.7 ambazo roughly ni kama mil 17.
Maswali ambayo hata yeye anapaswa kujiuliza ni je kilimo gani kinaweza kuleta faida ya kurudisha hiyo pesa kwa heka 1?
Ndio maana wengi walikua wakiubeza ule mradi wa BBT maana uhalisia wake ni mdogo sana, Kama mnatumia gharama kubwa hivi hiyo pesa mtarudisha kwa kilimo cha aina gani? Hili kosa pia umelifanya kwenye BBT, gharama ni kubwa mno, Hawa vijana watalima nini ili kurudisha pesa ya uwekezaji? Si ndio baada ya misimu miwili watu wanakata tamaa kila mtu anaenda na njia yake
Ugumu wa kilimo upo hapo, ndio maana tunasemaga kilimo bongo hakilipi sababu unachowekeza na unachopata ni tofauti. Sasa Mimi ninaomba kujua hiko kilimo ambacho kwa heka 1 Kitarudisha zaidi ya milion 17? Ni kilimo gani hiko?
Si ajabu jana niliona nguvu ikitumika kwa vijana mtandaoni kusifia hii hotuba yako, walikuwa busy na hashtags. Hadi nikajiuliza kwa nini hii nguvu ya kutumia watu influential mitandaoni wasifie hotuba yako. Mawaziri wengi wamewasilisha hotuba zao lakini sijaona wakitumia hii nguvu unayotumia. Naamini raisi atakua anajiuliza maswali haya pia.