Anapiga weee bado anakuta macho makavu, nikimchoropoka hanioni naenda kumchukua bibi aniombee msamaha, anamwmbia bibi ondoka naye simtaki, kama atarudi kwangu labda Mimi siyo wa kwa ....... Atataja ukoo wa kwao, bibi ananinong'oneza we nenda endelea na majukumu ya nyumbani, ndiyo nishasamehewa hivyo, na hapo hapo anasahau kila kitu, hanaga kuweka kitu moyoni.
Nakupenda sana mamangu.
Na kunipiga kote lakini hajawahi kuwaficha wengine kuwa ananipenda kuliko wao wote hadi huwa wakubwa na wadogo zangu wanajisikia vibaya. Sahivi wameniachia Mimi ndiye nihangaike naye, nami nafurahia, nalipa fadhila ya kupendwa, bila yeye sidhani kama ningekuwa hivi nilivyo leo, am proud of her kwakweli.