Wazee wa Madrassa wampiku Mama Samia Suluhu?

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,521
2,000
Leo nimezikuta habari za Mzee wa Madrassatul Abraar ambae pia ni member wa JF kwenye group la kuwezeshana ujenzi zilizonifurahisha sana na nikajiuliza, hawa wazee wa Madrassa wamempiku hatua moja Mama Samia Suluhu?

Mama Samia Suluhu juzi alipokuwa akiwaapisha Makatibu Tawala alisema "asilimia 46" ya aliowaapisha ni wanawake. Mama alinifurahisha sana sana kuona kuwa hatutupi wanawake wenzake.

Kilichonifurahisha zaidi ni habari iliyotumwa leo kwenye group la whatsapp na telegram kuwa wazee wa madrassatul Abraar ni muda sasa wameanzisha mpango wa kuwawezesha wanawake kabla ya Mama Samia Suluhu. Wanawawezesha kwa kuwwfundisha fani na taaluma mbali mbali za kazi kwa vitendo, hata mtaa wao unaitwa Vitendo.

Ya leo waliotuma ilikuwa ni kina mama waliojifunza ujenzi kuanzia hapo hapo Madrassatul Abraar, msimamizi wao (Mke wa Mzee wa Madrassa) yeye pia kajifunza usimamizi wa ujenzi hapo hapo Madrassa na mteja wa nyumba wanaoijenga ni mwanamke pia.

Mwenye nyumba hiyo pia nampongeza sana kwa kujitolea kuwakabidhi ajengewe nyumba yake kwa roho nyeupe kina mama hao ambao bado wanapata uzoefu wa ujenzi. Chini ntapandisha video clip.

Hongereni sana wazee wa Madrassatul Abraar, Hongera Bi Samira uliejitolea ujengewe bila hofu ili kina mama wenzio wapate uzoefu,

Jioneeni team ya kina mama ikiwa kazini...

Waandishi wa habari mko wapi mambo mema kama haya yanafanywa na wazee wa madrassa hamyatangazi? Hawa Madrassatul Abraar nimepitia hapa JF nimeona wamebuni mpango wa kuwezeshana wanaouita Nyumba kwa Wote ambao wanatamba kuwa haujawahi kutokea duniani, cha kushangaza si wanasiasa si waandishi wa habari wanaokwenda kuona mipango hii ambayo wangewawezesha hawa wazee ingefanywa kitaifa kabisa tena kwa ufanisi mkubwa kabisa.

 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,367
2,000

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,521
2,000
Wana JF waliuliza sana lakini mkurugenzi hakupata wasaa wa kujibu kiu wa waliotaka kujiunga na mradi huu. Mkurugenzi aje tena maana inaonesha mradi una potential kwa jamii ya kiTanzania ijiinue, hivyo aatoe ufafanuzi "Social Economic Empowerment Program,." Madrassa Yabuni Mpango wa Kijamii wa Kuwezeshanana kiuchumi. Haujawahi kutokea, duniani

Social Economic Empowerment Program,." Madrassa Yabuni Mpango wa Kijamii wa Kuwezeshanana kiuchumi. Haujawahi kutokea, duniani​

In shaa Allah tuombe Mungu na mimi ntautuma ujumbe wako kwenye telegram group la Abraar Nyumba kwa Wote, kama hajasoma hapa atauona kwenye group. Au jiunge kwenye hilo group utapata majibu
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,521
2,000
Shikamoo faizafoxy

Asalam alyekum

Nawapeni pongezi
Marhaba.

Wa Aleykum salaam.

Hiyo Madrasaatul Abraar inabidi ipongezwe kitaifa kwa mpango wao wanaouita Abraar Nyumba kwa Wote. Wanatamba kuwa kupitia kwao unaweza kuanza ujenzi kwa Shillingi 2,500 tu. Inashangaza.

Wana uzi wao humu JF unaongelea hilo la kuwezeshana ujenzi. Binafsi nawapa pongezi sana tena na naahidi kuwatembelea ntapokuwa huko.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,269
2,000
Leo nimezikuta habari za Mzee wa Madrassatul Abraar ambae pia ni member wa JF kwenye grup la kuwezeshana ujenzi zilizonifurahisha sana na nikajiuliza, hawa wazee wa Madrassa wamempiku hatua moja Mama Samia Suluhu?...
Binafsi niwapongeze kwa kupiga hatua. Mafanikio hayaepukiki sehemu yoyote yenye ushirikiano.

Ila sijaelewa ni kwa vipi hao wanawake wamempiku Rais Samia.
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,521
2,000
Huyu bibi tulimmis sana. Ama kweli JPM aliwapoteza wengi
Hakuna siri, ukweli ni kuwa Tanzania ilikuwa ya vitisho sana awamu iliyotutoka.

Ukienda huku Makonda, ukienda kule Sabaya ukirudi unatumbuliwa hata kama hauna jipu. Mara una kesi za uhujumu uchumi mara una kesi za kutakatisha fedha, ohoooooo.

Ikabidi wengine turudi zetu kwenye kwenye barafu tupoe kidogo.

Mama Samia katutoa hofu. In shaa Allah aishi kama jina lake "msikivu".
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,521
2,000
Binadamu wote sawa regardless ya jinsia at least kwenye uwezo wa kufanya maamuzi na kuongoza...
Kwa clips za audio na video na maelezo wanayotoa hao wazee kwenye group lao na hata humu JF wana uzi wao, wanaonesha wanafanya kweli. Mliopo karibu kwanini hamuwatembelei na mkawapa na hayo mawazo mnapoona hawaelekei?

Lakini niwaonavyo na jinsi wanavyotamba na ubunifu wao kuwa ni wa kipekee duniani, hadi sasa sijaona aliewapinga, nahisi badala ya kuwapelekea jipya wao mtaenda kuchota mapya mengi kwao.
 

kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
3,440
2,000
Leo nimezikuta habari za Mzee wa Madrassatul Abraar ambae pia ni member wa JF kwenye grup la kuwezeshana ujenzi zilizonifurahisha sana na nikajiuliza, hawa wazee wa Madrassa wamempiku hatua moja Mama Samia Suluhu?...
Makosa mengi sana yasahihishe la sivyo utaambiwa shule ulienda kusomea nini
 

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
8,641
2,000
Leo nimezikuta habari za Mzee wa Madrassatul Abraar ambae pia ni member wa JF kwenye grup la kuwezeshana ujenzi zilizonifurahisha sana na nikajiuliza, hawa wazee wa Madrassa wamempiku hatua moja Mama Samia Suluhu?...
unasemaje kuhusu kipenzi chako jpm
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom