Wazee wa Madrassa wampiku Mama Samia Suluhu?

Jirani upo vizuri sana hajat FaizaFoxy .
Kongole sana na Mungu akubariki.
Tumsaidie Mh. Mama Samia Suluhu Hassan kuwatoa Watanzania katika lindi la ufukura.
Nifahamishe huo ujirani wetu upoje? Sikufahamu.

La Kumuunga mkono Mama Samia halina budi. Tuanze kufanya sisi tusingojee serikali itufanyie.

Naona wazee wa Madrassa wanafanya kweli na hawangoji Serikali iwafanyie. Tunawaombea serikali iwaone na iwa boost au japo waandishi wa habari muwaone mkajionee wanachofanya muwa boost kwa kuwatangaza kwa faida ya jamii.
 
Mambo mapya kutoka darsa la FaizaFoxy:

Kila rais mwislamu anapokuwa ikulu, siasa kali huanza chokochoko zao. Mihadhara ya kukashifu imeshaanza mitaani na redioni. Huu ni udhaifu kubwa
Acha roho mbaya wewe,, mihadhara ajakatazwa mtu kufanya as long as uwe na kibali tu,, uwe mpagani,rastafari,budha etc. Unaonyesha chuki za wazi kabisa kisa dini tu ya mkuu wa nchi. Ongoza wewe basi na chuki zako fala wewe.
 
Hilo linahusiana nini na mada ya uzi huu?
 
Acha roho mbaya wewe,, mihadhara ajakatazwa mtu kufanya as long as uwe na kibali tu,, uwe mpagani,rastafari,budha etc. Unaonyesha chuki za wazi kabisa kisa dini tu ya mkuu wa nchi. Ongoza wewe basi na chuki zako fala wewe.
Mihadhara inayoshambulia na kukashifu imani za wengine huibuka pindi rais akiwa muislamu, hiyo ndiyo hoja yangu.
 
Na hizo siasa baridi ndio zipi?

Unamfahamu au umewahi kumsoma Ole Sabaya na Bashite? Hao ndio siasa zao ni baridi?

Wazee wa Madrassa wanafanya kweli, hilo hukuliona?
Faith without reason....
 
Leo nimezikuta habari za Mzee wa Madrassatul Abraar ambae pia ni member wa JF kwenye group la kuwezeshana ujenzi zilizonifurahisha sana na nikajiuliza, hawa wazee wa Madrassa wamempiku hatua moja Mama Samia Suluhu?

Mama Samia Suluhu juzi alipokuwa akiwaapisha Makatibu Tawala alisema "asilimia 46" ya aliowaapisha ni wanawake. Mama alinifurahisha sana sana kuona kuwa hatutupi wanawake wenzake.

Kilichonifurahisha zaidi ni habari iliyotumwa leo kwenye group la whatsapp na telegram kuwa wazee wa madrassatul Abraar ni muda sasa wameanzisha mpango wa kuwawezesha wanawake kabla ya Mama Samia Suluhu. Wanawawezesha kwa kuwwfundisha fani na taaluma mbali mbali za kazi kwa vitendo, hata mtaa wao unaitwa Vitendo.

Ya leo waliotuma ilikuwa ni kina mama waliojifunza ujenzi kuanzia hapo hapo Madrassatul Abraar, msimamizi wao (Mke wa Mzee wa Madrassa) yeye pia kajifunza usimamizi wa ujenzi hapo hapo Madrassa na mteja wa nyumba wanaoijenga ni mwanamke pia.

Mwenye nyumba hiyo pia nampongeza sana kwa kujitolea kuwakabidhi ajengewe nyumba yake kwa roho nyeupe kina mama hao ambao bado wanapata uzoefu wa ujenzi. Chini ntapandisha video clip.

Hongereni sana wazee wa Madrassatul Abraar, Hongera Bi Samira uliejitolea ujengewe bila hofu ili kina mama wenzio wapate uzoefu,

Jioneeni team ya kina mama ikiwa kazini...

Waandishi wa habari mko wapi mambo mema kama haya yanafanywa na wazee wa madrassa hamyatangazi? Hawa Madrassatul Abraar nimepitia hapa JF nimeona wamebuni mpango wa kuwezeshana wanaouita Nyumba kwa Wote ambao wanatamba kuwa haujawahi kutokea duniani, cha kushangaza si wanasiasa si waandishi wa habari wanaokwenda kuona mipango hii ambayo wangewawezesha hawa wazee ingefanywa kitaifa kabisa tena kwa ufanisi mkubwa kabisa.

View attachment 1808538
Kumbe upoooo

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Hakuna siri, ukweli ni kuwa Tanzania ilikuwa ya vitisho sana awamu iliyotutoka.

Ukienda huku Makonda, ukienda kule Sabaya ukirudi unatumbuliwa hata kama hauna jipu. Mara una kesi za uhujumu uchumi mara una kesi za kutakatisha fedha, ohoooooo.

Ikabidi wengine turudi zetu kwenye kwenye barafu tupoe kidogo.

Mama Samia katutoa hofu. In shaa Allah aishi kama jina lake "msikivu".
We si ulikuwa mfuasi wa mwendazake
 
Safi ila ili waende mbali zaidi kwenye mafunzo ya kidunia na kujikimu wasichague imani..., hata akija mpagani kama tu anataka kujifunza kusuka au kutengeneza ugoro na akaribishwe
 
Mihadhara inayoshambulia na kukashifu imani za wengine huibuka pindi rais akiwa muislamu, hiyo ndiyo hoja yangu.
Mihadhara ni ya kupuuzwa tu, ukiendeleza kwenda kuisikiliza ndiyo itakukwaza. Waache waendelee ali mradi wanayoyafanya yapo kisheria bila kukashifu dini zingine.
 
Leo nimezikuta habari za Mzee wa Madrassatul Abraar ambae pia ni member wa JF kwenye group la kuwezeshana ujenzi zilizonifurahisha sana na nikajiuliza, hawa wazee wa Madrassa wamempiku hatua moja Mama Samia Suluhu?

Mama Samia Suluhu juzi alipokuwa akiwaapisha Makatibu Tawala alisema "asilimia 46" ya aliowaapisha ni wanawake. Mama alinifurahisha sana sana kuona kuwa hatutupi wanawake wenzake.

Kilichonifurahisha zaidi ni habari iliyotumwa leo kwenye group la whatsapp na telegram kuwa wazee wa madrassatul Abraar ni muda sasa wameanzisha mpango wa kuwawezesha wanawake kabla ya Mama Samia Suluhu. Wanawawezesha kwa kuwwfundisha fani na taaluma mbali mbali za kazi kwa vitendo, hata mtaa wao unaitwa Vitendo.

Ya leo waliotuma ilikuwa ni kina mama waliojifunza ujenzi kuanzia hapo hapo Madrassatul Abraar, msimamizi wao (Mke wa Mzee wa Madrassa) yeye pia kajifunza usimamizi wa ujenzi hapo hapo Madrassa na mteja wa nyumba wanaoijenga ni mwanamke pia.

Mwenye nyumba hiyo pia nampongeza sana kwa kujitolea kuwakabidhi ajengewe nyumba yake kwa roho nyeupe kina mama hao ambao bado wanapata uzoefu wa ujenzi. Chini ntapandisha video clip.

Hongereni sana wazee wa Madrassatul Abraar, Hongera Bi Samira uliejitolea ujengewe bila hofu ili kina mama wenzio wapate uzoefu,

Jioneeni team ya kina mama ikiwa kazini...

Waandishi wa habari mko wapi mambo mema kama haya yanafanywa na wazee wa madrassa hamyatangazi? Hawa Madrassatul Abraar nimepitia hapa JF nimeona wamebuni mpango wa kuwezeshana wanaouita Nyumba kwa Wote ambao wanatamba kuwa haujawahi kutokea duniani, cha kushangaza si wanasiasa si waandishi wa habari wanaokwenda kuona mipango hii ambayo wangewawezesha hawa wazee ingefanywa kitaifa kabisa tena kwa ufanisi mkubwa kabisa.

View attachment 1808538
Naona Mama Samia baada ya kumaliza kusimamisha serikali mpya sasa umepata tena wasaa wa kurudi na kujumuika na sisi hapa JF
 
Back
Top Bottom