Waziri apiga marufuku vimini au tight maofisini!

Ghasia bwana, mwanamke toka lini kapendeza bila kuvaa 'tights'. Haya turudishe TANU ilikoanzia maana walitia mikasi sana nguo za watu. TANU hadi CCM wamekua na mawazo ya kimjahdini kama wewe toka enzi hizoooooo na ndio maana nchi yetu ipo nyuma kama ilivyo.

Waziri mzima kama wewe umekaa unaangalia nani ana behind kubwa, nani ana boobs safi...kama ni Lesbian ama kama ungependa kuwa Lesbian naomba vumilia. TANU na CCM waliponzwa na 'fikra sahihi za CHAMA kimoja ama za m/kiti' ndo maana walighafirika, usifuate maovu yao fuata mazuri waliyoyajenga ktk jamii toka uhuru mpaka kwenye demokrasia tulipofikia. Kwa nini uanze kudivide watu kwa kufuata mavazi badala ya kuichukulia jamii yetu ktk mapana yake. Kumbuka si wote tunaoona kua HIJAB yako ni nguo ya heshima.

Acha wanaovaa vibaya wasemwe msikitini/kanisani ama wazazi na dugu zao, rafiki zao ama wapenzi wao, hii sio 1961. Kama sheria haikufutwa ni uvunjaji wa haki na ni wote tunajua kuna sheria nyingi za kikandamizaji TZ hazijafutwa. Tunachotaka ni maendeleo na kukuza uchumi wetu ikiwa ni pamoja na kutengeneza/kuimport/export/kuuza/ kuzawadiana/kuvaa ama kutovaa vimini kwa mapenzi yetu.
 
Hivi GHASIA anataka watu wavae kama miaka ya 1960s. Mimi naona anumwa. Hivi hiyo sheria inasema vipi? Je inaruhusu hijab?? Maana kumbukumbu zangu zinaniambia Mwinyi ndiye aliruhusu hijabu zivaliwe maofisini na mashuleni lakini sidhani kama alibadili sheria hiyo ya 1961. Kweli HAWA GHASIA NI GHASIA TUPU!!!!!
 
Kama kawaida yetu, tunapoteza wakati katika mambo yasiyo na maana. Katika superficialities. Mimi sijaona mini ofisini Tanzania. Ambayo inapelekea swali kuwa nani atatoa vigezo kuhusu nguo ya heshima? Sentimeta ngapi juu ya magoti au chini ya magoti, sentimeta ngapi zibakizwe kati ya mwili na nguo n.k. n.k. Nadhani viongozi katika kila sehemu watoe maagizo ya nguo gani zinafaa kwa usalama wa kufanya kazi. Huwezi kudai fundi mchundo avae tai akiwa kazini. Unachoweza kusema ni kuwa ni lazima avae viatu na miwani ya kinga anapofanya welding n.k. Haya mawazo ya nguo za kubana n.k itatupeleka mahali ambapo uhuru wa mtu utaingiliwa. Hivi kuna taabu gani mwanamke akivaa nguo za kuvutia? Si ndio ubinadamu!hii tendency ya kuoverlegislate itatufikisha pabaya.
 
Kila mtu ana mtazamo wake kuhusu mavazi, na pia anao uhuru wa kuvaa chochote bora tu asitembee uchi. sasa habari ya kutupangia nguo za kuvaa, she is going too far. kashindwa kuangalia jinsi ya kuboresha maisha ya watumishi anabaki anawapangia nguo za kuvaa. hapa si uarabuni.nguo anayoona yweye ni ya heshima inaweza kwangu isiwe ya heshima vilevile. Acha watu walipuke vimini na tops wawe free na roho zao ziwe confortable wakiwa kazini. Kwanihajui kazini pia ni sehemu ya mitego ili watu wapate wachumba waolewe? Anyways, hata hivyo vidume navyo macho yashafubaa kwa ndimu na milipuko ya vimini na tait.
 
Mimi mshamba kidogo. Hivi hivyo vi'top' ndiyo nini? Na hizo 'tight' ndiyo kabisa sizijui. Naomba nifahamishwe.
 
Are you guys kidding me? Where is she coming from? Zamunda? We living on different world, you cant control all the people all the time. I think this need to be resolved in individual company basis. Nadhani makampuni na office husika zinatakiwa kusema what is the dress code, kazi nyingine watu wanavaa casual, na nyingine serious professional. Sasa huyu mama anapojidai headmaster hapo ndio ninapobaki mdomo wazi.

Mtanganyika,

Nafikiri hili anaongelea wafanyakazi wa serikali labda na mashirika ya umma ambayo serikali ndio mwenye mali.

Kama anaongelea zaidi ya hapo matakuwa kavuka mipaka. Lakini hata kwa hao wafanyakazi wa serikali ilitakiwa awape nafasi ya kujadili na kushauriana juu ya dress code makazini maana wakilazimisha kutakuwa na mapambano magumu mno.

Naona mambo mengi yanawahusu wanawake, sisi wanaume je?

Ila kwenye mavazi ukifuata sheria ya mwaka 1961 hapo kutakuwa na kasheshe kubwa sana maana hata Hijab hazikuwepo na jeans lilikuwa vazi la kihuni, lakini leo hata mkuu wa kaya anavaa.
 
engineer
pole ka ushamba mzee mwenzangu.
Nijuavyo miye
vitop ni viblauz vidogodago- vifupi ambavyo huweza kuacha sehemu ya tumbo na kitovu kuwa wazi. Nafikiri vimeitwa vitop kwa sababu vinaishia juu juu havifuniki tumbo lote.

vitait ni vinguo nya kubana haswa.

pedopusha ni kama suruali ila hazifiki chini, yaani kama kaptura inayobana afu ipo chini kidogo ya magoti.
 
engineer
pole ka ushamba mzee mwenzangu.
Nijuavyo miye
vitop ni viblauz vidogodago- vifupi ambavyo huweza kuacha sehemu ya tumbo na kitovu kuwa wazi. Nafikiri vimeitwa vitop kwa sababu vinaishia juu juu havifuniki tumbo lote.

vitait ni vinguo nya kubana haswa.

pedopusha ni kama suruali ila hazifiki chini, yaani kama kaptura inayobana afu ipo chini kidogo ya magoti.

Asante mkuu kwa kunipandisha cheo na kunifahamisha! Mimi TECHNICIAN bwana, wala si injinia. Ma'injinia' wasomi, Mkuu, na mimi shule ilinishinda.

Kwenye vi'top' tatizo ni kuonyesha vitovu? Wahindi wananguo yao inaitwa sari ambayo inaheshimiwa san na inamfunika mama sawa sawa ila sehemu ya tumbo inaachwa wazi ( kwa wale wanaotoka kaskazini ya India). Hili vazi hata Indira Gandhi alikuwa anavaa na hakuona taabu kuonyesha kitovu. Hizo pedapusha naona zinakaribiana na zile tulizokuwa tunaziita 'njiwa' wakati wangu! haya ni mambo ya fesheni na yatapitwa na wakati. Badala ya kulikuza hili suala, Mh. angewaagiza viongozi walio chini yake watayarishe dress codes kutokana na sehemu walipo. Kwa wenzetu huwa wanakuwa na siku ya 'casual' ambapo wale wanaotakiwa kuvaa tai siku hiyo ruksa kuja hata na shorts! Inapunguza stress katika sehemu za kazi. Kwa nini tulazimishe mambo ya mwaka 61. Si tungekazania productivity badala yake?
 
Kwa kweli mimi naona ni bora tu vimini na vitop vipigwe marufuku. Siku hizi kila demu anaonekana bomba kwa ajili ya haya mavazi. Ngo wabakie natural tuone!!
 
Kwa kweli mimi naona ni bora tu vimini na vitop vipigwe marufuku. Siku hizi kila demu anaonekana bomba kwa ajili ya haya mavazi. Ngo wabakie natural tuone!!

Mbona hapigi marufuku mkorogo? Au nayo ni maadili ya Taifa! Nasikia GHASIA ana mkorogo mkali???
 
Haya mambo mara ya mwisho niliona yanakomaliwa miaka ya 70 mwanzoni chini ya usimamizi wa Rashid (Kawawa a.k.a Mhogo Mchungu), hakukuwa na mafanikio bali ilibidi wawaache akina mama wavae jinsi wapendavyo. Baada ya hapo sikulisikia jambo hili mpaka hivi leo. Hivi huyu Mama hajiulizi kwanini watangulizi wake wote walishindwa kukumbushia sheria hiyo? Ina maana wao walikuwa hawakereki na hiyo ghasia ya vimin?

Hapa naona kuna issue nzito zaidi, kwanza hizo nguo anazozisema yeye si ajabu hazipo sokoni (kwenye maduka), nguo nyingi zinanunuliwa kwenye mitumba ambako ndiyo kuna hivyo vimin na vitop ambavyo vimetoka majuu. Hata kama kuna wale wanao nunua nguo mpya madukani bado anaweza asipate specification ambayo Ghasia anaitaka. Labda waanzishe kiwanda chao cha kutengeneza nguo wanazotaka wao, lakini kama ni hizi za kwenye soko huria basi kazi ipo, labda wake zetu tuwaagizie nguo za kutoka uarabuni ambako vimini ni nadra!

Mwisho kabisa kila mwanamke anavaa nguo ambayo anaona inampendeza, sidhani kama ni haki kumlazimisha mwanamke kuvaa nguo ambayo anahisi kwamba akivaa hawezi hata kusalimiwa. Jamani lengo la kuvaa nguo za aina mbali mbali ni pamoja na kupendeza na ndiyo akina mama wana spend asilimia kubwa ya kipato chao kwenye vipodozi, nywele na mavazi, lengo ni kupendeza.
 
Pamoja na uwepo wa sheria hiyo huyu mama ethically anaweza kuonekana yuko wrong na hasa especially kwamba yeye huvaa hijabu sikuzote. Hivyo basi kuna kuladalili tht she's more personal on the issue na ndio maana nimetanguliza neno ethics. Angekuwa yeye ni mpiga vitop, na tights halafu akaamua kubadilika na kuisimamiahiyo sheria angekamata some credits. Anywayz hii ndio bongo. ishu za watu kuondoka ofisini na kurudi kesho au kupiga bia wakati wa lunch na kuendelea mpaka jioni amabazo ni too common kwa watumishi wa umma si priority kwa sasa.
 
sasa hii nikuingilia uhuru wa watu wa mavazi,acha watu wajionee usafiri,kama mtu ana fito aendelee kuvaa hijabu,hiyo sheria ilishapitwa na wakati ndio maana mawaziri waliopita wakaamua kuachana nayo,mbona makanisani watu wanatinga vimini na ibada zinaendelea kama kawaida,mimi naona waziri apiganie masilai ya watumishi.kama yeye amepitwa na wakati aendelee kuangalia kwa macho,
 
sina tatizo na agizo la waziri ..kimesimama kwenye sheria ...tatizo linakuja pale ambapo tunalazimika kuangalia PRIORITIES ..KWENYE WIZARA YAKE ....je tatizo la kushuka kwa moral kwenye utumishi linatokana na mavazi au MOTISHA ..zikiwa pamoja na kupandishwa mishahara ,vyeo,masomo ya kujiendeleza,ajira bila upendeleo,unyanyasaji wa kijinsia,uhamisho unaotenganisha wanandoa ..ets ets...


waziri hana kosa ila inaonekana raia watajiuliza kwa nini ameenda kupekuwa sheria iliyokuwa imeshaota ukungu kabatini....na kupoteza muda kuichimbua huku akiwajibu watumishi wa umma..kuwa tatizo la mishahara si kipaumbele..pia itaonekana kuwa amekuwa biased kukaa kifukua hiyo sheria kwa kuwa ...personel binafsi anapendelea MAVAZI YA STAHA [ndio nilipomaanisha niliposema anaongoza kwa mfano..yeye mavazi yake yote ni ya staha]...raia watajiuliza ,je anataka wote tuvae kama yeye!!!??...waziri aliyekuwepo kabla yake nafikiri ni mpiga vimini...kwani nguo zake nyingi zinafika magotini..na kwa utaratibu wa sasa inabidi zivuke magoti..hapo sasa itabidi hii sheria ianze kuwa implemented bungeni,alafu ije kwa mabinti na dada zetu askari kama traffic na wengine sare zao zinafika gotini ...hazi meet SI UNIT YA GHASIA...

TATIZO lingine wapo watumishi watasema wao hawana pesa ya kununua nguo mpya ..kwani makabati yao yamejaa mitumba yenye vimini ets ..aidha akubali kuwapandisha mishahara wanunue nguo mpya au aagize serikali inunue sare zinazofuata maadili na kuwagawia watumishi...

ndio nataka kuamini kuwa kama sheria hiyo ipo ingetakiwa aifanyie utafiti kwa kufaa wakati tulionao..kama bado haijapitwa na wakati...angeshirikisha na watu wa basata na wadau wengine ili ipatikane consensus ya mavazi ambayo yanaweza kukidhi haja zote za kinadada ..yaani ..KUPENDEZA..na ..HESHIMA...UTANDAWAZI[FASHENI]..UTAMADUNI WA MTANZANIA.
 
Mimi naona this is absolutely political issue! Huyu Mama utendaji wake unasuasua, hivyo ameanza kuvamia ishu ambazo ziko off point. Kama anataka watumishi wa serikali wafuate maadili aanze kwanza kuzungumza kuhusu work ethics (watu wanatimuka saa 10 utafikiri akibaki hata dk 5 extra atakufa! People hawana morali ya kazi ktk public offices), haya tuje kwenye rushwa hiyo ndiyo kabisaaa!
Sasa kuzungumzia sheria ya mwaka 1961 is like searching desperately for some straw to clutch at. That law ilikuwepo hata enzi za Mary Nagu mbona haikutangazwa rasmi. Mimi nimetembelea ofisi nyingi na mashirika na sijawahi kuona tops au vimini. And by the way what constitutes 'kimini'? Je kama sketi imefika just above knees ni mini? That is standard siku hizi! Au mini ikifika kwenye mapaja, au ikifika just below the bum?!
Sasa mama anavaa kama ninja si atakwambia sketi ikifika magotini ni mini!
Dress Code is something that doesn't need to be in law, it is a code. And there are no 'penalties' for not dressing just chastizing!
She should concentrate ont he reforms waliotangaza watafanya badala yake tunaona mambo yako vilevile!
 
..SUSUVIRI well said ..ukijaribu kuangalia uvaaji ..watumishi maofisini tanzania wanajitahidi sana kuvaa nguo za heshima..mimi sijapata kuona mtumishi aliyevaa nguo inayozidi juu ya goti..wanajitahidi sana kuvaa ..ukitaka kupagawa nenda southafrica,botswana ets ..
 
Hizi ni fujo au ghasia ambazo mwisho wake zinatupumbaza tuache mambo ya maana na kufuatilia huyu kavaa nini sijui nichukue katua gani ...nk Mimi nimewahi kuona mvaa hijab na kanzu lake lakini kumbe ndani hana nguo yoyote. Upepo ulimuumbua sasa nguo ya heshima ni ipi? Ni vema tukawa wawazi kama nchi inageuka kuwa ya kiislamu kwa gia hiyo ya mama ghasia au fujo itakuwa matatizo humu nchini. Zamani tulivaa bugaloo na raizoni viko wapi sasa. wakati ule vijana wa TANU/ CCM wanatembea na makasi ya kukata nguo za mabinti wanaovaa nguo fupi. Tunarudi kulekule. Haya yanapita. Shughulikia mambo ya maana ewe waziri wa ghasia.
 
Ilitakiwa Waziri atuambie kuwa kuna sheria ambayo imepitwa na wakati na mipango yake ya kuiweka vizuri ili iendane na wakati. Na sio kutusomea kwenye "archives". Kama swala ni kusoma sheria basi anyone can be a minister, waziri anatakiwa atuambie updates zake. Hii serikali sijapata kuona. JK naye akisikia hiyo na alivyomvivu wa kufikiri ataunda tume ya kuchunguza.
 
Kwanza kabisa hili ni suala la utendaji kwa hiyo angemwachia Katibu Mkuu Kiongozi atoe maagizo kwa hao waliochini yake.
Pili kwa mheshimiwa kulifanya suala la siasa itabidi kama kawaida yetu kuandaa makongamano kuwa'sensitize' wahusika wote na watoa mada watatoka majuu kutueleza namna ambavyo mavazi kama haya yatawafanya watu waingie kwenye mambo ya ufisadi ili wawanase wanaovaa hivyo vi'top' na kadhalika na kadhalika. Halafu viongozi wataanza kuzungikia ofisi zao (za mjini mpaka mikoani) wakiwa na tape measure na chupa za soda kuhakikisha kuwa hakuna kitop na kitait kinachokatiza. Of course, kabla ya kufanya hivi itabidi wafanye study tour majuu kujifunza kutoka kwa wenzetu!
Mbona Condi anavaa vi'mini'na hakuna ambaye amemshutumu kuwa anafanya hivyo kuwachanganya wenzie? Au ndiyo maana Bush achezi mbali? Mimi naona ni kututukana wanaume ati tukiona mapaja tu basi hatuwezi kujizuia! Tumekuwa mbwa? Kuna vitu vya muhimu zaidi vya kufanya kuliko hili. Hivi hili agizo litawabana na wale wanaotembelea hizo ofisi?
 
Mi nafikiri swala la kimini au kichupi litazamwe kwa style nyingine. Kuna wadada ambao wanavaa vimini lakini wanashangaza pia as utawakuta wakiwa wamekaa kwenye daladala, utakuta wanavutavuta sketi chini ili mapaja yasionekane na abiria. Hapa huwa nachoka zaidi. Kama umepanga kula mini, kamua mini, wacha watu waone usafiri hata kama ni mchafu..!! Kama huwezi ligi za mini, tupa kwenye dust bin na kuendelea kukamua ijabu. Au mwasemaje wana JF..!!..??
 
Back
Top Bottom