Matukio kama hayo yanatokea kwa wingi sana zanzibar kwa tanzania bara yanatokea ila si sana kivile kwa sababu sheria kidogo inafanya kazi,Visiwani kule tatizo lake kubwa ni kulindana bado wanaishi na ile mifumo ya kizamani, yaani mtu akifanya kosa mfano kabaka unakuta suala linafikishwa polisi baadae wahusika wanaelewa huko mtaani mfano kama ni mtoto aliyebakwa unakuta mzazi wa mshitakiwa na mzazi wa mshitaki wanaelewana kama kesi ilitakiwa iende mbele zaidi sasa hata polisi wanashindwa kuifuatilia kutokana ns kukosa ushirikiano na upande stahiki,Au utakuta bado wana yale huyu ni mtoto wa fulani,mzazi wake tunamjua muache tutaongea na mzazi wake.Sasa ndiyo maana matukio yanakuwa hayaishi sana.Kwa tanzania bara hasa wazazi wakiuwasha moto hilo unalo kweli kama kwenda ndani utakwenda tu.Ukiacha matukio ya ajabu ajabu kama ya huko mikoani na imani za ushirikina ila kwa bara kesi hizo zimepungua mno.Na hilo la ushirikina ni ukosefu wa elimu stahiki tu kama itafika huko mauji yakishirikina yatapungua kiasi fulani japo itakuwa ngumu kuyamaliza kabisa.